Hapa ni Gbadolite, Kijijini kwa dikiteta Mobutu Sesseko Kuku Wazabanga, nyumba zimegeuka Magofu na mahame

Hapa ni Gbadolite, Kijijini kwa dikiteta Mobutu Sesseko Kuku Wazabanga, nyumba zimegeuka Magofu na mahame

Mzee baba mimi ni mtetezi wake ila kwa haya ya airport na mataa na mabenki yasiyo jengwa kwa kuangalia wingi wa wateja na fursa halisi simuungi mkono hata kidogo.

Hii ni 'precedent' mbaya sana kwa viongozi watakaomfuatia.
Mimi ndiye nitakayemfuata, haki ya nani nawaahidi watanzania wenzangu, chochote alichojenga hapo lazima nikivunjevunje! Sitajali gharama iliyotumika maana ni upumbavu huu anaotufanyia!
 
Mzee baba mimi ni mtetezi wake ila kwa haya ya airport na mataa na mabenki yasiyo jengwa kwa kuangalia wingi wa wateja na fursa halisi simuungi mkono hata kidogo.

Hii ni 'precedent' mbaya sana kwa viongozi watakaomfuatia.
Ni kweli, akija rais kutoka Nachingwea, n.k naye anaweza jenga airport kijijini kwake. Africa kusonga mbele ni kazi kweli kweli
 
Wakongo walishindwa kuyataifisha na kuyaendeleza haya makazi ? Nafikiri hata serikali za sasa nazo zina matatizo kichwani. Hiyo ni pesa ya walipa kodi inateketea !
 
Kwa hiyo unatetea kitu gani basi?! Au unalipwaa yaani professional praise singer? Kama wachina wanaolipwa kilioni wakalia sana wakati msiba hauwahusu?!
Nasifia na kutetea yale mazuri yake.
Nakosoa na kupinga yale mabaya yake.

Utaifa kwanza. Mimi sio kada, Kada wa chama chochote ni kusifia tu au kukosoa tu kulingana na mlengo au maagizo ya chama chake.

Mwaka 2015 nilimchagua Magufuli, lakini 2010 nilimchagua Dr.Slaa.
Nachagua kiongozi(mtu) sichagui chama.
 
Mleta mada naona unaendana na ule msemo wa dua la kuku halimpati mwewe.

Huwezi kumlinganisha Mobutu na JPM, ni watu wawili tofauti kabisa katika suala la maono yao.
 
KWANINI HAPAWI MAKUMBUSHO AU HATA KUJENGWA KACHUO FULANI HATA KA UONGOZI BORA?
CHUKI ZISITUPUMBAZE WAAFRIKA!
Labda Chuo cha Uongozi Hovyo maana uongozi wa Awamu hii ni mbaya kwa kila kitu. Toka kuingia madarakani hakuna chochote walichojaribu kufanya kilichofanikiwa. Maneno ndio mengi lakini vitendo hakuna hata wakiongoza miaka 20 hakuna cha maana kitafanyika watatuachia magofu tu pamoja na uwanja wa Chato.
 
Wakongo ni wapuuzi....si waibadirishe hio ikulu kuwa shule au chuo..

Au mwana mmoja ajimilikishe aishi zake flesh..
Mimi siwezi acha pesa zangu za kodi kuwa magofu ...ningeenda kuishi pale
 
Watawala wote wa kiimla waga hawajifunzi kutokana na historia ni watu very conservative, waga wana mapepo sugu sana.
 
Wakongo walishindwa kuyataifisha na kuyaendeleza haya makazi ? Nafikiri hata serikali za sasa nazo zina matatizo kichwani. Hiyo ni pesa ya walipa kodi inateketea !
Mutex iko pale Musoma, unajua iko ktk hali gani, mbona usiwambie wakaiendeleze.
 
Nasifia na kutetea yale mazuri yake.
Nakosoa na kupinga yale mabaya yake.

Utaifa kwanza. Mimi sio kada, Kada wa chama chochote ni kusifia tu au kukosoa tu kulibgana na mlengo au maagizo ya chama chake.

Mwaka 2015 nilimchagua Magufuli, lakini 2010 nilimchagua Dr.Slaa.
Nachagua kiongozi(mtu) sichagui chama.
Hakuna wewe ni kada
 
Back
Top Bottom