Hivi samaki ni Halal kuliwa kwake au si halal? Maana huwa naona wanajifia wenyewe tu.
Hawachinjwi. Na vitabu vinataka tule mnyama aliye chinjwa sasa hapo wadau inakuaje?
Maana mimi huwa nasita sana. Naona tunakula kibudu.
Mkuu kwa sisi Waislam hakuna shida kula samaki hata kama wamejifia wenyewe.
Kwa maana wanyama wengine tunawchinja kuondoa ile damu inayotiririka miilini ambapo ukiwachinya damu ile kwa msaada wa mapigo ya moyo inatoka na sumu nyingi mwilini na kuiacha nyama kuwa laini na inayoweza kukaa muda mrefu kabla ya kuandaliwa kwaajili ya kula.
Ila samaki hana damu ya namna hiyo, hivyo hatuna sababu ya kumchinja kuiondoa damu inayotiririka.
Kula samaki mkuu,
Samaki wana Omega 3, wana Vitamin D na B2, pia wana madini ya Calcium, Chuma, Potassium, Magnessium na Zinc.
Ulaji wa samaki hupunguza hatari ya kupata shambulio la moyo, unaboresha uwezo wa macho kuona, unapunguza hatari ya kupata saratani, unasaidia kutibu maradhi ya ini, na pia unaongeza afya ya ubongo.
Mkuu kula samaki walau mara mbili kwa wiki.