Harmo Rapa atimua mbio baada ya Mh. Nape kuoneshwa bastola

Kumtishia mtu na bastola ni kosa kisheria, kwa nini huyu asichukuliwe hatua za sheria? hatari tupu
 
Teh teh teh alienda kufanya nini na yeye mzee wa matukio
 
Leo nimeshangaa kuona mtu wa usalama kuombwa kitamblisho na kutoa bastola.Kutokana na video inayozunguka kuhusu mwana usalama kumtolea bastola Nape baada ya kuombwa kitamblisho.

Je sikuhizi mtu akikutolea bastola tuelewe kuwa moja kwa moja ni wa TISS?

Hata mimi ninayo na mimi ni TISS?
 
Jaman nataka kujua huyo, nii nanii alie vaa suti nyekundu anasema Utaaribu.. Naomba Kujuzwaaa
 
Msameheni bure maana anaonekana bado ni mgeni kazini. Nape amemuomba kitambulisho yeye anatoa bastola, hawezi kuwa na akili timamu ya kikazi.

Wenzake huwa wanaficha kuwa nayo hadi pale watakapoona diplomasia imeshindikana na wapo katika hali ya hatari kwa maisha yao ndio hutoa ili kujihami.

Sasa ona alivyoaibika maana aliyemnyooshea bastola hata hajashtuka akaamua kuirudisha, aibu kwake na kwa aliyemtuma. Pia alihatarisha maisha yake, kairudisha silaha kiunoni na akaweka mazingira ya kusongwasongwa na watu je wangempora na kumdhuru?

Hilo ni tatizo la vijana kutofundishwa taratibu sahihi ya kazi zao.
 
Kilochoteka hapo na unprofessional kabisa... Hata kama umeagizwa kazi, kutumia akili za kuzaliwa ni mihimu sana pia...


Mpaka anaambiwa ataaharibu mambo sasa... lakini bado anapandisha jazba...


Ni hatari sana kwa kweli...
 
This is very sad. Matumizi ya mamlaka yasiyo ya lazima. Tatizo la hao Jamaa ni kuwa nguvu nyingi akili kidogo.
Nimeogopa sana. Tunakoenda sio kuzuri kabisa.
Kwa style ndio maana bashite alienda na platoon clouds.
 
huyo askari baada ya kujitambulisha ana toa pisto. au ndo mfumo mpya wa kuvamia watu sasa
 
Mie mwenyewe nimeshangaa!I expected them to be people from the same system lakini hawaonyeshi kuwa na team work.
Hili tukio limenistua sana,i keep on repeating again and again hii clip siamini nnachokiona.
Mpaka raia wanasogea na kuwatulizeni maafisa usalama,sasa nani aliye salama,wewe mwenye fani yako au yule raia mbumbumbu?Doh!
 
Kumtishia mtu na bastola ni kosa kisheria, kwa nini huyu asichukuliwe hatua za sheria? hatari tupu
Kwa bashite ambay alienda na platoon clouds kachukuliwa hatua gani.
Zoea tu hayo mambo, ndio maisha ya siku hizi yalivyo.
 
mkuu badala ya kumhurumia nape ,,
nimecheka hadi nimekaa chini.
hamorapa level zake za kiki si za nchii hii

Dah, kijamaa (Harmorapa) ni mtaalamu sana wa kutafuta kiki, ni mtaalam wa kujipenyeza kama Makonda alivyojipenyeza kwa Mzee Kamese, Mzee Sitta, Mzee Kikwete na sasa kwa Magu

Kweli alivyopotea ni balaa, naona alienda kuitupa Suruali kwa sababu ya kufuatwa na nzi
 
Kwa Kuangalia tu hii scenario unaweza gundua mafunzo yanatolewa kwa vijana wetu miaka hii ya karibu hayakidhi mahitaji kabisa!! Pale ilikuwa ni diplomasia tu inemaliza mambo sasa mtu nipe kitambulisho unanionyesha Bastola kwani nimekwambia nataka Bastola? Halafu wakati huo huo unaonekana kwenye macamera ya waandishi Wa habari! Kuanzia juu hadi chini hamna cha maana
 
Kwa bashite ambay alienda na platoon clouds kachukuliwa hatua gani.
Zoea tu hayo mambo, ndio maisha ya siku hizi yalivyo.
Nimeogopa sana mtu ambaye alikuwa waziri anafanyiwa hivyo tena mchana kweupe, je sisi akina yahe? hatari sana
 
Mungu atusamehe kwa makosa ya mwaka 2015
 
Hamorapaa kashatusahaulishaa kila kitu sasa sio kwa spidi hizoooo
 
Yaani kuitisha prescon tu,tena hawajui anaenda kuongea nini,
tena mtu amewahi kuwa topliner wa chama,anafikia hatuwa ya kunyooshewa bastora na kereng'ende fulani wwwwhhhhyyyy?

Ina maana sasa makirikiri wanaendesha nchi kwa mtutu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…