Tujikumbushe vituko vya huyu jamaa aliyewahi kuwa Raisi wa zamani wa Zaire. Mobutu Sese Seko Kuku Gbendu Wa Za Banga. Moja ya vitu alifanya huyu bwana mkubwa vilivyoushangaza uliwengu ni kitendo chake cha kutumia mamilioni ya dola na kwenda kubadilisha Gbadolite ( kijijini alipozaliwa) kuwa paradiso ndogo. Kwanza Alijenga bwawa la kuzalisha umeme karibu na mto Ubangi, uwanja wa ndege wa Gbadolite, Kasri kubwa na hoteli alotumia kama makazi na sehemu ya kupokelea wageni wake. Gbadolite pia kulikuwa na makampuni makubwa kama vile CDIA Zaire kwa ajili ya kilimo. SOZAGEC kampuni ya ujenzi wa barabara na SAFRICAS kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi kulikuwa pia na hospitali kubwa iliyokuwa na vifaa vya kisasa ambayo iliharibiwa vibaya mwaka 1997. Mobutu pia alijenga kanisa kubwa sana lililojulikana kama
Chapelle Marie la Misericorde ambapo huko ndipo alimzika mkewe mama mobutu.
Mwandishi na mpiga picha wa gazeti Guardian la uingereza bwana Sean Smith alisafiri mpaka Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo iliyokuwa zaire na kutuletea picha ya yaliyomo Gbadolite ya sasa.
President Mobutu's ruined jungle paradise, Gbadolite - in pictures
Hii ni iliyokuwa air-traffic control tower ya Gbadolite international airport, ambayo runway yake ilikuwa ndefu kuwezesha ndege aina ya Concorde kutua (concorde zilikuwa ndege maarufu kubwa za abiria miaka ya 1979 hadi 2003 zilizokuwa na uwezo wa kubeba abiria 92 hadi 128.
Picha zote na Sean Smith wa gazeti la Guardian la uingereza
hapa ni ndani ya air control tower iliyotelekezwa kama inavyoonekana.

Hii ni VIP arrivals terminal: sehemu ya kupokelea wageni muhimu ambapo watu maarufu kama vile Pope John Paul II, UN secretary-general Boutros Boutros Ghali walipita hapa.

Hapa ni ndani main airport terminal


hili ni jengo la wizara ya Maji ambalo halikumalizika na sasa linatumika kama shule.

- ndani ya shule

Hii inaitwa Motel Nzekele, iliyojengwa na mobutu kijijini kwao. ilikuwa na hadhi ya nyota tano kipindi inafunguliwa mwaka 1979.

Bwawa tupu la kuogelea kama linavyoonekana kwa picha. wageni mblimbali mashuhuri wanaoripotiwa kufika katika moteli hii ni pamoja na Papa wa kanisa katoliki, mfalme wa Ubelgiji, na raisi wa ufaransa , François Mitterrand

kumbi ya kuangalia cinema Motel Nzekel

Picha ya daraja ambalo halikufanikiwa kumalizika kwatika kijiji cha Gbadolite

Hili ni geti la kuingilia makazi binafsi ya Mobutu kijijini kwao. wakazi wa hapa wanatoza dola 20 kwa wageni kuingia na kutazama.




Kwa majina mengine walipaita Mobutu’s palace. katika makazi haya waliajiriwa wafanyakazi zaidi ya 700 staff wakiwemo wapishi, vijakazi na wanajeshi 300 soldiers

Ndani ya viwanja vya kasri la mobutu ambapo taratibu pameanza kumezwa na vichaka.


- Hii ilikuwa chemchem ya ndani ya kasri hilo iliyokuwa na sanamu la simba lililochongwa wa ustadi wa hali ya juu.
