Hapa Kazi Tu (HKT) kiwe chama kipya cha kisiasa Tanzania kitakachoenzi falsafa na maono ya Hayati Dkt. Magufuli na kiwe tegemeo la Watanzania

Huyo ambaye mnatumia mtazamo wake hakuwahi kuamini kuhusu katiba mpya, yeye alijiona mungu mtu. Katiba aliifanya atakavyo

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Falsafa ya Kimagufuli inaamini China ni rafiki, adui, au wa kuchukuliwa kwa tahadhari?
 
hamna mahali mtafika na hiyo cult group.
Unakuja kwa mihemuko ya hovu, wenzako wanakuja na blessed strategy. Sasa utajua kati ya fisadi na mtetezi wa wanyonge nani ni rafiki wa Mungu. Mungu na watenda haki, shetani na wahuni.

Naomba anayejua zaidi kuhusu hiki chama kipya azidi kutujuvya tafadhali.
 
Sasa unaanza kuongea kama mtu, hivi nini kilichowafanya muwe Wanyama kwa kuunga mkono ukatili dhidi ya Watanzania wenzenu? Magufuli alikuwa na nafasi ya kuwa Rais bora kuwahi kutokea nchi lakini nafasi hiyo aliichezea mwenyewe ikamponyoka. Wakati anaingia madarakani asilimia zaidi ya 90 wakiwemo wanasiasa waliamini atatenda haki kwa vile hakuwahi kuziishi siasa za KiCCM za hila na hinda. Lakini ghafla akajiunga na ukandamizaji na kuwa dikiteta asiyependa kukosolewa. Kwa sasa ukitaja jina MAGUFULI mbali ya mazuri yake kama ulivyosema, lakini tafsiri ya haraka kwa Mtanzania inayomjia akilini ni Ukatili, Uuaji, Utesaji, Ubambikiaji kesi na mabaya yanyofanana na hayo halafu ndo afikirie mazuri machache kama ujenzi wa miundombinu, uboreshaji wa utumishi nk.
 
Kwanini usikiite "Hapa Kinyesi Tu" ili angalao upate Wateja wa Komoni?
 
Kiwe tegemeo la Watanzania!! Ajabu kabisa. Au unamaanisha kiwe tegemeo la Watanzania wajinga, washamba na wanafiki?
 
Nipende kuunga hoja hili jambo.
Inatakiwa tuanze mchakato wa kukisajili hiki chama yasiishie kuwa maneno ya mtandaoni.
Mkuu uwe mwenyekiti 😊☺️
 
Kuzilinda rasilimali halafu ukawa huna uwezo wa kuziendeleza ni ujinga mwingine wa kiwango cha juu sana. Ni akili zile zile za kuwaogopa Wakenya kwa kusema kuwa jumuiya ya afrika mashariki inakwenda kuwapa ardhi yetu, wakati sehemu kubwa ya ardhi hatuna uwezo wa kuiendeleza!!.

Akili za kujivunia rasilimali wakati huna teknolojia pana ya kuiendeleza ni sawa na mswahili fulani anayemiliki shamba la heka mia la minazi halafu hana jeuri ya kuchukulia mkopo benki wala hana ndugu wa kushirikiana nao wenye maarifa ya kulifanya liingize kipato.

Hata hicho kiwanda cha kuchenjua dhahabu kilichofunguliwa na Rais Mwanza ni cha ubia kati ya serikali na wawekezaj wa kigeni. Liganga na Mchuchuma inakwenda kufunguliwa ili nchi iweze kuendelea.

Dhana za mabeberu na malengo yao mabaya kwetu ni za kihisia zaidi, ukweli ni kwamba hakuna mwenye ujanja wa kuzitumia rasilimali alizonazo pasipo muingiliano na watu wa mataifa mengine. USA na jeuri aliyonayo anamtegemea Mchina kibiashara. Muingereza na ujanja wake wote anajuta kuanzisha michakato ya BREXIT kagundua anawahitaji wazungu wengine wa Ulaya kuliko alivyodhania awali.

JPM nilimkubali, lakini hakuwa malaika na ushahid wa ubinadamu wake kila siku unaanikwa hadharani. Namuunga mkono Rais Samia na naiunga mkono Tanzania yenye umoja wa kitaifa.
 
Hahah

Nimeona clip anasema vyombo vya habari vya nje vinakuja KUM BRAND,amekuwa bidhaa?
 
Kisajilini haraka tuanze kupambania katiba mpya.

Au kwenu katiba iko poa tu.
Katiba mpya inabidi ifanyiwe mabadiliko makubwa sana ya kubadilisha mfumo wa utawala ambao utaleta nguvu kwa wananchi ili iwe Rahisi kwa viongozi kuwajibishwa kwa makosa waliyoyafanya wakiwa madarakani lkn pia katiba mpya ijikite kutatua matatizo ya msingi yanayoisumbua nchi hiii kwa mfano Rushwa, ifikie hatua Rais wa nchi akikosea awajibishwe na kuondolewa madarakani, uwepo uwazi wa kiwango cha hali ya juu kwenye mikataba kifupi tunahitaji mabadiliko yenye kuwanufaisha Watanzania
 

Naamini kuna umuhimu mkubwa wa chama kipya na Katiba mpya.

Chama kipya kiwaunganishe Watanzania wote bila kujali, dini, kabila, jinsia, ukanda. Kiwe chama cha kitaifa.

CCM inahitaji changamoto wa cha imara, madhubuti kitachosimamia haki, kupinga rushwa, upigaji, vyeo kutolewa kwa undugu, udini, ukabila, vitolewe kufuata (merits), mtu ana vigezo.


Katiba Mpya ni muhimu, hapa inabidi kuwashirikishs wadau wote wa vyama vyote including CCM, viongozi wa dini zote, tassisi zote.

Katiba mpya itasaidia:-
1. Mikataba yote mikubwa iwekwe wazi all terms, conditions, small prints.

2. Kuondoa kinga za kutoshtakiwa. Kiongozi yoyote aweze kushtakiwa na ikithibitika alivunja sheria, afungwe. Aweze kushtakiwa hata baada ya muda wake wa uongozi (Retrospectively)

3. Mahakama ziwe huru kusimamia haki na sheria bila kujali cheo, pesa. Zibadilike kuweza kutenda haki kwa maskini, wajane, yatima. Kila mtuhumiwa apewe wakili kwa wale wasiojiweza.

Dhamana iwe haki ya msingi kwa watuhumiwa wengi except (kesi za mauaji, ubakaji, uhujumu uchumi, ugaidi, flight risk)

4. Bunge liwe huru, kuisimamia serikali na kujadili mikataba kwa uwazi, kuhoji kwa staha.

5. Tume huru ya uchaguzi ni muhimu. Ruzuku kwa vyama zipunguzwe wapewe vyama vipya tu. Kwa chama kikongwe kama CCM ziondolewe kabisa. Wabunge wapunguzwe. Posho, mikopo zipunguzwe.

Mawaziri, wabunge, Wakuu wa Mikoa, wilaya, kata, watendaji wawe watu wenye weledi, uzoefu, maadili, waadilifu, waaminifu.

Wachaguliwe kutokana na kazi walizozifanya huko nyuma. Sio lazima wawe wanachama kwenye chama kinachoongoza serikali.
 
Chama kile kilitengenezwa na kina msoga, na akina miebe kwa kusudi la kudhoofisha upinzani. Hiki kipya kisiwe na element za ubinafsi ama ujasusi wa mafisadi.
Hiki Chama kitaachana na mapungufu ya vyama vyote ikiwemo CCM na kuchukua mazuri ya vyama vyote, kitaangalia uhalisia wa shida zinazowakabili Watanzania kwetu Tutapanua na kuwa na tafsiri sqhihi ya Kiafrika ya haki za binadamu lzma tujue kuwa haki za msingi za binadamu ya kwanza ni haki ya kuishi, haki ya kupata huduma bora za kijamii
 
Mnataka muenzi faisafa ya kuteka na kupiga watu risas kukwiba pesa za wafanya biashara na kuwa ben SAA 8 wanaowapinga sio?

Bali wafanyabiashara matapeli kama kina ruge wakishirikiana na viongozi waongo, wasanii, wanafiki wakubwa na matapeli kuiba kodi za walalahoi wa nchi hii kupitia mikataba ya kiwizi wizi na kifisadi ndio sawa kwako. Safari hii mtashaa uzalendo uliojengwa na JPM kwa miaka 5 aliyo kirimiwa na Mungu wa Mbinguni atuongoze utawatafuna mmoja mmoja.
 
Kuwa na chama kipya ni jambo ambalo nangojea kwa hamu.
Alafu kuonyesha uzalendo kuwa strategies za bora za uongozi ili wapendwa rushwa na na viongozi wasiokuwa na uzalendo wasipate fursa na wasitamani kuingia.

Na hili je ni lini litatukia ni bora mikakati bora ikawekwa. Tuanze kwa vitendo, tusingojee uungwaji mkubwa mtandaoni. Twende field tukaelimishe wananchi dhamira ya chama. Upungufu uliopo kwa vyama vya sasa. Na nini dhamira yetu na maono tuliyonayo.
 
Uthubutu kwa kutopenda kukaguliwa ? Na akikaguliwa basi na ukweli ukasemwa kuhusu ufujaji wake wa pesa za walipa kodi basi CAG anatafutiwa zengwe!? Kwe alikuwa na uthubutu wa utekaji na unyang'anyi.
 

Kabisa,Imefikia sehemu lazima Tanzania iwe na chama kingine imara, cha kitaifa. Macron alianzisha chama kipya akavishinda vyama vikongwe Ufaransa ndani ya miaka mitano.

(Labour party) Chama cha wafanyakazi UK. Kilipoanzishwa kilikuta vyama vikongwe viwili Liberals and Conservatives.

Ndani ya miaka michache wakaleta mageuzi makubwa sana nchini Uingereza. Kama elimu bure, Afya (kutibiwa bure), Makazi kwa kila mwananchi, Pesa za kujikimu usipokuwa na kazi, minimum wage, usawa kwa wanawake, maskini, kujenga miundombinu mingi shule, hospitali, barabara, viwanda, reli nk ikatengeneza ajira nyingi sana kwa watu wao.

CCM siku hizi sio tena chama cha mapinduzi ni chama cha wenye nguvu, matajiri, wachache,elites.

We need proper, credible, serious altenative party to the goverment with serious policies and candidates to eady the country from day one.
 
wenzetu wanaanzisha chama serikali ikiwa transparency. wakiwa na taasisi imara kabisa ndio maana wanafanikiwa.

hapa nyumban hatuna taasisi imara.. kiasi kwamba kila chama kinachoanzishwa kinaonekana halina lolote mbele ya ccm. why?
taasis hizi zimeruhusu ccm kujipenyeza kwenye idara nyeti nchini. matokeo yake ni kuwa chama chochote kinaochojarib kuwa threat kwa ccm.. serikal huwa inatumia taasisi hizo kukigandamiza.

kwanza reverse hiyo effect ya uccm kwenye taasisi hizi. otherwise safari itakuwa ngum sana
 
Ni jambo jema sana. lakin nani ana approve existence ya hiko chama? ni serikal hii hii ya ccm au nyingine?
 
Mafanikio ya Samia ni habari mbaya sana kwa Lisu maana 2025 hana chake tena.

Ccm itaendelea kupeta
Hahahaha! Naona taga limeanza kumkubali mama taratiiibu! Usijisahaulishe kuwa wewe umeongoza mapambano ya kumpinga mama. Tuna rekodi zako.
 
Tena mfanye haraka kukisajili, mjikusanye wote wenye roho mbaya bila kumsahau Chalamila aliyewahi kutamka mbele ya mwendazake kuwa anatamani vyama vya upinzani vyote vifutwe kiaki kimoja tu kitakaitwa "Magufuli Ruling Party"! Msiwasahau pia wale wanyang'anyi na waporaji wa aina ya Sabaya ili ije kuwa rahisi kuwakamata kwa pamoja mkasote lupango mpaka dunia iwasahau kabisa!
Yaani kuzungumzia misimamo ya Mwendazake maana yake unazungumzia:-
1.Ukandamizaji wa haki za wananchi.
2.Udini,ukabila,ukanda na yote yafananayo na hayo
3.Utekaji, utesaji , na mauaji ya wananchi
3.Uporaji wa fedha za wananchi kupitia vyombo vya dola.
4.Ununuzi wa viongozi na wanachama wa upinzani, ubaguzi wa kiitikadi na wizi wa kura uliotopea
5.Kuua ushirikiano wa kimataifa kwa kisingizio cha vita ya kiuchumi
6.Kukopa sana madeni huku ukidangaya wananchi kuwa unajenga miradi kwa fedha ndani
7.Kudhoofisha uchumi na kushindwa kabisa kutoa ajira na mishahara mipya kwa watumishi miaka 5 net!
8.Kubambikiza watu kesi ili tu kuwakomoa
9.Kufukuza watumishi kazi bila kuwalipa haki zao
10.Kubolea wananchi nyumba huku kukiwa na zuio la mahakama, a huwalipi fidia
Hivyo ni baadhi ya vipengele vinavyofaa kuingizwa katika katiba ya hicho chama na sjui itatawala wapi maana Watanzania kuanzaia sasa tunaendesha maombi tusijepata tena mkosi kama ule alotutua Mungu wetu mwenye huruma!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…