mcTobby
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 7,894
- 22,679
Hii ni picha ya miaka ya 1970s. Unaowaona hapa kwa tafsiri ya haraka unaweza sema ni mabinti walio na furaha na tabasamu pamoja na amani mioyoni mwao. Picha hii ya pamoja ni ya waumini wakiwa pamoja na mchungaji au Nabii wao ,wakieneza injili ya neno la Mungu na kuhubiri UPENDO kwa watu wote.
Lakini nyuma ya tabasamu kwenye nyuso hizi unazoziona hapo kumejaa hadithi ya kutisha na yenye kusikitisha sana. Unawaona hapo wanajiita Children of God wakisambaza injili na kuhubiri upendo kwa watu wote. Hawa wakujiita Children of God( CoG) ilikuwa ni moja kati ya cult mbaya zaidi kuwahi kuundwa huko marekani ikitumia Jina la Mungu . Kivipi? Ngoja nikupe stori.
Children of God (CoG) ilikuwa ni dini ya aina yake ambayo tunaweza kuiita Cult iliyoundwa na jamaa mmoja aliyejulikana kama David Berg huko california marekani mwaka 1968.
Wakati inaanzishwa hili dhehebu au cult ,walengwa walikuwa ni watu wote ambao walikuwa wamepoteza tumaini katika jamii ,waliotengwa na familia zao n.k. yaani kiujumla ilikuwa inawalenga wale wote waliokuwa "Broke".
Ujumbe mkubwa aliokuwa akiutumia huyu Berg katika kujipatia wafuasi wa aina hii ulikuwa simple tu. "We are God family. A place of love and peace". Lakini baada ya huyu bwana kupata wafuasi wa kutosha ,ghafla mafundisho yake ya kidini yalibadilika.
Huyu bwana Berg kwanza alianza kujinasibu kwa kujiita Nabii wa siku za mwisho. "End times prophet"
Alianza kuandika machapisho na majarida mbalimbali yaliyojulikana kama "Mo letters " yanayofundisha kuhusu Ngono, siku ya mwisho ya hukumu na kuishi maisha makamlifu kwa mujibu wa akili zake zilivyomwelekeza.
Moja ya mafundisho yake yenye utata mkubwa yalikuwa yanajulikana kama FLIRTY FISHING.
Katika mafundisho ya huyu bwana kuhusu flirty fishing aliwataka waumini wake wasambaze "Upendo wa Mungu" kupitia ngono. Yaani kadiri wanavyofanya ngono na watu wengi wanasambaza upendo wa Mungu kwa watu.
Sasa hao waumini wake ambao wengi wao walikuwa wasichana wadogo kiumri walikuwa wakijiweka daraja la "high class Prostitutes" yaani machangudoa wenye viwango ambapo walikuwa wakiwatega watu mashuhuri na wenye hadhi kwenye jamii kama mabalozi, wafanyabiashara wakubwa, wanasiasa na pia wakati mwingine watu wa idara ya usalama wa taifa marekani.
Kwa mujibu wa mafundisho yao waliamini kulala na watu hao wenye hadhi ni njia mojawapo ya kusambaza upendo wa Mungu. Lakini nyuma ya pazia yote waliokuwa wakiyafanya walikuwa wakitumikishwa kingono pasipo ridhaa yao.
Matokeo yake ni kwamba watoto waliokuwa wanazaliwa kutokana na hizi harakati za "kulana" hovyo walikuwa hawajulikani status zao kwa maana baba na ubini wa mtoto haukujulikana.
Na la kutisha zaidi kama sio la kuhuzunisha ,hata watoto wadogo walikuwa wakiingizwa kwenye huu ushetani wa kutumiwa kingono kutokana na mafundisho yake.
Kwa mujibu wa biblia ya huyu david Berg iliyoitwa Mo letters alielezea kwamba hata watoto wadogo wana haki ya kuonja upendo wa Mungu kupitia Ngono.
Na kweli kwenye machapisho yake kulikuwa na maelezo na picha za pornografia zinazohusu watoto na jinsi wanavyopata upendo wa mungu kupitia kufanya mapenzi kwenye umri mdogo.
Kwa mfano aliwahi chapisha mafundisho yaliyokuwa yanachochea ngono ya watoto wadogo yenye kichwa kinachosema "The Devil hates Sex, Heaven's Girl and The story of Davidito".
Huyu davidito alikuwa ni mmoja wa watoto ambaye alimu adopt au kumuasili ili awe wake kutoka kwa mmoja wa waumini wake. Davidito kalikuwa katoto kadogo ambaye alifanywa kuwa "mtoto msafi na aliyetakaswa " wa kanisa hilo la child of God (CoG) kutokana na kupokea Upendo wa Mungu kupitia kufanyishwa ukatili wa kingono akiwa na umri wa miaka 2 na huyu Berg.
Matokeo ya haya mafundisho ni kwamba watoto walitenganishwa na wazazi wao na kukuzwa kivyao. Wengi wa hawa watoto walikuwa hawaendi shuleni, walilazimishwa kufanya kazi pasipo ridhaa yao na kutumikishwa kingono ili kusambaza upendo wa Mungu.
Mmoja wa wahanga wa hii dini au cult ya david berg alikuwa kijana maarufu ambaye alikuwa ni mtoto wa kufikia wa huyu Nabii berg.
Kutokana na madhila na manyanyaso ya kingono aliyoyapitia akiwa mdogo ilimfanya kushindwa kuishi maisha ya kawaida kama watu wengine(post traumatic stress disorder PTSD) akaamua kujiua mwaka 2005. Huyu Rodriguez alijua baada ya kumuua mmoja wa kiongozi wa hii cult ya CoG mwanamama angela smith ambaye alikuwa akimnyanyasa kingono akiwa mdogo. Alieleza sababu zote hizi kwa kurekodi mkanda wa video na kuacha kama ujumbe kabla ya kujiua.
Pia mwigizaji maarufu Joaquin phoenix aliyecheza filamu ya JOKER alikulia kwenye hii cult ya CoG. Na alikiri madhila yaliyomkumba akiwa humu kwenye hii cult kwa kufanyiwa unyanyasaji wa kingono akiwa mdogo.
Ilipofika miaka ya 90 shinikizo kutoka serikalini na pia kwenye jamii ya wa marekani iliongezeka baada ya watu waliokuwa humo wakitoka hadharani wakielezea madhila na manyanyaso yaliyokuwa yakiendelea humo kwenye dini ya CoG.
Kuona hivi hili dhehebu la CoG likaamua kubadilisha baadhi ya mafundisho yake. Baada ya david berg kufariki mwaka 1994, CoG ilibadilishwa jina na kuwa The Family International na kujitetea kwamba imebadilisha mwenendo wake wa tabia chafu.
Tokea mwanzoni wa miaka ya 2000 wanachama wa zamani wa hii cult walijitokeza hadharani waziwazi kukiri kuhusu unyama waliokuwa wakifanyiwa wakiwa ndani ya cult hii hatari ya CoG chini ya david berg. Wengi wao walihojiwa kwenye runinga, redio na pia hata machapisho mbalimbali yaliandikwa kuhusiana na hii cult ya CoG.
Cult hii bado ipo lakini imehamia kwenye ulimwengu wa kidigitali ikijiendesha huko ikitumia majina masafi na mazuri yasiyotiliwa mashaka kwenye mitandao ya kijamii.
Ndio maana kuna nukuu inasema "Cults don't die. They just adapt to the times".
NB:wijamaG, oswampasM, Oge vidavida et al hao wote ni cult leaders.
