The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Sie bure, wewe utakuwa ni mhanga wa zile issue za mishahara hewa. Mirija ilipobanwa lazima njaa iingie nyumbani.
Kumbuka mkuu kwamba njia yetu ni moja. Siku yako ya kulala na wewe itafika ukiwaacha wengine wakiendelea kulifurahia jua.
1. Mimi siyo muhanga wa mishahara hewa. Niko fixed na kipato changu binafsi.
2. Yes, wote tutakufa. Tunakufaje na kwa sababu gani? Hii ndiyo tafauti...
Yaani nitakavyokufa mimi na utakavyokufa wewe ni tofauti kabisa. Ni tafauti kabisa na alivyokufa Magufuli...
Sikiliza ndugu;
Kuna watu huwa wanaandaa na kuikaribisha mauti/kifo kwa makusudi na kwa haraka kabla ya wakati wao kwa nguvu na kwa mikono yao mwenyewe...
Magufuli ni mmoja wao...
Huyu bwana ni mtu aliyekuwa na chuki, dharau, visasi, kiburi, majivuno, roho ya uuaji na tabia zinazofanana na hizo. Kwanini asife vibaya na mapema...?
Alikuwa anaumiza na kuua/kumwaga damu za watu wasio na hatia, yeye angebakije hai na salama....? Impossible..
Huku ni kujiua mwenyewe. Ndiyo maana ya unakufaje na kwa sababu gani..!