Happy Birthday to me

Happy Birthday to me

Huyu bwege anapenda kujijazia misifa [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Pamoja na yote hayo hadi Kunichukia Kwako ila 24/7 uwapo JamiiForums ni lazima tu utamsoma, utachangia na hata Kusoma tena kwa Utuo kabisa Mada zake.

Nikiwa nawadharau hapa huwa Sikosei.
 
Asante Mwenyezi Mungu, Asante Wazazi wangu, Asante Walimu, Wakufunzi na Wahadhiri wangu, Asante wale Wote mlionilea na Kunijenga Kimaadili na Kinidhamu, Asante wote ambao mlikuwa na mnaendelea kuwa Wema Kwangu kwa hali na mali, Asante Ndugu, Jamaa na Marafiki pamoja na wale Maadui zangu tukuka ndani na nje ya JamiiForums.

27th March ni Siku Muhimu Kwangu.
Happy birthday DOMOKAYA
 
Happy birthday DOMOKAYA
Domokaya happy bethdei banaaaaaaa

Pokea tu

Wewe ndiye lopolopo la JF AISEE

Mola akujaze domo refu zaidi na kifua kisicho na pumzi ili ushindwe kutunza siri

Allah akupe bahati zote zihusianazo na ulopolopo wa domo lako

Ameen
 
Heri ya kuzaliwa ndugu yangu na Mkuu mwandamizi hapa jukwaani.

Nakumbuka katika nyakati kadhaa tumewahi kupopoana na kuparurana hapa ndani kwa maneno makali na mazito katika pita pita zetu kwenye hoja mbali mbali humu jukwaani. Nilikuwa sijawahi kula Ban ila Ban yangu ya kwanza humu ndani ilisababishwa na wewe baada ya kupopoana maji yakazidi unga ukakimbilia kwa moderators. Nilistaajabu sana mtu kutoka kanda maalumu kutupa taulo ulingoni kirahisi hivyo.

Ilifikia kipindi nikakuandikia hadi barua ya wazi ili kukukumbusha na kukurudisha kwenye njia maana niliona nina wajibu wa kukurudisha kwenye msitari mara zote ninapohisi umepotoka.

Leo naomba nikutakie heri na baraka tele katika siku yako hii ya leo. Sahau yote yaliyopita na tugange yajayo. Sikufichi mimi ni shabiki yako mkubwa sana licha ya kupopoana mara kwa mara na kitu pekee napenda kutoka kwaku ni ukweli na kutokumung'unya maneno.

Happy birtday again Game changer. Siku ya leo pia uitumie kufikiria uhusiano wako na Mungu na mchango wako kwa jamii. Zaidi ya yote nikutakie kwaresma njema.

Cheers
 
Back
Top Bottom