Hapa ni eneo gani kati ya Ubungo na Kariakoo - DSM

Hapa ni eneo gani kati ya Ubungo na Kariakoo - DSM

Sio zamani kivile,mwaka 1991 nikiwa pale kivukoni ilikuepo stand ya mabasi mikangafu kama hilo,,daladala za kawaida ilikuwa ni chai maharage,,
Hii sio 1991 ni nyuma zaidi. 91 juzi tu jiji lilikuwa limeshachangamka watu tunaruka kopo kwa Macheni tukitoka hapo tunaenda Lang'ata Kinondoni tena tunatumia gari za kisasa kabisa
 
Lakini wangechomoa kibao, ikumbukwe enzi hizo sheria zilikuwa kali, mfano ni pale magari madogo yote yalikuwa hayaruhusiwi kutembea Jumapili baada ya saa 7 au 8 kama sijakosea, kwahiyo hata kibao kisingeachwa hapo iwapo bus lilikuwa linakwenda shamba
Sheria zilikuwepo ila mambo ya route hayakuwa magumu sana.basi zilikuwa zina uhuru wa kwenda kwenye abiria wengi
Mambo ya kufupisha route yalikuja kukomeshwa na mwaibula kama uliwahi kumsikia
 
Hii miLeyland ya zamani, kuna utingo ashawahi kuachwa porini juu ya mti...

Basi lilikuwa limeshona, sasa utingo akaona isiwe tabu akabana zake juu kwenye 'keria'...

Basi likakata mbuga fulani yenye miti miti kiasi kwamba kuokoa uhai wake ikamlazimu utingo ajisalimishe kwenye tawi la mti...
 
Editing naona ,Super Slide linaenda perpendicular na barabara(lami),angalia gari dogo muelekeo wake kama linavuka barabara kuwafata mwanamke na mwanamme mbele kule ambapo hakuna barabara.
Jaribu kuangalia vizuri
 
milima ya pembezoni mwa morogoro road pale Kibanda cha mkaa bado ipo??

sa imagine miaka hio pale kama unapanda kutokea Jagwani kenda Magomeni Mapipa Hamna miinuko??

Enzi hizo Sinza ilikuwa mashamba ya mpunga
Inawezekana maana kama hakuna nyumba kuna miiti barabara haijachongwa vizuri
 
[emoji849]
FB_IMG_16147956688473478.jpg
 
Kuna mtu anatongoza hapo. Haya mambo hayakuanza leo.
 
Kama ionekanavyo pichani, hili ni eneo gani along Morogoro road DSM

View attachment 1716199
Barabara ya kuingia mjini ilikuwa inapitia Kigogo, hapo ni mlima kupanda kwenda Magomeni, huo mwinuko kushoto ni pale Rutihinda Primary ilipo. Daraja lililotumika ni lile pale Rutihinda, ndio mana pale Magomeni kuna lango la jiji hapo ndio ilikuwa sehemu ya kuingilia mjini. Kumbuka wimbo usemao "Heri kufa kwa kugongwa na gari la gorofa la kwenda Ilala, ooh heri kufa kwa kugongwa na gari la tela liendalo Zambia, kifo cha penzi ni kifo kibaya..." route illikuwa Kariakoo pale KAMATA kupitia Boma. Neno KAMATA linatokana na kuwa Depot ya mabasi ya mjini DMT (Dares salaam Motor Transport) baadae KAMATA (Kampuni ya Mabasi Tanzania)
 
Route nyingine mabasi yakitoka mjini yanaishia kinondoni mjini hapo ndiyo mwisho

Ova
 
Back
Top Bottom