Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Kama mtu umefanya biashara nchi hii utagundua kwamba aliyetunga sheria zingine za kodi hajawahi hata kuuza karanga.
Sheria za kodi na kanuni zake zimelalamikiwa kwa miaka nenda rudi, huku TRA wakisema hawahusiki na sheria hizo na wanawakandika wafanyabisahra kama zilivyoandikwa, liwalo naliwe.
Kwa sheria hizi kuna wafanyakazi wa TRA wametajirika sana, maana wanazitumia kwa rushwa. (Kama aliyekutwa na Tshs bilioni 7 nyumbani kwake)
Kanuni moja inayo lalamikiwa sana ni ile ya ulipaji wa kodi ukitoa tu Invoice.
Yaani ukiandika madai yako kwa mteja, uwe umelipwa au haujalipwa unatakiwa ulipe ndani ya mwezi mmoja VAT 18% ya ile ankara(Invoice). Na ankara hiyo shurti iambatane na risiti ya EFD, kuwa umelipa hiyo kodi.
Hili imelalamikiwa sana na wafanyabiashara kwani serikali ndio walalamikiwa wakuu kwa kutolipa madeni yao kwa wafanyabiashara.
TRA huwa halielewi hilo, na usipolipa kwa wakati, deni hilo linazaa fine na interest ya malibiizo.
Huu ni wizi wa mchana.
Suala hili limelalamikiwa kwa miaka nenda rudi, toka kanuni hizi zianze kutumika.
Kimsingi ni kama Serikali inapora wafanyabiashara kwa kalamu.
Rais Samia apewe maua yake kwa kuliona hili na kulifanyia kazi kwa kuziangalia upya sheria na kanuni hizi za kodi zisizo halali za Serikali kwa kuitumia TRA.
UPDATE
=====
Mama Samia tayari jana 31/7/2024, ameteua Tume itakayotoa mapendekezo ya sheria zinazo athiri biashara kama zinavyotekelezwa na TRA.
Big step forwad.