kante mp2025
JF-Expert Member
- Nov 11, 2022
- 631
- 1,192
Mbele yenu ni kijana wa kitanzania mpambanaji ninayechukia kukata tamaa, Kwani kukata tamaa ndio mwanzo wa umaskini.
Leo nimeona nishare visa tunavyokumbana navyo wagonga ulimbo hasa graduates katika kutafuta ajira rasmi hasa sisi tuliotokea kwenye familia duni ambazo ikihitajika laki moja basi ukoo mzima lazima mjichange.
Basi bhana tokea nimalize chuo kichwani nilikuwa tayari nimejiandaa kisaikolojia kuhusu changamoto ya ajira kwani nilikuwa napenda sana kusikiliza visa na mikasa vya mabraza ambao tayari walinitangulia kumaliza jinsi walivyokuwa wanapambana walau kupata japo hata mchongo wa laki mbili na bado wanaikosa.
Hivyo basi wakati wenzangu hasa wale watoto wa Dady Me I Want To Party"" walipokuwa wakizimimina shampeni kwa fujoo siku ya mahafali ya chuo pale makao makuu, Mimi kiumbe wa Mungu nilikuwa kwenye msongo mkubwa wa mawazo maana sikuwa hata na ndugu ambae alikuja kwenye mahafali yangu nikajikuta najutia uamuzi wa kufanya sherehe ile.
Lakini niliazimia kufanya sherehe ya kuhitimu maana kitendo cha mimi kuhitimu ilikuwa ni muujiza mkuu ukizingatia ndio msomi pekee wa taaluma hiyo katika ukoo wangu, lakini pia mapito niliyopitia hadi kumaliza chuo yalinipa nguvu ya kuhisi ninapaswa nishiriki graduation maana hapo kati nilihairisha mwaka kwa kukosa ada, pili yale maisha ya kula ili niishi nikimaanisha ile kula mara moja kwa siku kama niko kwaresima yote hayo yalinipa sababu ya kushiriki sherehe ile ya mahafali chuoni.
Nikiwa katika dimbwi zito la mawazo ndipo nikawa nasikia wazazi wa watoto wa Dady me i want to party wakiwaahidi mambo makubwa makubwa vijana wanaomaliza pale, Niliwasikia baadhi wakiwaambia watoto wao kuwa nishaongea na yule mkurugenzi ukipata tu cheti chako kuna nafasi pale Mloganzila, wengine wakazitaja sehemu kubwa kubwa tu.
Hapo mimi mgonga ulimbo na joho langu nikawa na simanzi sana hasa nikiwa sina ramani yeyote ile ya kujua nitaelekea wapi, nikiyakumbuka mazingira ya kule kijijini kwetu ambako kupata network ya mtandao hadi upandishe vilima nikawa nayaona tu mashamba ya mahindi yakiningojea kwenda kuyakatua.
Lakini pia nikakumbuka wazazi na wanakijiji wananiona mimi kama kijana wa mfano, ukizingatia kule kijijini msomi anaheshimika vibaya mno na wanaamini elimu ndio ufunguo wa maisha.
Nikawaza nikiwa chini ya mti nimejiinamia je nirudi bush, Nikakumbuka hata nauli ya kunirudisha tu bush sina mfukoni nina elfu ishirini tu niliyopatiwa na mwalimu wangu kama zawadi ya kunipongeza kuhitimu, huku geto nikiwa na kiroba cha unga alioniagizia mama toka kijijini na kipeto cha viazi na gesi ipo nikasema hapa ni kukaza tu sina connection ila Mungu hutengeneza connection.
Basi wengine wakiwa wanaelekea kwenye kumbi za kisasa kusherekea sherehe yao ya kuhitimu na familia zao wengine wakiwa na misafara ya magari, Mimi kwa kutumia usafiri adhimu wa miguu nikaanza kujirudisha magetoni huku nikiwa na msongo mzito wa mawazo.
Nikiwa njiani wakati naelekea magetoni ghafla nikasimamishwa na chombo kimoja cha usafiri ambacho ndani yake kulikuwa na mtu anaenifahamu na anayewafahamu wazazi wangu kule kijijini, akaniuliza vipi hukuwaambia nduguzo kuwa uko na sherehe mbona upo mwenyew mwenyew nikabrush kuwa aah niliona nisiwasumbue, kwa kuwa yule ni mtu mzima akajiongeza na kunambia nawe ingia humu akaniunganisha kwenye sherehe ya ndugu yao mmoja aliekuwa anamaliza pale
Ambapo ilifanyika sehemu moja nzuri sana hivyo kiumbe wa Mungu nikapata kula vyuku na soda siku hiyo kwa hisani ya watu wema na si haba walinipa na zawadi japo kimoyo moyo nilikuwa najisikia vibaya maana kwa kila kinachotokea nikawa nasema huenda tungekuwa na mapesa kama watoto wa Dady Me i want to party basi nami ningepigwa kasherehe fulani hivi ka kitaita, Nawashukuru sana watu wale.
Ile sherehe ilipokwisha nikarudi kwenye zone yangu "Stress zone* nikiwa najirudisha kwenye kiota changu na si haba na zile zawadi za watu wale wema nikajikuta nina kama elfu sitini mfukoni.Kichwani nikawa na swali moja kubwa NAANZIA WAPI KUJITAFUTA BAADA YA KUHITIMU....
Fuatana nami kiumbe wa Mungu kwenye safari hii ya harakati za wagonga ulimbo💉