Happy birthday Mtume na nabii wa mwisho wa Soka Saint Gaucho

Siku ukiamua kujifunza utaelewa ni namna gani maneno "nabii " au "god " yanaweza kutumika nje ya muktadha wa dini.
 
Naomba mafanikio yake ndani ya PSG, Barcelona, na AC MILAN kwa miaka aliotumikia. Halafu compare na fundi Lapulga kwa miaka aliotumikia FC BARCELONA
Mafanikio makubwa kabisa ni World Cup, huyu Messi kachukua mara ngapi?
 
Mwanzoni nilidhani una hoja nzuri kumbe ni ujinga mtupu, eti timu ya taifa ni uchezaji wa timu nzima ila club ni suala la mchezeji mmoja mmoja.
 
Yote kwa yote Dinho Magic alibeba tuzo ya mwanasoka bora wa Dunia kipindi kile wachezaji timamu wapo weengi mno ila hawa ushuzi wao wapo wawili tu.
Enzi za Dinho tuzo walipokezana mastaa, sio kama kina Messi na Ronaldo.

Dinho alikuwa ni hatari sana!
 
Happy birthday to the greatest magician of all times

Kwa wale tuliobahatika kumuona katika ubora wake 2003 hadi 2007 tuna bahati sana, tutawasimulia wajukuu zetu hajawahi kutokea mchawi wa soka kama huyu.
 
Heri ya siku ya kuzaliwa kwa nabii wa mwisho kwenye soka...Dinho Gaucho
 
Miaka 43 sasa
 
Gaucho mchumba kwa Zidane, hata Wabrazili wenyewe wanakiri. Ni taarifa tu
Zidane hamfikii Gaucho, acha uongo wako.

Sema Gaucho kacheza kipindi kifupi, na hajawa na mafanikio baada ya kutandika daluga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…