Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Msalimie Mange KimambiHapo ni kama umnasemea chooni. Kama mnge kuwa na hoja msingezima bunge live, msingetunga sheria ya mtandao, msingepiga marufuku mikutano ya siasa, msingeleta sheria ya statics, msingeteua wanasiasa kwenye nafasi za utendaji zisizo husu siasa, msingeleta sheria za habari mlizoleta, msingemsaidia kwa kutumia polisi lipumba. Kifupi hamna hoja wala hamna hoja. Kam mnasema hao wapinzani wanatumia hotuba za mkuu kupata cha kusema si mrekebishe utaratibu wa anasema nini? badala ya kuacha aseme na nyinyi mpate kazi ya kufafanua au kuteteta hum JF. Wakati mwingine nachefuka kusikia watu wa namna hii wamesoma.
Mimi nikisikia ving'ora huwa napaki pembeni apite amirijeshi mkuu, kura yangu sijui hata kama ilimfikia LUBUVA.
Mwanzoni mwa mwaka huu, niliweka taarifa kwenye mitandao ya kijamii hususan hapa Jamiiforums juu ya Mkuu wa Sera na Utafiti CHADEMA, Ben Saanane kununuliwa vitendea kazi kama simu, kompyuta mpakato, ipad, tablets na zana nyingine. Nilieleza kuwa aliyemnunulia vitu hivyo ni Edward Lowasa. Nilitoa sababu za Lowasa kufanya hivyo ni kutaka Mkuu huyo wa Sera na Utafiti afanye kazi ya kumsafisha Lowasa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia amshambulie Rais Magufuli ili tunapoingia 2020, asiaminike tena. Nilieleza kuwa Ben na Lowasa wamekubaliana kuwa malipo ya kazi hiyo ni milioni 4 kwa mwezi.
Kwenye uzi ule, nilieleza bayana kuwa Ben Saanane amepangiwa ofisi ya kufanyia kazi hiyo katika sehemu ambapo sikubainisha kwenye mtandao kutokana na sababu za kimkakati.
Hata hivyo, baada ya uzi ule kuwekwa, Ben Saanane alikosa uvumilivu. Aliishia kuporomosha lugha zilizokosa staha kwa lengo la kushinikiza mods waufute. Alifanikiwa. Uzi ule ukaenda na maji. Leo mdogo wangu Ben namuomba awe mvumilivu ili tujadili kwa staha.
Miezi 5 imepita sasa tangu Ben Saanane anunuliwe. Matunda ya uwekezaji ule yameanza kuonekana. Ben Saanane na genge lake wameanza mashambulizi dhidi ya Rais kwa hoja ambazo kimsingi hazina mashiko.
Ben Saanane na genge lake wameshindwa kabisa kuona udhaifu wa Rais Magufuli kiutendaji na badala yake wanaegemea kwenye mipasho na mapambio. Wanafanya siasa za kuvizia. Niliwahi kuanzisha mada humu kwamba, ikitokea Rais akawa bubu, je CHADEMA watakuwa na ajenda zipi?
Tathmini yangu ya muda mfupi imebaini kwamba, hoja zinazojengwa na Ben Saanane na genge lake zinategemea nini Rais anaongea. Kwa maana utendaji wa Rais uliotukuka unasababisha Ben Saanane na Genge lake wakose hoja za kumkosoa. Hata kama wanapojaribu kukosoa utendaji, wanakosoa kwa hoja dhaifu. Mathalan, ziliponunuliwa ndege mpya mbili aina ya Bombadier Q400, walijenga hoja za kitoto eti ndege hizo hazina mwendo. Mara wanasema ni mapangaboi. Mara wanasema eti water salute haikufanyika kisawasawa. Almradi wanawaonesha wafadhili wao kuwa wametimiza wajibu wao. Utoto.
Uwezo wa vijana wa CHADEMA katika kujenga hoja ni mdogo. Kuna wakati Lusinde aliwahi kuwaambia kuwa akili zao zimeshikiliwa na Mbowe na ndio maana wanawaza kimbowembowe tu.
Hata hivyo, najaribu kuwaza, je kazi anayofanya Ben Saanane na genge lake inatosheleza matakwa ya wafadhili wake? Je watafanikiwa kushusha morali ya Rais Magufuli katika kuwatumikia wananchi? Je watakwamisha juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Magufuli katika kutekeleza ilani ya CCM? Thubutu! Rais ameapa kuwa hakuna atakayekwamisha utekelezaji wa Ilani ya CCM. Ben Saanane na Genge lake wataishia kujadili water salute, kuomba Salary Slip ya Rais na kujipongeza kutokana na kauli ya Rais kuwa anatamani malaika afungie mitandao ya kijamii kwa mwaka mmoja ili itakapofunguliwa wakute Tanzania imepaa.
Nimhakikishie Rais wangu kuwa, hawa wapiga kelele mitandaoni hawatafanikiwa kukwamisha harakati zako za kuwaletea maendeleo wananchi. Waache wapige kelele. Wewe piga kazi. Mwisho wa siku kelele zao zitageuka kuwa kicheko kwako. Watanzania tuna imani kubwa kwako. Kazi unayofanya inapokelewa kwa mikono miwili na Watanzania. Utafiti wa Twaweza unabainisha kuwa 96% ya Watanzania wanakulibali. Endelea kupiga kazi ili ifikapo 2020, wapinzani waone aibu kumsimamisha mgombea Urais kupambana na wewe.
Hawana jipya Babicha.Bavicha ni watu waliochanganyikiwa,na wala hawatafanikiwa kumtingisha Rais wetu
Wewe Ni Kama Nepi AKA Waziri Rumbesa, aliyesema Kuwa Lowassa Kanunua Chadema, Unajua Tunakamataje Waongo, they pretend to have details ambazo kikawaida Haiwezekani Kuwa Nazo. Nani sasa anaamini Kuwa Lowassa alinunua Lowassa kwa Mbowe Kama alivyokuwa Akisema huyu Mwehu kwenye Kampeni? Kama Una akili Mwambie Rais Nani aliwaua Wale Askari wanne Pale Bank na Yule Mwingine Vikindu, Maana wanasema Kikulacho Kinguoni Mwako!
see huwezi jua, Ni mfano wa waongo, wanafiki na wahalifu Kama WeweHizi video zinahusiana vipi na mada?
Kinachosikitisha ni kwamba hawana hoja yoyote ya maana wanayotoa zaidi ya kumuattack tu binafsi. Washindwe kwa jina la Mwenyezi MunguRais ni muacheni afanye yake huyo kijana apewe tu pesa lakn ninaiman kwa uwezo wa mungu Rais hawez kuchafuka hata kidogo....
Mkuu Kibosho, naunga mkono hoja kwa sababu jf was meant to be the home of great mind, ila kwa vile huu ni mtandao huru wa kijamii kila mtu yuko huru, matokeo yake ndio haya watu wenye sound mind wamejiunga na wanaleta hoja zenye mashiko kama Mkuu Ben Saanane ila pia watu wenye unsound mind pia wamo.Thread kama hizi ndizo zinazofanya Jf kuonekana ya Hovyo. Source ya habari yako? Ushahidi? Yan JF sasa imekuwa sehemu ya kushambulia watu binafsi bila ushahidi. Thread kama hii haina uwalali wa kukaa hapo kwa Heshima ya JF