Sisi tunaamini kwenye misimamo ya Magufuli ndiyo hasa misingi ya Chama Cha Hapa Kazi Tu... HKT. Kwenye hii misingi tutajenga Tanzania imara sasa na kwaajili ya vizazi vijavyo.
Uhuru wa kiuchumi ni jambo linalowezekena kama tutasimamia vizuri maliasili tulizonazo kwa manufaa ya wote.
Hatutakaa kimya pale tunapohisi rushwa, wizi na upotevu wa rasilimali za nchi unapotokea.
Naamini kuna umuhimu mkubwa wa chama kipya na Katiba mpya.
Chama kipya kiwaunganishe Watanzania wote bila kujali, dini, kabila, jinsia, ukanda. Kiwe chama cha kitaifa.
CCM inahitaji changamoto wa cha imara, madhubuti kitachosimamia haki, kupinga rushwa, upigaji, vyeo kutolewa kwa undugu, udini, ukabila, vitolewe kufuata (merits), mtu ana vigezo.
Katiba Mpya ni muhimu, hapa inabidi kuwashirikishs wadau wote wa vyama vyote including CCM, viongozi wa dini zote, tassisi zote.
Katiba mpya itasaidia:-
1. Mikataba yote mikubwa iwekwe wazi all terms, conditions, small prints.
2. Kuondoa kinga za kutoshtakiwa. Kiongozi yoyote aweze kushtakiwa na ikithibitika alivunja sheria, afungwe. Aweze kushtakiwa hata baada ya muda wake wa uongozi (Retrospectively)
3. Mahakama ziwe huru kusimamia haki na sheria bila kujali cheo, pesa. Zibadilike kuweza kutenda haki kwa maskini, wajane, yatima. Kila mtuhumiwa apewe wakili kwa wale wasiojiweza.
Dhamana iwe haki ya msingi kwa watuhumiwa wengi except (kesi za mauaji, ubakaji, uhujumu uchumi, ugaidi, flight risk)
4. Bunge liwe huru, kuisimamia serikali na kujadili mikataba kwa uwazi, kuhoji kwa staha.
5. Tume huru ya uchaguzi ni muhimu. Ruzuku kwa vyama zipunguzwe wapewe vyama vipya tu. Kwa chama kikongwe kama CCM ziondolewe kabisa. Wabunge wapunguzwe. Posho, mikopo zipunguzwe.
Mawaziri, wabunge, Wakuu wa Mikoa, wilaya, kata, watendaji wawe watu wenye weledi, uzoefu, maadili, waadilifu, waaminifu.
Wachaguliwe kutokana na kazi walizozifanya huko nyuma. Sio lazima wawe wanachama kwenye chama kinachoongoza serikali.