Hapa jirani yangu pana nyumba haijawahi kukaliwa na watu tokea ikamilike kujengwa. Ni mwaka wa 10 huu, mpaka geti linaanza kuoza. Nijitwalie?

Miaka ya 2004 kuna jamaa maeneo ya Karakata (Kipawa) alijimilikisha kiwanja. Yy aliuziwa kiwanja akajenga akahamia..Kulikuwa na kiwanja Pembeni yake akawa anapanda matembele kiaina na kufugia vifaranga mchana ( ile style ya kuzungushia net). Hakuwahi kumuona mmiliki ila majiran wake waliwahi kumuona (Mama). Aliendelea kulihudumia kama lake kwa kisingizio kuwa likiwa pori linaweza kumletea nyoka/Nge. Alijiaminisha endapo mmiliki atajitokeza hatalingangania eneo la watu.
Baada ya kuona imeisha kama miaka 7 hivi hakuna anaekuja kulalamika kuwa eneo lake limevamiwa, Akawa anawadanganya majirani zake kuwa ameuziwa lile eneo na huyo Mama. Alifanya hivyo baada ya kuhisi huenda akajitokeza jiran anaejua historia ya hilo eneo akajifanya lake.

Hakutaka kulijenga mapema kuogopa hosara, alizungushia ukuta wa tofali pamoja na nyumba yake.

Kwa sasa sijui nini kinaendelea karibia miaka 20
 
Hii ni dhuluma mali sio yako,hao ndgu zake hata wamgeuza ni sawa mana mali ya ndgu yao
 
Mimi kuna wakati karibu nijitwalie jengo la Naura Springs Hotel kwasababu ya kukaa miaka mingi hakuna mwendelezo yaani niko shule ya msingi hadi namaliza sekondari hakuna kitu. Kumbe lilikuwa na mgogoro
Labda naura ya kazimkazi
 
Unaishi kwa kukiogopa kiumbe kinachotakiwa kukuheshimu!

Tupo mbali Sana..!
 
Wewe ni mwizi
Kaa hivyohivyo..sio mimi mimi nimenunua sijataifisha..kiufupi wao walinunua na mm nilinunua...mwenye eneo ndio alikuwa tapeli maana aliwauzia akaona miaka inaenda hawafanyi kitu akaniuzia na mimi pia bila mm kujua kama lilishanunuliwa
 
Mtego wa P diddy huo sasa jichanganye
 
TRUE STORY... Kuna mradi mmoja ulikuwa wa Viwanja Elfu 2 nadhani wengi mnaukumbuka... KIBADA,KISOTA,MBWENI,BUNJU,MIVUMONI,,TUANGOMA,MWONGOZO nk.Moja eneo tajwa Ardhi ilitenga viwanja kama 50 hivi kwa ajili ya NATIONAL HOUSING CORPORATION. (NHC)Sasa NHC wakadai hawaitaji mradi mpya Dar kwani waliyokuwa nayo enzi hizo 2000es ilikuwa mingi. Vikabaki Iddle Maafisa wa Mradi wakagawana wee... kisha wakaanza kuwauzia watu kwa Bei elekezi kisha wanaongeza cha juu Mfano kiwanja Sq.1500 Bei elekezi ni 2M bei ya soko enzi hizo watakuuzia 6M... sasa kuna jamaa alikuwa navyo 7 akauza kama vi 3 vikabaki vi 4...
Kwa bahati mbaya hakumuonyesha mtu yeyote... na wenzake pia walikuwa busy maeneo mengine... akajq kupata ajali ya Gari mwaka 2009.

Hivyo basi viwanja vinne vimepotea. Alikuwa bado ajaoa ila alikuwa na Mchumba Mjamzito.
 
Hahaha
 
Duuh zamani sana
 
Kwamba umeokota nyumba?
 
Duuh hatari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…