Pole. Kama mko kwenye hatua za uchumba za kuchunguzana,chukulia kwamba huyo hatakuwa mume sahihi kwako.
Wanawake huwa mnaongozwa na hisia kuliko akili. Mwanamke akimpenda kweli mtu halafu akasalitiwa anaweza kufanya jambo lolote kuua au kujiua.
Kuna dada mmoja aliwahi kutaka kujiua kwa sababu yangu.
Nilikuwa nae kwenye uchumba na kwa wakati huo alikuwa ndo amepata kazi hata hajamaliza miezi mitatu akiwa kazini na alikuwa amepanga chumba anaishi peke yake. Nilichompendea ,the girl was very smart kuna mambo mengi alinibadilisha ambayo nilikuwa na mtazamo mbaya nayo na alikuwa anajitambua.
Sasa tulikuwa tunapiga stori muda mwingi mpaka stori zinaisha.Akaanza tabia ya kunisimulia namna anavyoishi akiwa kazini bila kuficha chochote. Akaniambia namna manager wake ambaye ni boss wake kwenye ofisi yao anavyomsumbua kumtongoza lakini anamkataa na aliniambia alimkataa kwa sababu anajua tayari boss wake ana mke wake nyumbani anamuona kama boss wake ni umalaya tu ndo unamsumbua. Akawa ananisimulia namna wafanyakazi wa kiume hapo ofisini wanapenda kutongoza wadada wanaokuja kupata huduma kwenye ofisi yao. Akanisimulia kwamba kuna mfanyakazi mmoja pia wa kiume ofisini kwao alimtongoza akamwambia tayari ana mtu lakini yule mfanyakazi mwenzake akamkazia akataka wapange mpango aende akamle kwamba itakuwa ni siri yao mimi sitajua. Girl alikuwa open sana kwangu aliniambia mambo yake mengi ya sirini mpaka aliniambia namna boss wake alivyokuwa anamuwekea mitego amle binti anachomoa mitego mpaka yule boss alianza kumuwekea chuki na kuanza kumpa tuadhabu adhabu hapo ofisini kwao.
Binti akawa anapewa kazi za ziada za kujaza data kwenye mifumo ya computer ya ofisi na boss wake ili abaki mpaka usiku ofisini peke yake na boss. Ilifikia hatua binti akaanza kumdharau boss wake, akawa hatii boss wake anacho muambia. Muda mwingine akawa anatoka kazini muda anaotaka yeye au kazini anaenda muda anaotaka yeye.Kuna wakati nilikuwa nachati nae mida ya saa ya sita akaniambia eti ndo alikuwa anajiandaa aende kazini.Nikawa namtania unaenda kazini saa sita !!! Katika utani wangu nami nikawa naingizia kuidharau ofisi yao baadae nikamwambia "ndo maana wafanyakazi wa serikalini huwa mnalalamikiwa huduma zenu mbovu." Girl akajitetea kwamba manager wake ambaye ndo boss wake hayupo ameenda kwenye semina.
Wakati wote girl ananisimulia mambo yake ya sirini sababu alikuwa ananiamini, Mimi nilikuwa simwambii siri zangu. Siku moja wakati tumetoka out , nikamjaribu kama nikisha muoa na tukiwa ndani ya ndoa akagundua nina mchepuko atafanya nini!!!. Akaniambia kwanza akishaingia kwenye ndoa hatakuwa anajihangaisha kukagua simu yangu hata nikiwa na mchepuko kwake haina shida muhimu niwe nazingatia kuijali familia yetu mimi na yeye. Baadaye nikamwambia namuhakikisha kwamba sitachepuka . Baada ya kauli yangu kwamba sitachepuka ulizuka ubishi wa nguvu, girl alikataa kata kata kwamba siwezi kuacha kuchepuka.Girl akasema wanaume wa karne hii hakuna asiyechepuka.
Baada ya siku hiyo nilianza kuitafakari kauli yake kwamba "Wanaume wa karne hii hakuna asiyechepuka."Nikawa nazitafakari stori zake za namna maisha yalivyo kazini kwao,nikaanza kuingiwa na wivu. Nafsi yangu ikaanza kuniambia girl itakuwa ameshaliwa na boss wake au yule mfanyakazi mwenzake pale ofisini!!! Wivu ukazidi kuwaka moyoni mwangu.
Nikapanga nimjaribu zaidi ili nijue mbivu na mbichi kama yaliyomo yamo.
Nikachati na girl mwingine kimahaba halafu sms sikuzifuta. Nikamtoa out tena huyu girl niliyenae halafu nikategesha zile sms azione. Girl akafanikiwa kuziona na kuzisoma. Weee!!! Girl aliumia akaondoka na hasira zinajaa simtank zima.
Baadae jioni nikawa nampigia simu hapokei.Natuma sms najitetea girl hajibu sms hata moja.Baada ya kuona sms zimekuwa nyingi,akajibu kinyonge "Nilikuamini sana Gamic,moyo wangu unauma sana. Nahisi maumivu makali moyoni.Maumivu ninayoyasikia ni kama nimechanwa na kisu moyoni mwangu". Baada ya girl kunijibu , mimi nikafarijika nikajua sasa ataendelea kuchat na mimi. Nikaendelea kutuma sms nyingi sana za kumbembeleza,girl hajibu.
Nikaacha kutuma sms . Akili ikaniambia niende kwake maana akiwa anaishi peke yake. Nafika nagonga hodi mlango wake girl hajibu.Nikagonga sana hodi , girl hajibu.
Nikatikisa kitasa bahati nzuri alikuwa hajafunga mlango kwa ndani,mlango ukafunguka nikaingia.Nikakuta girl amejilaza kitandani,pembeni yake kuna vidonge vingi na dompo. Kumbe girl tulivyoachana nae alienda kununua vidonge vingi na dompo. Akaanza kunifukuza eti niondoke anataka kujiua.
What!!! Nikaanza ku-please asijiue.
Huku ninacheka,nikamwambia "Nilikuwa nakuona wewe una akili,ni smart,unanitambua lakini girl kujiua ni jambo la kijinga zaidi.You are more than this. Umejifikiria watu wanaokufahamu watapata maumivu kiasi baada ya wewe kujiua,mama yako, wafanyakazi kazi wenzako kazini,taifa linakutegemea."
Baada ya kazi nzito ya kumbembeleza na kumsihi asifanye ujinga,Girl alifungua moyo. Akapika tukala chakula. Mimi nikavichukua vile vidonge na ile dompo nikaondoka navyo.Nikamtakia Usiku mwema.
Moral of the story: Siku hizi hakuna mahaba. Usimpende mtoto wa mtu mpaka ukawa unamuona yeye ndiye dunia yako.Unamuona kwamba bila yeye huwezi kuishi.Usimpende mtoto wa mtu mpaka unafikia hatua akikusaliti unataka kumchoma kisu kumuua.