Endelea kusimulia bado upo kaunta km barmedi au sasa hivi umehamia kwenye idara ya ubaunsa na ulinzi au umekua dalali mtu wa kati mzee wa kutembeza mikasi almaarufu km winga teleza?
Tunaendelea wakati ule nikiwa waiter kwenye bar ile yenye utulivu mwingi na ilikuwa ni sehemu ambayo ni rahisi sana kuwaona hata viongozi wa chama na serikali wakija kupata moja baridi moja moto kulingana na mazingira yake ya utulivu,Naweza sema ilikuwa ni bar ya watu waliostaarabika.
Mgonga ulimbo kama kawaida yangu nilikuwa najitahidi sana kutoa huduma bora sana kwa wateja ikiwemo kuwachangamkia na kuwakaribisha kwa heshima na adabu kwa waliokulia kijijini wanaelewa vile huwa tunafundishwa vijana wa mikoa ya kusini wanaelewa hili
Mungu sio faru john basi wengine walikuwa wanakuachia tips kiumbe cha Mungu napata walau nauli na hela kidogo ya kuwatumia wazee kijijini lakini kwa wazoefu na bar hili wanalijua sana kwa mhudumu wa kiume tips huwa ndogo ukilinganisha na waitress maana iko wazi wanaume hatuna cha kuoffer kwa watoa tips hivo mtu akinipa hata jero nilikuwa nashukuru vibaya mno.
Siku zikasonga masaa yakasogea akilini mwangu nikawa nasema hapa ndio sehemu sasa ya kutengeneza connection maana watu wazito wengi wanakuja hivo nilikuw nahakikisha nikikupiga service yangu mpaka unafeel kuniuliza hivi umeishia form ngapi hapo ndipo nilikuwa nafunguka kuwa mimi ni graduate basi swali linalofuata ilikuwa lazima uulizwe kwani umesoma kozi gani.
Nilipokuwa nawatajia kozi yangu walikuwa wanashtuka like either wanahisi nimefeli au laa sipambani kutafuta michongo,Ila mimi ndio nilikuwa najua uhalisia wa ground ulivo na hiyo ni kawaida sana kwa waliojipata kuona wanaopambana na maisha kama hawapo serious hivi.
Basi bhana kama kawaida ya pombe ikishamkolea mtu maboss wengine ilikuwa wakilewa wanakupa mausia mengi na kukuahidi mambo makubwa hadi unahisi kesho utaamka upo ofisi fulani maana unakuta anakutajia maboss wakubwa wa mji anaofahamiana nao huku akikwambia kijana usijali mimi nitakusaidia😁Kiumbe wa Mungu nashikwa na imani kumbe pombe anyway ni maisha.
To be continued wakuuu wa wakuu...hii ni true story no fake detail, tunashare experience za maisha