Happy Birthday: Jiunganishe na mtu ambaye amezaliwa mwezi mmoja, siku moja na wewe

Happy Birthday: Jiunganishe na mtu ambaye amezaliwa mwezi mmoja, siku moja na wewe

Yes kuna nyota haziendani kimahusiano. Na kuna zinazoendana, tafuta kwa kweli hutojuta. Kama unataka mapenzi ya kweli, kupendwa mpk uchanganyikiwe basi Gemini ndiyo jibu [emoji847][emoji847][emoji847]
Haha basi sawa, ngoja nianze kufuatilia kama nyota yangu inaendana na Gemini, ili nianze kazi ya kumsaka mtoto wa mama mkwe mwenye nyota yake [emoji2][emoji2]
 
Elimu ya nyota/Unajimu (Astrology) ni elimu kama zilivyo elimu nyingine japo wapo wanaoihusianisha na imani za giza lakini fikra hio ... ni potofu [kwa fikra za mwandishi]. Unajimu ni uhusiano wa nyota na maisha ya binadamu. Hasa hasa [yanaangaliwa] mahusiano ya wakati wa kuzaliwa na sayari zilizopo katika mfumo wa Jua. Binadamu wote tumeumbwa katika mojawapo ya makundi 12 ya nyota (Zodiac signs). Kila kundi katika makundi nyota 12 lina tabia tofauti, mtizamo tofauti, nguvu na haiba zinatofautiana. Ili uishi vizuri na watu inatakiwa utambue utofauti na uheshimu hilo kwa maana hatuwezi kufanana. Ukiachana na issue za makuzi, mazingira na malezi, issue ya nyota katika maisha ya mtu inaplay part kubwa katika haiba, mitazamo pamoja na tabia ya mtu. MAKUNDI NYOTA Makundi nyota kama tulivyoona awali kuwa yapo 12 na yamepangwa katika mtiririko kuanzia nyota ya kwanza hadi ya mwisho. 1) Aries (Punda) - 21 March hadi 19 April (in between hizo tarehe) 2) Taurus (Ng'ombe) - 20 April hadi 20 May 3) Gemini (Mapacha) - 21 May hadi 20 June 4) Cancer (Kaa) - 21 June hadi 22 July 5) Leo (Simba) - 23 July hadi 22 August 6) Virgo (Mashuke) - 23 August hadi 22 September 7) Libra (Mizani) - 23 September hadi 22 October 8) Scorpio (Ng'e) - 23 October hadi 21 November 9) Sagittarius (Mshale) - 22 November hadi 21 December 10) Capricon (Mbuzi) - 22 December hadi 19 January 11) Aquarius (Ndoo) - 20 January hadi 18 February 12) Pisces (Samaki) - 19 February hadi 20 March CHAGUO SAHIHI Ukitaka kuanzisha mahusiano na kujihakikishia mahusiano ya muda mrefu na yenye kudumu basi chagua mojawapo ya partner katika makundi yafuatayo, i) Kama wewe ni Aries basi chagua: Leo, Sagittarius, Libra, Gemini au Aquarius ii) Taurus: Virgo, Capricon, Cancer, Scorpio au Pisces iii) Gemini: Aries, Leo, Libra, Sagittarius au Aquarius iv) Cancer: Pisces, Scorpio, Virgo, Taurus au Capricon v) Leo: Aries, Sagittarius, Libra, Gemini au Aquarius vi) Virgo: Taurus, Capricon, Cancer, Pisces au Scorpio vii) Libra: Gemini, Aquarius, Leo, Sagittarius au Aries viii) Scorpio: Pisces, Cancer, Virgo, Taurus au Capricon ix) Sagittarius: Leo, Aries, Gemini, Aquarius au Libra x) Capricon: Virgo, Taurus, Cancer, Scorpio au Pisces xi) Aquarius: Aries, Leo, Gemini, Sagittarius au Libra xii) Pisces: Cancer, Scorpio, Virgo, Taurus au Capricon Tofauti na machaguo haya, mahusiano yako yatakua na short term pleasure lakini in long term hayatokua na maisha marefu.
 
 
Back
Top Bottom