Hapa ni Gbadolite, Kijijini kwa dikiteta Mobutu Sesseko Kuku Wazabanga, nyumba zimegeuka Magofu na mahame

Hapa ni Gbadolite, Kijijini kwa dikiteta Mobutu Sesseko Kuku Wazabanga, nyumba zimegeuka Magofu na mahame

Andika vitu kwa facts sio unaongea kama upo kijiweni. Huyu mtoa mada ameweka mpaka vielelezo vya picha. Na wewe tupe facts zako
Inawezekana mleta mada umri wake ni mdogo, ni kijana. Sidhani kama anajua huyo Mobutu alikaa ikulu kwa miaka mingapi.

Uhakika uliopo ni kwamba JPM mwaka 2025 atamuachia kiti mrithi wake pale uwanja wa Uhuru kama Mungu akipenda.

Msuya aliendeleza upareni, Mrema akaendeleza uchagani, ukipewa nafasi ya urais ukashindwa hata kusomesha ndugu zako au kujenga mazingira yao ya maendeleo katika siku zijazo basi wewe ni mpumbavu wa mwisho.
 
Heshima kwako mkuu.

Umechambua vizuri sana. Na hivi ndivyo twapaswa kuelezea mambo kuonesha pros and cons za miradi, na sio kishabiki kam wengi tunavyokua tunafanya. Kwamba kisa mm nimezaliwa Mbeya nikijenga Mbeya nimepapendelea.

Nyerere katika kipindi chake na mazingira ya nchi yetu ilikua tofauti sana.
1. Miundombinu ilikua mibovu na duni sana i.e barabara za mikoa na miko, wilaya na wilaya n.k, umeme, maji, hospital.

2. Elimu kwa watz; majority walikua hawana elimu. Ndo maana Nyerere alijikita sana kueneza elimu kufuta ujinga.
3. Uwezekaji ulikua mdogo sana na wengi walikua kwenye "Subsistence economy"

Kwa hiyo ni vigumu sana kufananisha mazingira ya nyerere na hali ya sasa.

Miji kama Mwanza, Geita na nchi ya Rwanda ni fursa kubwa kwa maeneo mingine ya jiran kibiashara. Hiyo miji ina watu wengi na ili kuendeleza biashara ndani ya hii miji inahitajika iwepo miji mingine maeneo jirani ya kibiashara ili uchumi wa ukanda husika uweze kua na "Multiplier effect....la sivyo biashara itajikuta ni Mwanza na Dsm,Mbeya, n.k
Ingawa mhe.alitakiwa pia aiangalie miji kama Musoma, Ngara, Biharamulo, Sirari, Shinyanga, Nyamongo, n.k ili kuhamasisha biashara na mji wake wa chato.

Mfano mji wa nyamongo, Geita, n.k una madini mengi sana angeboresha miundombinu na viwanja vya ndege ili kuleta ushindani ktk huo ukanda.

Kuna mdau humu ndani aliwahi kuleta mada kuhusu maendeleo kikanda akishauri ukanda flani ujitegemee wenyewe kimaendeleo kulingana na maliasili za ukanda husika. Yaani ukusanyaji kodi, allocation of resources etc visimamiwe na mamlaka (halimashauri) za ukanda huo.
Mfano Mwnza, Mara, Kagera, Geita (Ukanda wa ziwa) viwe na mamlaka ya ukusanyaji wa kodimgawanyo wake. Vivyo Hivyo kwa kanda zingne, pia kuwe na fungu la kwenda serikali kuu. serikali kuu ikiwa ni mshauri na pengme kuingila pale panapostahili.

Lkn hili kwa sasa naona linafanyika indirectly kwan kama maeneo duni katka ukanda flan yanajengwa na kuimarisha ni hatua nzuri ya kuelekea point ya maendeleoya ushindani kikanda.

Wito tu sheria na taratibu zifuatwe ktk allocation of Scarce resources we have, na haki itendeke.
Magufuli anachota hela bila kufuata sheria na utaratibu.

Hata kama angepeleka hela kwenye most deserving location (which he doesn't) angekuwa bado aakosea kwa kupeleka hela nje ya utaratibu.

Kwa hivyo, kwa sasa anafanya makosa mawili.

1. Anapeleka miradi kwake, kwa sababu ni kwake, si kwa sababu kuna priority ya kiuchumi.

2. Anapeleka miradi kwa kuchota fedha nje ya utaratibu, open tender, na bajeti.

Huu si uongozi bora, labda bora uongozi.
 
Ahahahhaha. Sawa mkuu. Mamlaka zote duniani zimetoka kwa Mungu kwa hiyo twapaswa kuziheshimu. Ila zile tetesi za kutawala milele zote ndo inabidi tuzipinge kwa nguvu zote. Maana huko kunakopelekewa pesa bila utaratibu kutakua kama ulaya ilihali wengme ni maskini wa kutupwa.

Ebu muone huyu member maoni yake juu ya watu weusi.

Hua naamini waafrika tukibebwa kama tulivyo tukapelekwa US na US wakabebwa kama walivyo wakaletwa africa haitapita mwezi tutakuja kuomba msaada Africa tena msaada wa tech mpya kutoka Africa manake hizo za tutakazokuta kule tutaua ndani ya mwezi
 
Ahahahhaha. Sawa mkuu. Mamlaka zote duniani zimetoka kwa Mungu kwa hiyo twapaswa kuziheshimu. Ila zile tetesi za kutawala milele zote ndo inabidi tuzipinge kwa nguvu zote. Maana huko kunakopelekewa pesa bila utaratibu kutakua kama ulaya ilihali wengme ni maskini wa kutupwa.

Ebu muone huyu member maoni yake juu ya watu weusi.
Unasema mamlaka zote zimetoka kwa Mungu.

Unaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo na hizo habari si uongo tu unajazwa na watu kama wewe?
 
Inawezekana mleta mada umri wake ni mdogo, ni kijana. Sidhani kama anajua huyo Mobutu alikaa ikulu kwa miaka mingapi.

Uhakika uliopo ni kwamba JPM mwaka 2025 atamuachia kiti mrithi wake pale uwanja wa Uhuru kama Mungu akipenda.

Msuya aliendeleza upareni, Mrema akaendeleza uchagani, ukipewa nafasi ya urais ukashindwa hata kusomesha ndugu zako au kujenga mazingira yao ya maendeleo katika siku zijazo basi wewe ni mpumbavu wa mwisho.

Kama kuendeleza kwenu au kuwasaidia ndugu zako ufanye kwa pesa yako lakini sio ya walipa kodi. Hayo waliyoyafanya Msuya na Mrema yalikuwa ni makosa.
 
Wakti Baba wa Taifa anang'atuka hakuwa amejenga chochote pale Butiama.
Kwa vile alirudi kuishi kijijini na kukawa na Trip za mara kwa mara za Viongozi wa Kitaifa na kimataifa.....Mzee Ruksa akatumia Busara kwa kuliagiza Jeshi likamjengee nyumba angalao yenye hadhi ya mtu aliyewahi kuwa Rais wa nji hii.
Haya ndo yalikuwa maneno ya Mwalimu kwa JWTZ:'
'....MUNANI JENGEA NYUMBA KUBWA SANA KWANI MIMI TEMBO...??''

View attachment 1148125
View attachment 1148126

Lakini hapa Gbadolite ndani ya Kongo tunashuhudia mtu mmoja Dikteta Mobutu alijijengea Majumba (siyo jumba) makubwa wanpoweza kulala hata tembo kadhaa huku Wakongoman wengi wakiogelea kwene lindi la umaskini.
Hii ndiyo hasa akili ya Magufuli....no differences.
Kuna siku nilitembelea Butiama. Kulikuwa na Kampuni ya Ujenzi wa barabara ikifanya kazi kujenga barabara ya Makutano - Natta. Project Manager, raia wa Ethiopia akanikaribisha ofisini. Katika mazungumzo akaniambia kuwa hapo tulipokaa ndio palikuwa Ikulu ya Butiama. Na kwamba meza hiyo na chumba hicho ndiyo ilikuwa ofisi ya Mwalimu. Walikuwa wamepewa jengo lile na mke wa Baba wa Taifa watumie kama ofisi. Mwisho akaniambia kwa Kiingereza: "Your first President was a humble and a down to earth person. It is as if God wanted you Tanzanians to be a benchmark to the rest of Africa; a place where our leaders would come and learn the lessons of humbleness and humility."
Nikiifikiria CCM ya hawa mbwa mwitu wanaovaa ngozi ya kondoo, machozi yalinitoka!!!
Hakuendelea tena na mazungumzo, ikabidi kuaendelea na shughuli iliyonipeleka pale.
 
Mkuu hakuna mimi na wewe tunachoweza kufanya katika kubadilisha hali iliyopo. Ni kujitakia sononeko na maumivu ya moyo pasipo kuwa na ulazima.

Wewe kama huna moyo wa kupigania haki wapishe watu wengine waendelee. Vitu vingine sio vya kufumbia macho
 
Wewe kama huna moyo wa kupigania haki wapishe watu wengine waendelee. Vitu vingine sio vya kufumbia macho
Yale yale ya Dada Mange Kimambi, keyboard warrior. Wenye kudai haki wapo Sudan, wanakwenda barabarani kudai mabadiliko mpaka wanakuja kuyapata. Watanzania tunachokiweza ni kulialia hovyo tu.
 
Yale yale ya Dada Mange Kimambi, keyboard warrior. Wenye kudai haki wapo Sudan, wanakwenda barabarani kudai mabadiliko mpaka wanakuja kuyapata. Watanzania tunachokiweza ni kulialia hovyo tu.

Hakuna anayelia hapa. Ndio maana nikakwambia kama huna moyo wewe vaa shanga ukalale waache wanaume wa shoka wafanye kazi.
 
Hakuna anayelia hapa. Ndio maana nikakwambia kama huna moyo wewe vaa shanga ukalale waache wanaume wa shoka wafanye kazi.
Bwana mdogo unaingiza matusi baada ya kuishiwa ya hoja, ushujaa wa watu wa aina yako ni wa kulalama humu mitandaoni, hamna jeuri ya kuidai hiyo haki mnayosema kuwa imeminywa kwa kuingia mtaani.

Za kwenu ni kelele za chura, hazina uwezo wa kuyafanya maji yakawa sio matamu kwenye mdomo wa Tembo.

Sio uwanja wa ndege tu, sasa kuna hifadhi ya wanyama inayokwenda kuongeza pato la taifa kupitia utalii.
 
Hizo "kelele za chura" ndizo zilizofanya serikali kuufyata na kubadili sheria za takwimu. Nchi yetu bado ni ombaomba kwahiyo wapinzani wao wanaongea moja kwa moja na walioshika mpini ambao nyie mnawaita mabeberu halafu wao wanatoa amri kifanyike nini.
 
Kaa huko na ndoto zako za kupenda kula pesa za wananchi. Na bado... mtaisoma namba hadi mnyooke
1149460

🙄😀😀😀
 
Tujikumbushe vituko vya huyu jamaa aliyewahi kuwa Raisi wa zamani wa Zaire. Mobutu Sese Seko Kuku Gbendu Wa Za Banga. Moja ya vitu alifanya huyu bwana mkubwa vilivyoushangaza uliwengu ni kitendo chake cha kutumia mamilioni ya dola na kwenda kubadilisha Gbadolite ( kijijini alipozaliwa) kuwa paradiso ndogo. Kwanza Alijenga bwawa la kuzalisha umeme karibu na mto Ubangi, uwanja wa ndege wa Gbadolite, Kasri kubwa na hoteli alotumia kama makazi na sehemu ya kupokelea wageni wake. Gbadolite pia kulikuwa na makampuni makubwa kama vile CDIA Zaire kwa ajili ya kilimo. SOZAGEC kampuni ya ujenzi wa barabara na SAFRICAS kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi kulikuwa pia na hospitali kubwa iliyokuwa na vifaa vya kisasa ambayo iliharibiwa vibaya mwaka 1997. Mobutu pia alijenga kanisa kubwa sana lililojulikana kama Chapelle Marie la Misericorde ambapo huko ndipo alimzika mkewe mama mobutu.
Mwandishi na mpiga picha wa gazeti Guardian la uingereza bwana Sean Smith alisafiri mpaka Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo iliyokuwa zaire na kutuletea picha ya yaliyomo Gbadolite ya sasa.

https://www.theguardian.com/cities/...e-mobutu-ruined-jungle-city-in-pictures#img-1

Hii ni iliyokuwa air-traffic control tower ya Gbadolite international airport, ambayo runway yake ilikuwa ndefu kuwezesha ndege aina ya Concorde kutua (concorde zilikuwa ndege maarufu kubwa za abiria miaka ya 1979 hadi 2003 zilizokuwa na uwezo wa kubeba abiria 92 hadi 128.
Picha zote na Sean Smith wa gazeti la Guardian la uingereza

Gbadolite: the airport and air traffic control tower.

  • hapa ni ndani ya air control tower iliyotelekezwa kama inavyoonekana.

    Gbadolite: the control tower  at Mobutu's airport.

  • Hii ni VIP arrivals terminal: sehemu ya kupokelea wageni muhimu ambapo watu maarufu kama vile Pope John Paul II, UN secretary-general Boutros Boutros Ghali walipita hapa.
    Gbadolite: the VIP arrivals terminal at Mobutu's airport.

    Hapa ni ndani main airport terminal

    Gbadolite: the main terminal at Mobutu's airport.

  • Gbadolite: the main terminal at Mobutu's airport.

  • hili ni jengo la wizara ya Maji ambalo halikumalizika na sasa linatumika kama shule.
    Gbadolite: the Water Ministry building never finished and now used as a school.
  • ndani ya shule
    Gbadolite: the Water Ministry building never finished and now used as a school.

  • Hii inaitwa Motel Nzekele, iliyojengwa na mobutu kijijini kwao. ilikuwa na hadhi ya nyota tano kipindi inafunguliwa mwaka 1979.

    Gbadolite: the Motel Nzekele, built by Mobutu

  • Bwawa tupu la kuogelea kama linavyoonekana kwa picha. wageni mblimbali mashuhuri wanaoripotiwa kufika katika moteli hii ni pamoja na Papa wa kanisa katoliki, mfalme wa Ubelgiji, na raisi wa ufaransa , François Mitterrand

    Gbadolite: the Motel Nzekele, built by Mobutu, with now-empty swimming pool.

  • kumbi ya kuangalia cinema Motel Nzekel

    Gbadolite: inside the Motel Nzekele

  • Picha ya daraja ambalo halikufanikiwa kumalizika kwatika kijiji cha Gbadolite

    Gbadolite: an unfinished bridge in Gbadolite

  • Hili ni geti la kuingilia makazi binafsi ya Mobutu kijijini kwao. wakazi wa hapa wanatoza dola 20 kwa wageni kuingia na kutazama.
    Gbadolite: the main gates and entrance to the private palace of President Mobutu.

  • Gbadolite: the entrance to the private palace of President Mobutu

  • Gbadolite: the ruins of the private palace of President Mobutu.

  • Gbadolite: the private palace of President Mobutu. A relative stands in the disused swimming pool.

  • Kwa majina mengine walipaita Mobutu’s palace. katika makazi haya waliajiriwa wafanyakazi zaidi ya 700 staff wakiwemo wapishi, vijakazi na wanajeshi 300 soldiers

    Gbadolite: the private palace of President Mobutu.

  • Ndani ya viwanja vya kasri la mobutu ambapo taratibu pameanza kumezwa na vichaka.

    Gbadolite: the private palace of President Mobutu.

  • Gbadolite: the president's ruined bedroom.
  • Hii ilikuwa chemchem ya ndani ya kasri hilo iliyokuwa na sanamu la simba lililochongwa wa ustadi wa hali ya juu.
    Gbadolite: the private palace of President Mobutu.
 
Back
Top Bottom