Baraka Mina
JF-Expert Member
- Sep 3, 2020
- 593
- 611
View: https://www.youtube.com/live/Kl7JY-zdy0c?si=TWJ9NKMmXZrdQII6
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka Mlimani City jijini Dar Es Salaam ambapo leo tarehe 12 Agosti 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinafanya harambee ya kuchangia Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wawakilishi, Wabunge na Urais.
Mgeni Rasmi katika harambee hiyo ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. Harambee hii inalenga kukusanya shilingi bilioni 100 kwa ajili ya maandalizi ya kampeni, ikiwemo gharama za magari, mabango, mafuta, fulana na kanga.
Jinsi ya kuchangia harambee:
Viongozi mbalimbali wa CCM wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Bara Ndugu Steven Masatu Wassira wameshawasili ukumbini.
Azim Dewji amwambia akina mbiombio wasimsumbue, hawana lolote.
Uchangiaji
1. Dkt. Samia Suluhu Hassan - Milioni 100.
2. Wachimbaji wadogo wadogo - Bilioni 16.2; (pamoja na ahadi), bilioni 9 imeshawekwa kwenye akaunti ya CCM.
3. GSM - Bilioni 10 (Zimeshawekwa kwenye akaunti ya CCM).
4. Young Africans SportsClub (Yanga) - Milioni 100.
5. Turky Group - Milioni 600 (Milioni 300 zimeshawekwa kwenye akaunti ya CCM).
6. Tosh Cargo - Milioni 100.
7. Azim Dewji & Singida - Milioni 300.
8. CCM Dar Es Salaam Mkoa - Milioni 20.
9. Mwanamke Kijani - Milioni 200.
10. Afr Oil Group - Milioni 200.
11. Wadau wa Songwe - Milioni 162.
12. Wafanyabiashara wa Dodoma - Milioni 200.
13. Wafanyabishara Arusha- Milioni 455.
14. Kagera Wafanyabiashara - Milioni 100.
15. Iringa Wafanyabiashara
- Milioni 230.
16. Wafanyabiashara Njombe - Milioni 122.
17. Wafanyabiashara Singida - Milioni 600.
18. Wafanyabiashara Simiyu Milioni 600
19. Wakulima korosho Milioni 800
20. Bodaboda Shinyanga milioni 5
21. Maafisa usafirishaji bodaboda na bajaj Tanzania Milioni 12
22. Wateule wa mama Tanzania Milioni 30
23. Tarimba achangia Milioni 20
24. Boniface Mwamposa achangia Milioni 50
25. Warembo wote Tanzania ( Miss Tanzani) Milioni 10
26. Wasanii bongo movie Milioni 10
27. Mawaziri na Manaibu Mawaziri Tanzania Bara Milioni 365
28. Mawaziri 7 kutoka Zanzibar wamechanga Milioni 70
CCM yafanikisha kuchangisha Fedha kiasi cha Shilingi Billioni 86.31 kwa ajili ya kampeni za CCM za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025, katika Harambee inayoendelea Katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar Es Salaam.leo 12 Agosti 2025