Hapa Rujewa, Mbarali umeme kwa sasa ni kitu ghali mno na nadra sana kupatikana

jitombashisho

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2020
Posts
667
Reaction score
2,245
Ndiyo,ni hapa Rujewa.

Leo ni karibu miezi 6 sasa upatikanaji wa umeme hapa Rujewa ni wa kiwango Duni ambacho hakielezeki!

Mfano, kwa wiki moja upatikanaji wa umeme hauzidi masaa 48 na tatizo halieleweki ni nini.

Mbaya zaidi, si Tanesco ama kiongozi yeyote hawasemi ama kutangaza kama upo mgawo wa umeme unaoendelea.

Tatizo hilo la kutopatikana kwa umeme limesababisha hasara kubwa kwa wakulima na wafanyabiashara wa zao la mpunga hali inayopelekea kutokukobolewa kwa wakati mazao yao.

RiP JPM!
 
Umeme umekuwa ni kaa la moto, ngoja tuone stiglaz itajaa maji yapi maana naona mvua msimu huu bado ni chenga...
 
Ndiyo,ni hapa Rujewa.

Leo ni karibu miezi 6 sasa upatikanaji wa umeme hapa Rujewa ni wa kiwango Duni ambacho hakielezeki!

Mfano, kwa wiki moja upatikanaji wa umeme hauzidi masaa 48 na tatizo halieleweki ni nini.

Mbaya zaidi, si Tanesco ama kiongozi yeyote hawasemi ama kutangaza kama upo mgawo wa umeme unaoendelea.

Tatizo hilo la kutopatikana kwa umeme limesababisha hasara kubwa kwa wakulima na wafanyabiashara wa zao la mpunga hali inayopelekea kutokukobolewa kwa wakati mazao yao.

RiP JPM!
 
Tunashukuru kwa taarifa tafadhali tusaidie namba yako ya simu kwa urahisi wa kufatilia na kuchukua hatua stahiki

TANESCO Makao Makuu

Huduma kwa Wateja
 
Mmeshatajiwa eneo lenye tatizo.

Namba ya mtoa habari ya nini tena?

Kwenye hilo eneo hamna watendaji wa TANESCO? kwanini msiwawasiliane na hao watendaji wenu na mkatupatia majibu sahihi?
 
Mmeshatajiwa eneo lenye tatizo.
Namba ya mtoa habari ya nini tena.?
Kwenye hilo eneo hamna watendaji wa TANESCO? kwanini msiwawasiliane na hao watendaji wenu na mkatupatia majibu sahihi?
Tafadhali tambua msingi bora wa huduma kwa wateja umejangwa kwenye mambo kadhaa kubwa zaidi ni kupata taarifa kamili, kuzifanyia kazi na kumpa mrejesho mteja kwa ufanisi zaidi
 
Ofisi yao si ipo Kidatu pale?
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
Tafadhali tambua msingi bora wa huduma kwa wateja umejangwa kwenye mambo kadhaa kubwa zaidi ni kupata taarifa kamili, kuzifanyia kazi na kumpa mrejesho mteja mwa ufanisi zaidi
Pumba nyie kma ndio nyie acheni porojo za urojo fanyeni kazi
 
Tunashukuru kwa taarifa tafadhali tusaidie namba yako ya simu kwa urahisi wa kufatilia na kuchukua hatua stahiki

TANESCO Makao Makuu

Huduma kwa Wateja

Ninyi mmeelezwa tatizo namba ya simu ya nini, HAYA matatizo ya kukatika umeme yamekua sugu sana nchini
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
Ikitokea shoti ya umeme, nguzo kuanguka na kuhatarisha maisha ya watu mngesubiri namba ya simu humu?
 
Taarifa ili ifanyiwe kazi inapaswa itusaidie kukuhudumia. Tupo kuwahudumia wapendwa wateja wetu
 
Back
Top Bottom