Kwa nini nembo ya taifa haikuandikwa "Kazi na barabara ?" Aliuliza Mheshimiwa Lissu !!
Uchaguzi huu utakuja na ajenda za ajabu sana. Ajenda hiyo ya lissu inaweza kuwafanya wafuasi wake kuanza kuvunja barabara zilizojengwa hasa wale wasiokuwa na magari kwa vile inawajenga kuamini kuwa barabara siyo za muhimu. Vile vile inajenga sana kasumba kuwa serikali inatakiwa kuwa inawawekea pesa wananchi pesa mifukoni wakati contract baina ya serikali na wanachi ni kodi+infrastructure, yaani raia analipa kodi, halafu serikali inajenga miundo mbinu na kujenga ulinzi wa nchi na raia wake; jambo mabalo haliwezi kufanywa na mtu binafsi.
Sasa ukianza kubeza kuwa barabara na madaraja siyo ya muhimu, halafu akaja mtu akaanza kuyalipua kwa mabomu ya kigaidi, itakuwa ni hatua nyingi sana za kurudi nyuma. Wakati tunapata uhuru hatukuwa na barabara yoyote yenye lami, ndipo Nyerere akaaza kujenga pole pole; hadi anaodoka alikuwa ameacha Dar-Tunduma, Morogoro-Dodoma, Chalinze-Tanga-Arusha, na Mwanza-Sirari. Leo hii zipo nyingi sana karibu nchi nzima na ni muhimu tujivune kuwa nazo siyo kuzibeza kuwa siyo za muhimu kwa maisha yetu. Cheap politics huweza kuleta unintended consequences kwa jamii.
Halafu nembo inasema "Uhuru na Kazi", haisemi "Kazi na Uhuru."