Heshima kwako mkuu.
Umechambua vizuri sana. Na hivi ndivyo twapaswa kuelezea mambo kuonesha pros and cons za miradi, na sio kishabiki kam wengi tunavyokua tunafanya. Kwamba kisa mm nimezaliwa Mbeya nikijenga Mbeya nimepapendelea.
Nyerere katika kipindi chake na mazingira ya nchi yetu ilikua tofauti sana.
1. Miundombinu ilikua mibovu na duni sana i.e barabara za mikoa na miko, wilaya na wilaya n.k, umeme, maji, hospital.
2. Elimu kwa watz; majority walikua hawana elimu. Ndo maana Nyerere alijikita sana kueneza elimu kufuta ujinga.
3. Uwezekaji ulikua mdogo sana na wengi walikua kwenye "Subsistence economy"
Kwa hiyo ni vigumu sana kufananisha mazingira ya nyerere na hali ya sasa.
Miji kama Mwanza, Geita na nchi ya Rwanda ni fursa kubwa kwa maeneo mingine ya jiran kibiashara. Hiyo miji ina watu wengi na ili kuendeleza biashara ndani ya hii miji inahitajika iwepo miji mingine maeneo jirani ya kibiashara ili uchumi wa ukanda husika uweze kua na "Multiplier effect....la sivyo biashara itajikuta ni Mwanza na Dsm,Mbeya, n.k
Ingawa mhe.alitakiwa pia aiangalie miji kama Musoma, Ngara, Biharamulo, Sirari, Shinyanga, Nyamongo, n.k ili kuhamasisha biashara na mji wake wa chato.
Mfano mji wa nyamongo, Geita, n.k una madini mengi sana angeboresha miundombinu na viwanja vya ndege ili kuleta ushindani ktk huo ukanda.
Kuna mdau humu ndani aliwahi kuleta mada kuhusu maendeleo kikanda akishauri ukanda flani ujitegemee wenyewe kimaendeleo kulingana na maliasili za ukanda husika. Yaani ukusanyaji kodi, allocation of resources etc visimamiwe na mamlaka (halimashauri) za ukanda huo.
Mfano Mwnza, Mara, Kagera, Geita (Ukanda wa ziwa) viwe na mamlaka ya ukusanyaji wa kodimgawanyo wake. Vivyo Hivyo kwa kanda zingne, pia kuwe na fungu la kwenda serikali kuu. serikali kuu ikiwa ni mshauri na pengme kuingila pale panapostahili.
Lkn hili kwa sasa naona linafanyika indirectly kwan kama maeneo duni katka ukanda flan yanajengwa na kuimarisha ni hatua nzuri ya kuelekea point ya maendeleoya ushindani kikanda.
Wito tu sheria na taratibu zifuatwe ktk allocation of Scarce resources we have, na haki itendeke.