Hapa ndipo Area D, Dodoma. Na hili ndilo geti lililoachwa wazi na walinzi kutokomea siku Lissu aliposhambuliwa

Hapa ndipo Area D, Dodoma. Na hili ndilo geti lililoachwa wazi na walinzi kutokomea siku Lissu aliposhambuliwa

..hapo chini kuna video inayoonyesha makazi ya Area D.

..hususan ni hilo geti na nyumba ya walinzi ambao tunaambiwa siku ya tukio hawakuonekana.

..hakuna video yoyote nyingine inayoonyesha eneo hilo kama hii hapa chini.



Mlinzi anasemaje?
 
Mkuu 'JokaKuu', unamaana ya wakati gani? Sasa hivi, au enzi zile za akina Gwanda kupotea kwa habari ambazo hata haijulikana walichoandika juu yake hadi kusababisha kutoweka bila kujua walipo?

Ninayo matumaini, kwa sasa hivi inawezekana, na bila shaka mengi yatajitokeza. Tukio la aina hii haliwezi kufunikwa liwe siri milele.

Ninachomsihi Tundu Lissu akifanye pia, ni kuandika kitabu juu ya mkasa wote uliompata. Nina matumaini kuwa anazo taarifa za kutosha kabisa kuandika kitabu, ambacho hata pengine huko mbeleni kinaweza kuzalisha filmu yake.

Na gari lake likakae makumbusho.
 
hahahaha kama ulivyo mshahara wa mtekaji, mtesaji, na mbambika kasi za uongo
tunapigana vita ya uchumi ndugu zangu
Tanzania hakuna corona ikamfyeka yeye
Walikataa katu katu kabisa kuwa Ngosha hakuwahi kuhusika kwa namna yoyote na hili tukio pamoja na serikali yake!

Wamebanwa vya kutosha na spana za jamaa wamekuja na hii statement kuwa msaliti afaa kuuwawa! Na wanajustify kwamba Lisu alikua msaliti!

Wapenda haki wote wataunga mkono hoja kwamba Lisu alikua msaliti. Laikini aliusaliti mfumo ambao ulianzishwa na Mwendazake, aliusaliti mfumo mbaya ambao Ni kinyume Cha taratibu, Mila na desturi zetu Watanzania!
Aliusaliti na aliukataa akakataa kuwa sehemu yake!
Wapenda haki wote hawatasema alistahili kuuwawa!
Jamaa wamepoteana hawajui wanatetea Wala kukubali Nini! Wanavizia aseme Jambo nao wadakie kujastify uharamia
 
..Nashauri Mdude Nyagali akafunguke mbele ya Tume ya Jaji Mkuu Chande.
Tungekuwa na mfumo wa haki mzuri, hata Said Mwema angewajibishwa kwa kuamuru mauaji ya waandamanaji halali Arusha mwaka ule.

Bahati mbaya sana wanaokumbuka ni wachache, na hao wachache wanaokumbuka wanaona kama haiwahusu.
 
Hapo chini kuna video inayoonyesha makazi ya Area D.

Hususan ni hilo geti na nyumba ya walinzi ambao tunaambiwa siku ya tukio hawakuonekana.

Hakuna video yoyote nyingine inayoonyesha eneo hilo kama hii hapa chini.


Hebu toeni hizi habari za miaka imepita. Mambo ya lissu ni jitihada kulitoa taifa kwenye mambo ya msingi kuhusu maendeleo ya wananchi. Mwenyewe tangu amerudi anathibitisha madai haya. Amekua anataka tujadili yeye kupigwa risasi tu na kashavua nguo hadharani kuonesha makovu.
Tusianguke kwenye huu mtego.
 
Tume ya Haki Jinai waanza kuhoji Wakuu wa Polisi na wakuu wa .... ikiwa pamoja na kuangalia utendaji wa taasisi zilizopo ktk mfumo wa haki jinai.... ..

Wanahojiwa hawana majina?

Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha taasisi za Haki Jinai nchini inayoongozwa na Mwenyekiti Jaji Mohamed Othman Chande na Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue.

Wajumbe wengine ni pamoja na:

  • Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP mstaafu Said Mwema

  • na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP mstaafu Balozi Ernest Mangu.

Askari Polisi mstaafu, Saada Makungu,
Hawa juu ndio wanaohojiwa? au Ndio wajumbe?
 
..tungekuwa na waandishi wa habari wachunguzi ingesaidia sana kupata ukweli wa tukio la Lissu.

..kwa mfano, muandishi mchunguzi angeweza kutegua kitendawili cha walinzi wa area D.

..kwanza, angeweza kujua kama walikuwepo. Na angeuliza walichukua hatua gani. Au angeweza kujua kama waliondolewa, na mamlaka gani inahusika na kuweka ulinzi eneo hilo.

..pili, muandishi mchunguzi angeweza kujua undani kuhusu CCTV ambazo Polisi walidai wanazo. Angedadisi zimechukuliwa na nani.

..tatu, muandishi mchunguzi angewahoji majirani kuhusu wanavyoishi na hali ya usalama ktk eneo lao. Jinsi watu wanavyoingia na kutoka katika makazi ya viongozi area D.
 
10 February 2023

Tume ya Haki Jinai waanza kuhoji Wakuu wa Polisi na wakuu wa .... ikiwa pamoja na kuangalia utendaji wa taasisi zilizopo ktk mfumo wa haki jinai.... ..


Mwenyekiti jaji Chande anasema kuna upungufu au mmomonyoko wa imani za wananchi kuhusu taasisi zilizopo ktk mfumo wa haki jinai pia jaji Chande awaomba raia kutoa maoni yao kuhusu utendaji wa taasisi hizo .. kwa kutuma maoni yao ktk anuani za mawasiliano za tume hiyo zilizopo twitter, FB, email, WhatsApp na simu.

Pia Toka maktaba :

Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha taasisi za Haki Jinai nchini inayoongozwa na Mwenyekiti Jaji Mohamed Othman Chande na Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue. Wajumbe wengine ni pamoja na:

  • Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dk Eliezer Feleshi,
  • Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais (Utumishi) Dk Laurean Ndumbaro,
  • Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP mstaafu Said Mwema
  • na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP mstaafu Balozi Ernest Mangu.
  • Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Dk Edward Hosea,
  • Askari Polisi mstaafu, Saada Makungu,
  • Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco Omar Issa,
  • Ofisa mwandamizi Ofisi ya Rais Baraka Leonard
  • na Mkurugenzi wa Utafiti katika Chuo Kikuu cha Zanzibar na Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Zanzibar, Yahya Khamisi Hamad.
Jenda imezingatiwa kweli, mbona wanaume tupu?
 
Hapo chini kuna video inayoonyesha makazi ya Area D.

Hususan ni hilo geti na nyumba ya walinzi ambao tunaambiwa siku ya tukio hawakuonekana.

Hakuna video yoyote nyingine inayoonyesha eneo hilo kama hii hapa chini.


Hapohapo getini kuna baa Sengia na kituo cha daladala.
 
Back
Top Bottom