Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Inawezekana mleta mada umri wake ni mdogo, ni kijana. Sidhani kama anajua huyo Mobutu alikaa ikulu kwa miaka mingapi.Andika vitu kwa facts sio unaongea kama upo kijiweni. Huyu mtoa mada ameweka mpaka vielelezo vya picha. Na wewe tupe facts zako
Magufuli anachota hela bila kufuata sheria na utaratibu.Heshima kwako mkuu.
Umechambua vizuri sana. Na hivi ndivyo twapaswa kuelezea mambo kuonesha pros and cons za miradi, na sio kishabiki kam wengi tunavyokua tunafanya. Kwamba kisa mm nimezaliwa Mbeya nikijenga Mbeya nimepapendelea.
Nyerere katika kipindi chake na mazingira ya nchi yetu ilikua tofauti sana.
1. Miundombinu ilikua mibovu na duni sana i.e barabara za mikoa na miko, wilaya na wilaya n.k, umeme, maji, hospital.
2. Elimu kwa watz; majority walikua hawana elimu. Ndo maana Nyerere alijikita sana kueneza elimu kufuta ujinga.
3. Uwezekaji ulikua mdogo sana na wengi walikua kwenye "Subsistence economy"
Kwa hiyo ni vigumu sana kufananisha mazingira ya nyerere na hali ya sasa.
Miji kama Mwanza, Geita na nchi ya Rwanda ni fursa kubwa kwa maeneo mingine ya jiran kibiashara. Hiyo miji ina watu wengi na ili kuendeleza biashara ndani ya hii miji inahitajika iwepo miji mingine maeneo jirani ya kibiashara ili uchumi wa ukanda husika uweze kua na "Multiplier effect....la sivyo biashara itajikuta ni Mwanza na Dsm,Mbeya, n.k
Ingawa mhe.alitakiwa pia aiangalie miji kama Musoma, Ngara, Biharamulo, Sirari, Shinyanga, Nyamongo, n.k ili kuhamasisha biashara na mji wake wa chato.
Mfano mji wa nyamongo, Geita, n.k una madini mengi sana angeboresha miundombinu na viwanja vya ndege ili kuleta ushindani ktk huo ukanda.
Kuna mdau humu ndani aliwahi kuleta mada kuhusu maendeleo kikanda akishauri ukanda flani ujitegemee wenyewe kimaendeleo kulingana na maliasili za ukanda husika. Yaani ukusanyaji kodi, allocation of resources etc visimamiwe na mamlaka (halimashauri) za ukanda huo.
Mfano Mwnza, Mara, Kagera, Geita (Ukanda wa ziwa) viwe na mamlaka ya ukusanyaji wa kodimgawanyo wake. Vivyo Hivyo kwa kanda zingne, pia kuwe na fungu la kwenda serikali kuu. serikali kuu ikiwa ni mshauri na pengme kuingila pale panapostahili.
Lkn hili kwa sasa naona linafanyika indirectly kwan kama maeneo duni katka ukanda flan yanajengwa na kuimarisha ni hatua nzuri ya kuelekea point ya maendeleoya ushindani kikanda.
Wito tu sheria na taratibu zifuatwe ktk allocation of Scarce resources we have, na haki itendeke.
Magufuli anachota hela bila kufuata sheria na utaratibu.
Hata kama angepeleka hela kwenye most deserving location (which he doesn't) angekuwa bado aakosea kwa kupeleka hela nje ya utaratibu.
Kwa hivyo, kwa sasa anafanya makosa mawili.
1. Anapeleka miradi kwake, kwa sababu ni kwake, si kwa sababu kuna priority ya kiuchumi.
2. Anapeleka miradi kwa kuchota fedha nje ya utaratibu, open tender, na bajeti.
Huu si uongozi bora, labda bora uongozi.
Hua naamini waafrika tukibebwa kama tulivyo tukapelekwa US na US wakabebwa kama walivyo wakaletwa africa haitapita mwezi tutakuja kuomba msaada Africa tena msaada wa tech mpya kutoka Africa manake hizo za tutakazokuta kule tutaua ndani ya mwezi
Unasema mamlaka zote zimetoka kwa Mungu.Ahahahhaha. Sawa mkuu. Mamlaka zote duniani zimetoka kwa Mungu kwa hiyo twapaswa kuziheshimu. Ila zile tetesi za kutawala milele zote ndo inabidi tuzipinge kwa nguvu zote. Maana huko kunakopelekewa pesa bila utaratibu kutakua kama ulaya ilihali wengme ni maskini wa kutupwa.
Ebu muone huyu member maoni yake juu ya watu weusi.
Inawezekana mleta mada umri wake ni mdogo, ni kijana. Sidhani kama anajua huyo Mobutu alikaa ikulu kwa miaka mingapi.
Uhakika uliopo ni kwamba JPM mwaka 2025 atamuachia kiti mrithi wake pale uwanja wa Uhuru kama Mungu akipenda.
Msuya aliendeleza upareni, Mrema akaendeleza uchagani, ukipewa nafasi ya urais ukashindwa hata kusomesha ndugu zako au kujenga mazingira yao ya maendeleo katika siku zijazo basi wewe ni mpumbavu wa mwisho.
QUICK ANSWERS COME FROM COPYING OTHERS' EASY MODELS!Neutral observers kwa kiswahili fasaha tunawaita ni 'wanafiki daraja la kwanza'.
Mkuu hakuna mimi na wewe tunachoweza kufanya katika kubadilisha hali iliyopo. Ni kujitakia sononeko na maumivu ya moyo pasipo kuwa na ulazima.Kama kuendeleza kwenu au kuwasaidia ndugu zako ufanye kwa pesa yako lakini sio ya walipa kodi. Hayo waliyoyafanya Msuya na Mrema yalikuwa ni makosa.
Kuna siku nilitembelea Butiama. Kulikuwa na Kampuni ya Ujenzi wa barabara ikifanya kazi kujenga barabara ya Makutano - Natta. Project Manager, raia wa Ethiopia akanikaribisha ofisini. Katika mazungumzo akaniambia kuwa hapo tulipokaa ndio palikuwa Ikulu ya Butiama. Na kwamba meza hiyo na chumba hicho ndiyo ilikuwa ofisi ya Mwalimu. Walikuwa wamepewa jengo lile na mke wa Baba wa Taifa watumie kama ofisi. Mwisho akaniambia kwa Kiingereza: "Your first President was a humble and a down to earth person. It is as if God wanted you Tanzanians to be a benchmark to the rest of Africa; a place where our leaders would come and learn the lessons of humbleness and humility."Wakti Baba wa Taifa anang'atuka hakuwa amejenga chochote pale Butiama.
Kwa vile alirudi kuishi kijijini na kukawa na Trip za mara kwa mara za Viongozi wa Kitaifa na kimataifa.....Mzee Ruksa akatumia Busara kwa kuliagiza Jeshi likamjengee nyumba angalao yenye hadhi ya mtu aliyewahi kuwa Rais wa nji hii.
Haya ndo yalikuwa maneno ya Mwalimu kwa JWTZ:''....MUNANI JENGEA NYUMBA KUBWA SANA KWANI MIMI TEMBO...??''
View attachment 1148125
View attachment 1148126
Lakini hapa Gbadolite ndani ya Kongo tunashuhudia mtu mmoja Dikteta Mobutu alijijengea Majumba (siyo jumba) makubwa wanpoweza kulala hata tembo kadhaa huku Wakongoman wengi wakiogelea kwene lindi la umaskini.
Hii ndiyo hasa akili ya Magufuli....no differences.
QUICK ANSWERS COME FROM COPYING OTHERS' EASY MODELS!
Mkuu hakuna mimi na wewe tunachoweza kufanya katika kubadilisha hali iliyopo. Ni kujitakia sononeko na maumivu ya moyo pasipo kuwa na ulazima.
Yale yale ya Dada Mange Kimambi, keyboard warrior. Wenye kudai haki wapo Sudan, wanakwenda barabarani kudai mabadiliko mpaka wanakuja kuyapata. Watanzania tunachokiweza ni kulialia hovyo tu.Wewe kama huna moyo wa kupigania haki wapishe watu wengine waendelee. Vitu vingine sio vya kufumbia macho
Yale yale ya Dada Mange Kimambi, keyboard warrior. Wenye kudai haki wapo Sudan, wanakwenda barabarani kudai mabadiliko mpaka wanakuja kuyapata. Watanzania tunachokiweza ni kulialia hovyo tu.
Bwana mdogo unaingiza matusi baada ya kuishiwa ya hoja, ushujaa wa watu wa aina yako ni wa kulalama humu mitandaoni, hamna jeuri ya kuidai hiyo haki mnayosema kuwa imeminywa kwa kuingia mtaani.Hakuna anayelia hapa. Ndio maana nikakwambia kama huna moyo wewe vaa shanga ukalale waache wanaume wa shoka wafanye kazi.
Bwana mdogo unaingiza matusi baada ya kuishiwa ya hoja, ushujaa wa watu wa aina yako ni wa kulalama humu mitandaoni, hamna jeuri ya kuidai hiyo haki mnayosema kuwa imeminywa kwa kuingia mtaani.
Za kwenu ni kelele za chura, hazina uwezo wa kuyafanya maji yakawa sio matamu kwenye mdomo wa Tembo.
Sio uwanja wa ndege tu, sasa kuna hifadhi ya wanyama inayokwenda kuongeza pato la taifa kupitia utalii.
Kaa huko na ndoto zako za kupenda kula pesa za wananchi. Na bado... mtaisoma namba hadi mnyooke