Ingawaje mwinuko inaonesha ni kwa Macheni (kama tuta-sticky Ubungo to K/koo) lakini sitaki kuamini kwamba ndo penyewe unless kama ni far back enzi za ukoloni. Miongoni mwa sehemu ambazo zilijengwa mapema sana ni Magomeni. Ninachokiona hapo kabla hilo lilikuwa "daladala" la Ubungo to Kariakoo lakini lilipochoka kupita kiasi, likawa linapiga route za shamba, labda from Ubungo to Kibaha or anywhere along Morogoro Rd kuelekea Kibaha. Sema dereva ili awatafune kiulaini watoto wa shamba, akaamua kuacha kibao kuwaeleza "yeye ni mtu wa Dar"! Asikuambie mtu, unaambiwa hadi miaka ya 80 tu hapo, mtu angeweza kutafuna mtaa mzima kwa kofia ya "anatoka Dar"!