Happy birthday Jay Z. Mc mkali kuwahi kutokea tangu dunia iwepo

Mc mkali kuliko wote hata ukimuuliza jigga mwenyewe ni Notorious BIG. Basi. Naona unamfagilia sana huyu mwabudu shetani

Ngoja nikupe sifa baadhi za Jay Z alafu umpime na ma Mc wote waliowahi tokea dunia hii

1. Uwezo wa kurap

Jigga anauwezo wa kipekee wa kurap anapiga style ata laki sita za kuchana ndio ,aana wanamwita king of all flows...anaweza kuchana taratibu au fasta fasta..anaweza kuchana huku anakusafirisha kwenye kitu kingine yani anachana mpaka un aona kitu mtu anachomaanisha kama ni gari basi utaliona gari linatembea ata kama huko gheto umelala...ameweza kupiga michano ya miaka hiyo mpaka watoto wa sasa anawakimbiza. Usisahau kufreestyle jamaa ni konyo.

2 uwezo wa kuandika

Jigga kwanza ni storyteller mzuri sana pia anaweza kuandika kuhusu topic yoyote bata, mademu, hustle, street na kila kitu.
3. Kukaa kwenye game

Jigga amekaa kwenye game kwenye generation tofauti tofauti na zote kakimbiza, wazee wenzie wameishiwa pumzi ila yeye ni kama ndio anaanza.

4. Kuweka history

Jigga ana records nyingi sana ameweka kuanzia ku-sell out madson square...kuanzisha vitu vingi alafu wengine wanafata

yani ni mengi mengi mengi
 
Everybody's like,"He's no item! Please don't like him.He don't wife 'em, he one nights 'em!" .... hahagh alafu kuna watu wanasema kwa vigezo gani!.. huyu jamaa anajua jamani tuache utani.
Story za vijiweni tu Chief. Wengi wamesikia Critics wakisema, wakadandia bila kufanya analysis zao wenyewe.

Wakafanye homework zao, waje watuambie. Halafu sis tutawaambia Kwanini Jigga man is tighter than any other Rapper who's not Tupac, and probably Em.
 
haya jigga happy birthday, ila ukisema ni mc bingwa kupata kutokea duniani watu hiphop watakubishia, wao wanawatajaga sana wakina Tupac na Nas, wakati wazungu wanamtajaga Eminem

hivi eminem si albino yule au???western albino ni mzungu
 
William Michael Griffin Jr. Is the Greatest EMCEE of all Time.
 

Jibu Ni Lassane Parish Crooks.. Unamjua!?

Kabla huja-google Ni Tupac "Makavelli".
 

Kuna ukweli Fulani hapa..:thumbup:
 

Inahitaji uijue Hip-Hop kwa kina kabla hujaanza kuichambua, and kitu muhimu katika Kuichambua Hip-Hop, biased opinions huwa hazihitajiki, coz Hip-Hop imebeba Emcees wengi wenye upekee wao tofauti, ndo maana yakupasa kuifatilia na kuisikiliza kwa makini Hip-Hop kabla hujaanza kuichambua,

Hip-Hop ni kama Soccer, ina mashabiki pia, na kila shabiki ana Emcee/rapper wake anaemkubali zaid, lakin utofauti wa Soccer na Hip-Hop, unakuja katika Misingi na utimilifu wa Emcees wanaoibeba Hip-Hop, ndo maana katika Hip-Hop ukileta Biased opinions na "mahaba" unajikuta upo nje ya box kabisa..

1. Umesema Jay Z ni "king of all flows" haya ni mahaba makubwa, kwanza kabisa katika Flows kuna Em na Biggie, sidhan katika ulimwengu wa Hip-Hop, utatengeneza Top 2 ya "King of all flows" hawa watu wawili usiwaweke, Then kuna kina Tech N9Ne (kama umemweka Jigga kama king of all flows, i doubt kama umeshawah kupoteza muda wako kumfatilia na kumsikiliza huyu mtu), and what about Big L (why mnamu-Underrate?)

2. umesema Jigga ni Konyo kwenye Free-style, well "he's not that Konyo".. kuna Big L (R.I.P), Biggie (R.I.P), Em, and most of all my nig' Lil snupe (R.I.P)..hii nyanja manguli kibao wanatulia kwa hao watu, wakina Rakim, Nas, Kool G rap, Master Ace Krs-One, 2pac, Cube, Jay Z, Canibus etc..

Then siku ukitulia mtafute na msikilize Kdot kwenye huu upande wa free-style..

3. kwenye uandishi, katika misingi ya Hip-Hop, interms of repn Culture ya watu weusi, pamoja na lyrical movements zinazoakisi Struggles, streets, projects, Ghetos, Politics, peace, inhuman activities (eg. racism, child abuse, etc), no one can beat Nas, Rakim, 2pac, (ImmortalTech) and Even Andre 3000, na pia nenda katulie msikilize Em na Jay Z na utakuja kunambia nan ni muandishi mzuri, Em ni Rapper timilifu zaid ya Jay Z.

Jay Z anaweza akawa amewapita headz wenzake kwa pesa na mauzo ya albums, but hiyo haivunji utaratibu wa kurate clinical rappers katika game, the fact kwamba Drake anauza zaid kwa sasa, haimfanyi kuwa better rapper than Kendrick and J.Cole..

Jay Z ni rapper mzuri, haipingiki kuwa Hawezi kukosekana katika List yoyote ile ya Rappers bora kuwah kufanya Rap Music, but he's not the greatest Emcee of all time, kama utazingatia uhitaji zaid wa Hip-Hop,
 

Who deceive it broh!
 
Hiphop ni nini? Ni kufokafoka kwenye beat?je Kila anaefokafoka kwenye beat anafanya hiphop?whack ni nani? Ili Uitwe emcee unatakiwa kufanya gemu kivipi? Je kufuata misingi na nguzo zote ndio u emcee? Je Ukifuata nusu ya misingi au nguzo bado utaitwa emcee? Mafanikio ya msanii ndiyo kipimo cha uwezo wake? Kama hapana apimwe kwa kutumia nini?



Haya maswali huwa yananifanya nishindwe kusema msanii fulani ni zaidi ya wengine.
 

Na Nasir Jones Bin Oludara
 

Kasome kitabu cha *The Art of Emceeing" cha Stic.man (Dead prez). utapata majibu yako yote bro.

kipo tu mtandaoni, you can read it.
 

Taja msingi wa Hip-hop ambao Jay-Z hawakilishi.


What's flows, to you?


Rakim? Tupac? KRS One? Cube? Nas? Wakali wa freestyle? I get a feeling unataja majina ili kumtisha jamaa, but you clearly have no idea.

Big L na Jigga kuna freestyle wako pamoja early 90s, niliwahi kuiweka jukwaa la "Entertainment" kama unaweza kuipata. Nimeshindwa kui-upload hapa, ila yeyote anaweza kuingia Youtube akaitafuta (Big L and Jay Z). Msisahau kuleta feedback please.

Masta Ace? Tafuta diss track yake inaitwa "aknowledge". Ameachia feelings zake humo baada ya kuvurugwa na jamaa wa kawaida tu kwenye freestyle (Boogey-man). Ka-panick mpaka aibu, anaongea vitu vya ajabu tu. If it's trouble much, I can analyze that track for you.


Mtoe Tupac. Nobody, and I mean nobody ever talked about struggles, ukombozi, n.k. kati ya hao uliowataja better than Jay. Chagua yeyote uliyemtaja kati ya hao, halafu tuchambue mistari yao kwenye field yoyote uliyotaja hapo.

Andre 3000 got more cred than Jay?? Hahaha, usiamini kila unachosoma google.

Jay-Z sio greatest rapper, true. Ila uhitaji zaidi wa Hip-hop ndio upi?
 

Unajua masta.. Tupac, Big L, Biggie Smalls.. Kwa kuwataja hao na uchambuzi wako inaonyesha how good you're.. Amani sana kusoma nondo kama hizi.:thumbup:
 
Rakim, ni Emcee bora zaid kuwah kufanya Hip-Hop Music.

Somehow I agree.. But still to me Uncle Pac leads then comes B.I.G (though I like Rakim More) and on 3rd there is Rakim.
 

... Naweza jibia hii tu masta, kwa freestyle Nas na KRS1 wanastahili kuwepo hapa tena sana.

For me.. Jigga=Buckshot on Freestyle.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…