Harakati na kelele za mitandaoni haziwasaidii CHADEMA, zinawaingiza mkenge kila siku ila hawajifunzi

Harakati na kelele za mitandaoni haziwasaidii CHADEMA, zinawaingiza mkenge kila siku ila hawajifunzi

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Naona mnajidanganya kuwa kelele zenu mitandaoni zinawasidia kusikika na kuonekana mnazo hoja kiasi cha kuanza kujipiga kifua.

Ninyi bado hamjapata sapoti kupitia mitandao mnajidanganya kama watoto wadogo.

Uhalisia wa mnachodhania kuwa mnasapoti kubwa kutoka kwa wananchi kupitia mitandao ni tofauti na hali ilivyo mitaani.

Kama kweli mngelikuwa na sapoti kubwa field na basi wananchi wangeandamana na kuunga mkono juhudi zenu kudai katiba mpya.

Chadema tatizo lenu hamna tofauti na raia wa Ukraine wanaopigana vita kupitia mtandao wa Twita huku field hali ni ngumu. Kuweni na busara za zaidi.
 
Naona mnajidanganya kuwa kelele zenu mitandaoni zinawasidia kusikika na kuonekana mnazo hoja kiasi cha kuanza kujipiga kifua.
...
Mkuu usiwasikilize wana ccm waliopo ngazi ya uwaziri, ubunge na ukatibu mkuu wa wizara au wakurugenzi wa mashirika ya uma

Wanahubiri shule za kata nzuri huku watoto wao wakisoma marekani na ulaya

Wanahubiri kiswahili ni lugha nzuri huku watoto wao wakisoma International school zenye mitaala ya uingereza kama International school of Tanganyika, Ada kwa mwaka ni zaidi ya Milioni ishirini

Kamwe usiamini Propaganda za wakubwa wa ccm

Maofisini kwa sasa watoto wao ndio wanaajirika kwa uwezo wa kuongea vizuri kwenye interview

Hao watoto wenu wa the.... the... of course, Yo know......OK no problem hakuna anayewataka na degree zao

Leo hii maofisini watoto waliosoma shule za kisasa kazi zipo kibao, Hao wenu hawajui lugha
 
Naona mnajidanganya kuwa kelele zenu mitandaoni zinawasidia kusikika na kuonekana mnazo hoja kiasi cha kuanza kujipiga kifua...
Sasa wewe huku mitandaoni unafanya nini kama siyo hicho hicho wanachokifanya wengine.

Kuna vijana wako field wanaelimisha wananchi kuhusu katiba..... Maza kaamua kuwatuma akina Zitto na Mkandara kuchelewesha.

Sidhani kama atafanikiwa.
 
Naona mnajidanganya kuwa kelele zenu mitandaoni zinawasidia kusikika na kuonekana mnazo hoja kiasi cha kuanza kujipiga kifua...
Bwana Idugunde,Hukumu ya Kesi iliyoisha juzi ya Jenerali Sabaya inakaribia,hawa ndio walikuwa na akili kama zako lakini leo wapo Jela Kisongo,nakukumbusha tu kwamba What Goes Around Comes Around,

IMG-20220319-WA0021.jpg
 
Bwana Idugunde,Hukumu ya Kesi iliyoisha juzi ya Jenerali Sabaya inakaribia,hawa ndio walikuwa na akili kama zako lakini leo wapo Jela Kisongo,nakukumbusha tu kwamba What Goes Around Comes Around,mjifunze kutumia akili za kichwani badala ya akili za makalioniView attachment 2160004
Nje ya mada dada
 
Naona mnajidanganya kuwa kelele zenu mitandaoni zinawasidia kusikika na kuonekana mnazo hoja kiasi cha kuanza kujipiga kifua.

Ninyi bado hamjapata sapoti kupitia mitandao mnajidanganya kama watoto wadogo.

Uhalisia wa mnachodhania kuwa mnasapoti kubwa kutoka kwa wananchi kupitia mitandao ni tofauti na hali ilivyo mitaani.

Kama kweli mngelikuwa na sapoti kubwa field na basi wananchi wangeandamana na kuunga mkono juhudi zenu kudai katiba mpya.

Chadema tatizo lenu hamna tofauti na raia wa Ukraine wanaopigana vita kupitia mtandao wa Twita huku field hali ni ngumu. Kuweni na busara za zaidi.
Ushindwe na ulegee kama huoni matunda yake basi wewe ni kipofu au ulizaliwa kuanzia 1994 mpaka 2006 kwa hiyo kujua umuhimu wa Katiba mpya kwako itakuwa ni shida kwa sababu haujui faida yake au hasara yake.
 
Zingekua hazisaidii dikteta asingesema anatamani malaika washuke na kuzima mtandao.

Pia asingeifungia twitter hadi anakufa.

Asingezima mtandao siku 6 kwenye uchafuzi mkuu.

Huo ushamba wenu wa kudharau nguvu ya mtandao ndio ulifanya akafanya uchafuzi mkuu kuwahi tokea baada ya influence yake kushuka kwa kiasi kikubwa baada ya kupewa brief na vijana wake mwezi August.
 
Hawa watu ni wa ajabu SANA wanahujumu uchaguzi halafu wanasingizia field,ccm bwana vichwa vigumu.
 
Back
Top Bottom