Sisi tunaangalia mazuri ya mtu akiwa hai, akiwa madarakani, that's how we should roll. Lakini mkuu tulitaka dikteta, refer speeches za Mnyika na Dr. Mihogo.
Huwezi kuangalia mazuri ya mtu wakati yupo madarakani kwa sababu kuna mengi yanakuwa yamejificha na hayaonekani kwa sababu atakuwa anayafunika!
Mfano mzuri kabisa ni Serikali yaMkapa... RIP Mkapa lakini alifikia kujiita Mr. Clean, na watu wakaamini ni Mr. Clean!!
Ile kuja kutoka madarakani sasa... salale!!!
Tukakuta:-1
1. Kaanzisha AnnBen Company wakati yupo Ikulu
2. Kajiuzia mgodi wa Kiwira,
3. Pesa za EPA,
4. Kagoda
5. Mereremeta,
6. Deep Green
Hayo ni machache tu ya hovyo na kuchefua ambayo yalifanyika under Mkapa Administration lakini hayakufahamika kwa sababu pamoja na Mkapa kujinadi alikuwa ni mtu wa Uwazi na Ukweli lakini serikali yake haikuwa ya uwazi kihivyo!!!
Tukija hoja ya dictatorship, mimi ni mmoja wa watu ambae niliandika zaidi ya mara 3 kuhusu hilo! Lakini binafsi sikutak Rais Dikteta bali nilitaka Dictatorship Constitution itakayowanyoosha watu!
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Dictatorship President na Dictatorship President!
Naamini hata hao waliokuwa wanasema wanataka Rais Dikteta walikuwa wanashindwa tu kutofautisha kati ya Rais Dikteta na Katiba ya Kidikteta kwa sababu hakuna mtu in a right mind anaweza kutaka Rais Dikteta wakati Katiba inahubiri Rules of Law!!
Lakini unapokuwa na dictatorship constitution tayari a dictatorship elements inakuwa a part of the law of laws... na muhimu zaidi, inakuwa ni mambo ambayo watu wamekubaliana how to handle different things sio haya ya Magu ya kufanya maamuzi kutegemea na ameamkaje!!!