Hapa ndio ninapokuwa na walakini na uwepo wa Mungu

Habari za usahihi umeleta wewe.

Kwa hivyo wewe ndio una jukumu la kuelezea huo usahihi.
Huwezi kukosoa pasipokuwa na kosa, wewe unasema upo humu ili kukosoa ndio maana nikakuuliza je wewe upo sahihi?

Usahihi ni hali ya kutokuwa na makosa,ukweli.

Je unachosimamia wewe hakina makosa, ni ukweli?
 
Umesema huna dhambi, u mtakatifu lakini umepitia mambo mazito. Je unaifahamu habari ya Ayubu kwenye Biblia
 
Huwezi kukosoa pasipokuwa na kosa, wewe unasema upo humu ili kukosoa ndio maana nikakuuliza je wewe upo sahihi?

Usahihi ni hali ya kutokuwa na makosa,ukweli.

Je unachosimamia wewe hakina makosa, ni ukweli?
Kosa ni nini?
 
Nimegusa hilo moja kwa sababu ndio nimeona kitu kipya kwangu tofauti na hayo mengine ambayo tushaona yakielezwa sana humu, ila kama unaona nalazimika kukujibu yote kwa wakati mmoja kinyume na hivyo nakuwa nakupotezea muda basi acha nisipoteze muda wako mkuu.
Sawa. Siku njema.
 
Kwa hivyo nikisema hakuna Mungu ni kosa?

Ila wewe ukisema kuna Mungu sio kosa sio?
Imani ya uwepo wa Mungu kila siku inakosolewa na ndio maana hata wewe ukasema upo hapa kukosoa, hiyo sio shida ila mimi nikaamua tu kukuuliza je wewe(atheist) unadhani upo sahihi?
 
Sisi binadamu wote,wazungu kwa waafrica tumepewa maarifa lakini hatujayatumia hata mia tu. Hata wewe hapo unapitia mambo mazito ksbb hujatumia maarifa tuliyopewa na MUNGU.

Maarifa tuliyopewa na MUNGU ni wachache wameyafikia. Na ukiyafikia utaishi kwa Raha na amani sana duniani. Utaheshimu kiumbe chochote hapa duniani. Utaongea na kiumbe chochote hapa duniani. Utakuwa na nguvu ya kukwepa matatizo yoyote ya mbele yako. Utakuwa na uwezo wa kiuchumi vyovyote upendavyo.

Ingia kwenye kuitafuta nguvu na maarifa tuliyopewa na MUNGU.
Anza kufanya meditation. Anza kidogo kidogo kwa kujizoeza kama kufanya mazoezi vile. Huko kuna nguvu kubwa ya KIMUNGU imefichwa huko.
Fanya hatua kwa hatua. Hata matatizo yako utayatatua huko yote.
 
Imani ya uwepo wa Mungu kila siku inakosolewa na ndio maana hata wewe ukasema upo hapa kukosoa, hiyo sio shida ila mimi nikaamua tu kukuuliza je wewe(atheist) unadhani upo sahihi?
Ndio nipo sahihi.

Kwa sababu hakuna uthibitisho wa uwepo wa huyo Mungu.

Kwa hivyo imani ya kusema kuna Mungu ni uongo.
 
Vp uthibitisho ukija kupatikana je uongo utabadilika kuwa ukweli? Au hufikirii kuwa inaweza kuja kupatika uthibitisho?
 
Kwa hiyo mlianza na uongo kwamba Mungu yupo bila uthibitisho?

Halafu bado unakataa kwamba Mungu hayupo?

Kumbe unajua kwamba kusema Mungu yupo bila uthibitisho ni uongo.

Sasa usibishe tena kwamba Mungu hayupo, Kama huna uthibitisho wa uwepo wake.
 
Mimi nachofahamu kukosekana uthibitisho tuhakufanyi jambo kuwa uongo bali inakuwa limekosa uthibitisho ndio maana kuna mambo mengi mifano mingi tu ya mambo ambayo hayakuwa na uthibitisho ila baada muda yakaja kuthibitishika. Ila kwakuwa wewe unasema jambo likiwa halina uthibitisho linakuwa moja kwa moja ni jambo la uongo ndio maana nikauliza je endapo siku ikaja kutokea kupatikana huo uthibitisho je uongo utageuka na kuwa ukweli?

Kwa sababu atheists wanasisitiza kuwa hawaamini Mungu kwa sababu ya kutokuwepo uthibitisho ila wewe unasema kutokuwepo kwa uthibitisho hufanya hilo jambo kuwa ni uongo.
 
Wewe uliwezaje kujua Mungu yupo bila uthibitisho?

Ulifikaje conclusion kwamba kuna Mungu, Bila ya kuwa na uthibitisho wowote wa kuwepo huyo Mungu?
 
Swali langu mbona haulijibu mkuu?

Mimi najua Mungu yupo kupitia imani, na zipo sababu na dalili zenye kufanya niamini hivyo.
 
Back
Top Bottom