Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kheri ya siku ya kuzaliwa BABA MAGUFULINi Oktoba 29, 1959 siku ambayo Mwenyezi Mungu alitupa Watanzania zawadi ya Mtoto John Pombe Magufuli ambaye Leo hii tunamkumbuka kama Mkombozi, Shujaa, Mtetezi, Mlezi, Mjenzi wa Watanzania,leo hii kwa Afrika ukilitaja jina la John Pombe Magufuli ni nembo ya uongozi wa mfano Afrika na Duniani kote.Leo hii John Pombe Magufuli ni tafsiri sahihi ya Uongozi bora wa mwana wa kweli wa Afrika,kwa Watanzania John Pombe Magufuli ni Rais wa mioyo ya wanyonge aliyeirudishia Tanzania heshima na utukufu wake!
John Pombe Magufuli mtu ambae amefanya kazi na watanzania bara miaka zaidi ya 20 akiwa ni Field Public Leader tangu akiwa Naibu Waziri miaka ya 1995 kisha Waziri kamili miaka ya 2000,2005,2010 katika wizara zaidi ya tano kwa miaka ishirini na baadaye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015 kwa miaka zaidi ya ishirini na tano,John Pombe Magufuli alilitumikia Taifa la Tanzania na kuwa mfano wao wa kiongozi bora,Watanzania wana performance appraisal ya kiongozi wao bora,Watanzania wote wanajua kuwa John Pombe Magufuli ndiye kipimo cha uongozi wanaouhitaji,Hayati Rais John Pombe Magufuli alikuwa Champion katika mambo mengi na kila mwananchi analijua hilo
Utendaji wa Hayati Rais John Pombe Magufuli na kazi zake zipo wazi nchi nzima,alikuwa ni mmoja wa Viongozi wachache sana Wazalendo wa kweli kutoka moyoni,wakweli kwa Wananchi wanyonge nchi nzima ya Tanzania,Hayati Rais John Pombe Magufuli alikuwa msemaji wa wale wasiokua na sauti,na kwa kuwasemea wanyonge na masikini,dunia nzima ililitaja jina lake,alipoongea kijijini kwake Chato,wazungu walimjibu kutoka London na Washngton,huyu ndiye John Pombe Magufuli mwana wa kweli wa Afrika ambaye leo tunafurahia kuzaliwa kwake,
Mcha Mungu,John Pombe Magufuli haukacha kulitaja jina la Mungu,kuomba neema na baraka zake kila alipoamka na kila alipofanya ziara zake za ufunguzi wa miradi kila leo,sifa na utukufu wa madaraka alimrudishia Mungu,tunafurahia kuzaliwa kwako John Pombe Magufuli,sifa kwa taifa zima-Tanzania, na utukufu kwa Mungu aliyekuchagua na kukuleta duniani tarehe hii ya leo,
Kwa muda mfupi maisha ya Daktari John Pombe Magufuli yalikuwa ya msaada mkubwa kwa Watanzania kwani alionyesha uwezo mkubwa wa kupambana na maadui zetu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini,Pia ulionyesha mapenzi ya dhati ya kusimama upande wa Watanzania wanyonge yaani wakulima, wafanyakazi, wavuvi na wafugaji kote nchini. Watanzania wanyonge hawana la kukulipa zaidi ya kukutakia Mwenyezi Mungu akupe heri uko uliko,utusamehe kama tulikulipa baya kwa wema,utuombee baraka na Mungu aibariki Tanzania na viongozi wetu,Amina.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
Yani vichaa hamuwezi kuisha Tanzania, mtu aliyepo kuzimu tena motoni anaweza vipi kukuombea?Happy birthday Dr John Joseph Pombe Magufuli. !
Huko mbinguni ulipo unaendelea kufanya kazi ya kuliombea Taifa Kwa Mungu ukishirikiana na Baba wa Taifa.
Hayo ya kuzimu unayajua wewe. Mimi najua Dr Magufuli na Baba wa Taifa wapo Mbinguni.Yani vichaa hamuwezi kuishi Tanzania, mtu aliyepo kuzimu tena moyoni anaweza vipi kukuombea?
Hakuna mbingu wala pepo kwa wauwaji, wauwaji wote makazi yao ni Jehenamu.
Usimfungamanishe muuwaji na Baba wa Taifa, Baba wa Taifa hata Wakatoliki wenzanke wana mchakato atangazwe mwenye Heri baadaye awe Mtakatifu, usimfananishe na huyo muhuni wenu.Hayo ya kuzimu unayajua wewe. Mimi najua Dr Magufuli na Baba wa Taifa wapo Mbinguni.
Ndio maana nakupendaa...Mungu aendelee kumlaza pema Magufuli. Amina
🥲🥲Tunakukumbuka sana JPM.
🙏🙏 Nakupenda pia brother AnthemNdio maana nakupendaa...
I miss JPM 🥲
Nikimtazama huwa naumia sana nakumbuka mengi sana pia.. Aendelee kupumzika kwa amani🙏🙏 Nakupenda pia brother Anthem
Huyu Rais alikua wa kitofauti sana yeye aliitoa roho yake kwa ajili ya watu.Nikimtazama huwa naumia sana nakumbuka mengi sana pia.. Aendelee kupumzika kwa amaniView attachment 2401168
Hii nchi mafisi mengi. Kuja kupata mtu kama huyu itachukua miaka mingi sana,Huyu Rais alikua wa kitofauti sana yeye aliitoa roho yake kwa ajili ya watu.
Kitu nilichojifunza Brother National adui wa mtu ni wa karibu sana anangoja uanguke akuonyeshe yeye ni nani na anasimama upande upi.
HakikaHii nchi mafisi mengi. Kuja kupata mtu kama huyu itachukua miaka mingi sana,
Sponsor kafa machawa mmebaki mnaweweseka tu.Tunakukumbuka sana JPM.