Hapa ndipo Area D, Dodoma. Na hili ndilo geti lililoachwa wazi na walinzi kutokomea siku Lissu aliposhambuliwa

Hapa ndipo Area D, Dodoma. Na hili ndilo geti lililoachwa wazi na walinzi kutokomea siku Lissu aliposhambuliwa

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Hapo chini kuna video inayoonyesha makazi ya Area D.

Hususan ni hilo geti na nyumba ya walinzi ambao tunaambiwa siku ya tukio hawakuonekana.

Hakuna video yoyote nyingine inayoonyesha eneo hilo kama hii hapa chini.

 
..waandishi wa habari makini wangetutoa hapo getini mpaka eneo aliposhambuliwa Lissu.

..mdogo-mdogo tutapata picha nzima pamoja na sehemu zilipokuwa CCTV.
Lissu ni mtu mwenye bahati sana.

Baada ya kunusurika mara ya kwanza alipomiminiwa risasi; muujiza mwingine ni kunusurika kwake baada ya uchaguzi wa 2020.

Ni jambo la kushangaza kidogo ukilifikiria kwa makini.
 
10 February 2023

Tume ya Haki Jinai waanza kuhoji Wakuu wa Polisi na wakuu wa .... ikiwa pamoja na kuangalia utendaji wa taasisi zilizopo ktk mfumo wa haki jinai.... ..


Mwenyekiti jaji Chande anasema kuna upungufu au mmomonyoko wa imani za wananchi kuhusu taasisi zilizopo ktk mfumo wa haki jinai pia jaji Chande awaomba raia kutoa maoni yao kuhusu utendaji wa taasisi hizo .. kwa kutuma maoni yao ktk anuani za mawasiliano za tume hiyo zilizopo twitter, FB, email, WhatsApp na simu.

Pia Toka maktaba :
Taarifa iliyotolewa jana Januari 6, 2023 na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus imewataja wajumbe hao;
Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha taasisi za Haki Jinai nchini inayoongozwa na Mwenyekiti Jaji Mohamed Othman Chande na Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue. Wajumbe wengine ni pamoja na:

  • Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dk Eliezer Feleshi,
  • Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais (Utumishi) Dk Laurean Ndumbaro,
  • Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP mstaafu Said Mwema
  • na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP mstaafu Balozi Ernest Mangu.
  • Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Dk Edward Hosea,
  • Askari Polisi mstaafu, Saada Makungu,
  • Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco Omar Issa,
  • Ofisa mwandamizi Ofisi ya Rais Baraka Leonard
  • na Mkurugenzi wa Utafiti katika Chuo Kikuu cha Zanzibar na Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Zanzibar, Yahya Khamisi Hamad.
 
..hapo chini kuna video inayoonyesha makazi ya Area D.

..hususan ni hilo geti na nyumba ya walinzi ambao tunaambiwa siku ya tukio hawakuonekana.

..hakuna video yoyote nyingine inayoonyesha eneo hilo kama hii hapa chini.



Thamani ya hiyo video ni kuonyesha mazingira ya tukio lililipotokea. Zaidi ya hapo hakuna kitu kabisa.

Ukitaka kufuatilia kwa makini; na ninatumaini Tundu Lissu au jamaa zake walishafanya kazi hiyo, kutafuta taarifa toka kwa mashuhuda mbalimbali wa tukio, usiwaweke kwenye video kama hawa tunaowaona wakihojiwa.

Hasa huo Mwenyekiti, majibu yake yanatia wasiwasi mkubwa sana.
 
..tungekuwa na waandishi wa habari wachunguzi ingesaidia sana kupata ukweli wa tukio la Lissu.

..kwa mfano, muandishi mchunguzi angeweza kutegua kitendawili cha walinzi wa area D.

..kwanza, angeweza kujua kama walikuwepo. Na angeuliza walichukua hatua gani. Au angeweza kujua kama waliondolewa, na mamlaka gani inahusika na kuweka ulinzi eneo hilo.

..pili, muandishi mchunguzi angeweza kujua undani kuhusu CCTV ambazo Polisi walidai wanazo. Angedadisi zimechukuliwa na nani.

..tatu, muandishi mchunguzi angewahoji majirani kuhusu wanavyoishi na hali ya usalama ktk eneo lao. Jinsi watu wanavyoingia na kutoka katika makazi ya viongozi area D.
 
I can feel the anxiety and depression of Lissu's assailants knowing that its going to be bad for sure.....

kufanya kaz za shetani na wewe uaonekana shetani.... time to pay the price in full.
Say it again.
Wako hoi popote walipo
 
..tungekuwa na waandishi wa habari wachunguzi ingesaidia sana kupata ukweli wa tukio la Lissu.

..kwa mfano, muandishi mchunguzi angeweza kutegua kitendawili cha walinzi wa area D.

..kwanza, angeweza kujua kama walikuwepo. Na angeuliza walichukua hatua gani. Au angeweza kujua kama waliondolewa, na mamlaka gani inahusika na kuweka ulinzi eneo hilo.

..pili, muandishi mchunguzi angeweza kujua undani kuhusu CCTV ambazo Polisi walidai wanazo. Angedadisi zimechukuliwa na nani.

..tatu, muandishi mchunguzi angewahoji majirani kuhusu wanavyoishi na hali ya usalama ktk eneo lao. Jinsi watu wanavyoingia na kutoka katika makazi ya viongozi area D.
Mkuu 'JokaKuu', unamaana ya wakati gani? Sasa hivi, au enzi zile za akina Gwanda kupotea kwa habari ambazo hata haijulikana walichoandika juu yake hadi kusababisha kutoweka bila kujua walipo?

Ninayo matumaini, kwa sasa hivi inawezekana, na bila shaka mengi yatajitokeza. Tukio la aina hii haliwezi kufunikwa liwe siri milele.

Ninachomsihi Tundu Lissu akifanye pia, ni kuandika kitabu juu ya mkasa wote uliompata. Nina matumaini kuwa anazo taarifa za kutosha kabisa kuandika kitabu, ambacho hata pengine huko mbeleni kinaweza kuzalisha filmu yake.
 
Back
Top Bottom