Hapa Kazi Tu (HKT) kiwe chama kipya cha kisiasa Tanzania kitakachoenzi falsafa na maono ya Hayati Dkt. Magufuli na kiwe tegemeo la Watanzania

Hapa Kazi Tu (HKT) kiwe chama kipya cha kisiasa Tanzania kitakachoenzi falsafa na maono ya Hayati Dkt. Magufuli na kiwe tegemeo la Watanzania

Nigrastratatract ,

..msimamo wa chama chenu kuhusu tume ya uchaguzi na sheria ya vyama vya siasa ukoje?

..je, mnadhani tume ya uchaguzi iko sawasawa, au kuna mabadiliko mnadhani yanahitajika?
Chama chetu cha HKT kinaunga mkono wazo lolote lenye nia njema na nchi yetu kwa 100% pasipo kupindisha hoja Katiba mpya yenye mlengo wa kuwasaidia watanzania inatakiwa ila isiwe ajenda ya kikundi fulani tunataka utumike weledi wa hali ya juu mimi nimegundua kiburi cha CCM Kufanya watakavyo ni kwa sababu wanajua watashinda tu kwa hiyo basi ili watawala wajikite kwenye mambo mema ya kuistawisha nchi lazima wawe waoga wa kuwakosea watanzania na njia pekee ya kuiogopa sauti ya Watanzania ni kuwatengenezea watawala mifumo ya kuwawajibisha kwenye sanduku la kura na kwa mjibu wa sheria , kwa mfano CCM ingelikuwa inawaogopa Watanzania mikataba mingi wangekuwa wanaiweka wazi maana sisi Wananchi ndio waajiri wao kwa hiyo lazima kupatikane mwongozo mpya wa kuwasukuma na kuwaogopesha watawala kwamba tukikosea tutawajibishwa na hivyo basi watajituma kuleta huduma za kijamii na watasita mara moja kutekeleza nia haramu ya nchi
 
Magufuli alikua ana maono??

Yalikua yapi??

Kusema analipwa millioni 9 kwa mwezi na haimtoshi?

Kujenga airport kwa gharama kubwa kijijini?
 
Chama chetu cha HKT kinaunga mkono wazo lolote lenye nia njema na nchi yetu kwa 100% pasipo kupindisha hoja Katiba mpya yenye mlengo wa kuwasaidia watanzania inatakiwa ila isiwe ajenda ya kikundi fulani tunataka utumike weledi wa hali ya juu mimi nimegundua kiburi cha CCM Kufanya watakavyo ni kwa sababu wanajua watashinda tu kwa hiyo basi ili watawala wajikite kwenye mambo mema ya kuistawisha nchi lazima wawe waoga wa kuwakosea watanzania na njia pekee ya kuiogopa sauti ya Watanzania ni kuwatengenezea watawala mifumo ya kuwawajibisha kwenye sanduku la kura na kwa mjibu wa sheria , kwa mfano CCM ingelikuwa inawaogopa Watanzania mikataba mingi wangekuwa wanaiweka wazi maana sisi Wananchi ndio waajiri wao kwa hiyo lazima kupatikane mwongozo mpya wa kuwasukuma na kuwaogopesha watawala kwamba tukikosea tutawajibishwa na hivyo basi watajituma kuleta huduma za kijamii na watasita mara moja kutekeleza nia haramu ya nchi
Nitakuwa mjumbe kwenye chama hili sitaliacha linipite viva jpm
 
Ukiwa ndani ya CCM hauwezi kuikosoa na kuisahihisha kwa sababu never outshine your master lkn ni rahisi sana kupush ajenda nje ya CCM kuna mwafizikia Newton aliwahi kusema nguvu ya ndani haileti mwelekeo bali ni nguvu ya nje mm nimezaliwa kusimamia ukweli lkn sio kujipendekeza ili nipate madaraka kwangu mm furaha yangu ni kuona matokeo

Well said, wanasiasa wengi wa kitanzania wanapenda kujipendekeza ili kupata nafasi za uteuzi. Kama unamaanisha anza taratibu za kutafuta wanachama wa mwanzo wanao takiwa ili kupata usajili. Usisubiri karibu na uchaguzi. Tanzania hii wanaweza kufanya zengwe usajili usipatikane kama walivyofanyiwa kile chama cha Sitta.

Uungwaji mkono upo! Tumechoka na siasa za kujipendekeza na kutafuta umaarufu. Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kiuongozi na mfumo. Kwasasa uongozi unabadilika kwa watu kupeana na mfumo huko pale pale. Hakutakuwa na jipya katika Tanzania yetu.
Tunahitaji kusimama kama nchi inayojitambua. Si kujipendekeza ati tuonwe wazuri. Tunahitaji kukua kiuchumi, na kinguvu kuwa Taifa kubwa. Tufute omba omba kama nchi, tujitegemee, tusomeshe vijana wetu na kuwatumia ktk kuendeleza nchi.

Magufuli alileta mabadiliko chanya. Sasa tunarejea enzi za nyuma. Wanaosema Magufuli aliuwa wanaushahidi? Mauwaji yamekuwepo katika hii nchi toka uhuru.
Kuanzia kwa Nyerere, nakumbuka nikiwa mdogo kuna mwanasiasa mmoja, alipigwa Risasi hadharani katika mkoa fulani. Wakati wa Mwinyi kuna mauaji yalitokea yakiwalenga Maprofesa Kadhaa.
Wakati wa Mkapa, watu waliuliwa na hasa ktk maandamano ya Mwembe Chai, na kule Zanzibar.

Wakati wa Kikwete kulikuwa na utekaji, Ulimboka, na baadhi ya waandishi wa habari, Mauaji ya Albino, Mwandishi wa habari aliyeuwawa huko Iringa. Hata Mauaji ya Kibiti yalianza JK akiwa madarakani.
Haya mambo hutokea katika nchi yoyote ile. Hakuna binadamu asiye na mapungufu. Hizo lawama anazopewa Magufuli ni kwa wale waliomchukia. Na kwa kawaida uwezi pendwa na binadamu wote. Au kuwafurahisha wote.
Hongera kwa wazo hili na anzisha hicho chama nauhakika wafuasi wengi wapo. VIva Tanzania Viva!
 
..nyinyi mtakuwa kikundi cha unyama na ukatili cha magufuli.

..mama hana mpango na nyie ndio maana mmeamua kujilipua kuja na chama kipya.

..hamna hata haya kuomba kuungwa mkono na Watz mliokuwa mkiwatesa, na kuwadhulumu.
 
Kwa mfano mkuu utata wa Mradi wa Bagamoyo inabidi pia wewe mwenyewe ujiulize kwa nn CHINA kila akiingia mikataba hii na nchi nyingi huishia kuzinyonyoa chukulia mfano SRI LANKA, ZAMBIA, KENYA zimeelemewa na mzigo wa sera za kiuwekezaji za Mchina huu mradi tungeuweza hata sisi trillion 23 tungeweza kuujenga hata kwa miaka 10 na ukaisha Tuna Bandari kibao ni sawa sawa na ww kuwa na TV ya sebuleni unang'ang"ana kununua TV ya chumbani matokeo yake unaongeza liabilities

Jaribu kukuza uelewa wa mambo kwanza na kuacha siasa za propaganda ndio ufikilie kuanzisha chama...nimeandika hivi kulingana na ulichoandika andika juu hapo.... maana hujui utofauti wa miradi kuanzia huo wa Sri lanka, Zambia na Kenya..... jaribu kufuatilia vitu kiundani na sio kumeza madesa mabovu na kuendelea kuaminisha watu ujinga...

Dr Slaa aliwahi kuwadanganya watu Gas yetu inaibiwa na kuna bomba la gas linapeleka gas arabuni limepita chini ya bahari.....huyu huyu Dr Slaa ndio muanzilishi wa ile story ya Riz 1 kukamatwa na madawa China.... then akaja mwingine akatuambia gas yote tumemuuzia mchina ilihali mchina hana na hakuwahi kuwa hata na kitalu cha gas TZ zaidi ya kupewa tenda ya construction ya bomba la gas..
 
Siasa za uongo uongo na propaganda ni siasa za kijamaa za kizamani sana matokeo yake ni kutengeneza kizazi cha watu wajinga ambao kichwani wanakuwa wamejaza propaganda kuliko uhalisia wa mambo...

Leo hii ukifunuliwa hayo mamikataba ya kila ujenzi unaondelea unaweza kuzimia, sidhani kama unajua cost za haya mamiradi yanayoendelea vs uhalisia na hizo cost zilizodhidi hela zinakwenda wapi...unajua SGR phase one ya mturuki hela ilitoka wapi? na kwa riba kiasi gani? unajua kwanini mturuku kafunga kambi Ethiopia na kaweka mizizi hapa? unajua kwanini waturuki wanamiminika TZ kila kukicha? unajua mpaka sasa Yapi anatudai kiasi gani?, Unajua gharama halisi za stieggler na hela inatoka wapi? unajua kwanino El-SISI na Endorgan walikuja Tanzania? Unajua kwanini kile kipande cha reli pale Dom kapewa Mchina na hela imetoka wapi?
Unajua gharama halisi ya kununua haya madege na kuziendesha na kwanini CAG alikuwa hakagui ATCL wala mchakato wa kuzinunua?...unajua kwanini maujenzi yote hayo CAG alikuwa hafiki na Tanroad hakuigusa...?

Unamjua aliyekuwa na tenda ya kujenga Chato international Airport, unajua gharama halisi ya huo ujenzi vs iliyotangazwa, unajua aliipataje pataje hiyo kazi?...MWISHO KABISA UNAJUA KWANINI DENI LA TAIFA LIMEKUWA KUBWA KWA MUDA MFUPI? Ilihali kila structure inayojengwa ni fedha za ndani?
 
Ulishawahi kujiuliza kwanini mataifa yote yanayofuata siasa za kijamaa za kizamani yanaishia kwenye migogoro na watu wake kuwa masikini....Angalia ulaya mashariki kuanzia baba lao Urusi, Romania, Bulgaria nk vs ulaya magharibi halafu niambie akina nani masikini na ombaomba na watu wamigogoro kila siku..

Leo kila Mwafrika anayezamia meli au kwenda kubeba box anataka kwenda Ulaya magharibi kwa mabeberu na sio kwa marafiki zetu Warusi, wachina au bulgaria..

Nimeandika hapo juu baada ya kuona unawaza kizamani na kuwa na maono ya kizamani ambayo yule jamaa unayempenda alikuwa nayo pia...jaribu kuwaza kisasa kulingana na kasi ya dunia vs wakati tuliopo sio mawazo ya kijamaa ya kizamani yanayowaza vita baridi na migogoro kwa kuamini kila unachowaza wewe ndio sahihi na wengine wote wakusikilize wewe...
 
Nakuonea huruma maana hata mke wa hayati hateseki Kama wewe
Mke wa hayati katoka shavu moja matata, na ngozi inameremeta! May be kwa sasa ni mmoja wa wanawake wenye furaha zaidi duniani, that mf alimtesa sana! Na hana mpango na huko Chato kwa sasa, yupo zake Masaki.
 
Sisi tunaamini kwenye misimamo ya JPM ndiyo hasa misingi ya Chama Cha Hapa Kazi Tu... HKT. Kwenye hii misingi tutajenga Tanzania imara sasa na kwaajili ya vizazi vijavyo.
Uhuru wa kiuchumi ni jambo linalowezekena kama tutasimamia vizuri maliasili tulizonazo kwa manufaa ya wote.
Hatutakaa kimya pale tunapohisi rushwa, wizi na upotevu wa rasilimali za nchi unapotokea.

Kwa mara ya kwanza maishani mwangu nitakata kadi ya chama. Kiko wapi?
 
Kwa mfano mkuu utata wa Mradi wa Bagamoyo inabidi pia wewe mwenyewe ujiulize kwa nn CHINA kila akiingia mikataba hii na nchi nyingi huishia kuzinyonyoa chukulia mfano SRI LANKA, ZAMBIA, KENYA zimeelemewa na mzigo wa sera za kiuwekezaji za Mchina huu mradi tungeuweza hata sisi trillion 23 tungeweza kuujenga hata kwa miaka 10 na ukaisha Tuna Bandari kibao ni sawa sawa na ww kuwa na TV ya sebuleni unang'ang"ana kununua TV ya chumbani matokeo yake unaongeza liabilities
Kumbe iko Siku tutaweza kuwalipa T 23 zao siyo?

Kwani ukikopa pesa Bank kwa miaka miwili lakini baada ya miezi 6 ukarudisha zote kuna ubaya?

Suala hapa ni kucheza na Clauses....

Siyo ati kusema huu mradi ni mbovu...

Negotiating with skills!!
 
Vip mtaendeleza pia kuteka na kupoteza watu.
 
Tumeanza taratibu maana tunaona CCM tunayoitaka haijirekebishi inarudia tabia za zamani za mikataba ya hovyo hovyo Rais wa nchi anakuwa mtu wa kujipendekeza kwa watu ambao hawakumchagua vyama vingine vya Upinzani vimekuwa matawi ya CCM, na waporaji wa rasilimali zetu tunataka ulinzi imara na kwa wivu wote wa rasilimali za nchi yetu tunawataka viongozi wa nchi wazidishe vita dhidi ya Rushwa kwa vitendo
 
Ulishawahi kujiuliza kwanini mataifa yote yanayofuata siasa za kijamaa za kizamani yanaishia kwenye migogoro na watu wake kuwa masikini....Angalia ulaya mashariki kuanzia baba lao Urusi, Romania, Bulgaria nk vs ulaya magharibi halafu niambie akina nani masikini na ombaomba na watu wamigogoro kila siku..

Leo kila Mwafrika anayezamia meli au kwenda kubeba box anataka kwenda Ulaya magharibi kwa mabeberu na sio kwa marafiki zetu Warusi, wachina au bulgaria..

Nimeandika hapo juu baada ya kuona unawaza kizamani na kuwa na maono ya kizamani ambayo yule jamaa unayempenda alikuwa nayo pia...jaribu kuwaza kisasa kulingana na kasi ya dunia vs wakati tuliopo sio mawazo ya kijamaa ya kizamani yanayowaza vita baridi na migogoro kwa kuamini kila unachowaza wewe ndio sahihi na wengine wote wakusikilize wewe...

Katika maelezo ya awali, naona lengo lao ni kulinda raslimali na kuzitumia katika kuleta na kujenga maendeleo ya uchumi katika nchi, na kujenga mahusiano ya kimataifa yenye mfumo huru na faidishi. Kupiga vita wizi,uonezi na dhurma dhidi ya utu wa Watanzania wote bia kujali itikadi, rangi, kabila dini, elimu na kujenga uwiano sawa katika matumizi ya raslimali za ndani kwa maslahi ya taifa la leo na kesho. Hatuwezi kukomboa nchi yetu dhidi ya dhurma na uonezi ikiwa tutakuwa na vyombo vya uongozi vionga, vinavyoogopa wezi na wabadhirifu.
Tunahitaji viongozi wenye ufahamu, nia na maarifa sahihi ya kulinda, kusimamia na kumuendeleza mtanzania bila unafiki wala uwoga.
 
Tumeanza taratibu maana tunaona CCM tunayoitaka haijirekebishi inarudia tabia za zamani za mikataba ya hovyo hovyo Rais wa nchi anakuwa mtu wa kujipendekeza kwa watu ambao hawakumchagua vyama vingine vya Upinzani vimekuwa matawi ya CCM, na waporaji wa rasilimali zetu tunataka ulinzi imara na kwa wivu wote wa rasilimali za nchi yetu tunawataka viongozi wa nchi wazidishe vita dhidi ya Rushwa kwa vitendo
Kisajilini haraka tuanze kupambania katiba mpya.

Au kwenu katiba iko poa tu.
 
Sisi tunaamini kwenye misimamo ya Magufuli ndiyo hasa misingi ya Chama Cha Hapa Kazi Tu... HKT. Kwenye hii misingi tutajenga Tanzania imara sasa na kwaajili ya vizazi vijavyo.

Uhuru wa kiuchumi ni jambo linalowezekena kama tutasimamia vizuri maliasili tulizonazo kwa manufaa ya wote.

Hatutakaa kimya pale tunapohisi rushwa, wizi na upotevu wa rasilimali za nchi unapotokea.
sawa wasukuma sajilini chama chenu
 
Back
Top Bottom