mama kubwa
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 6,230
- 9,889
Hata mie nimeshangaa ushujaa wa wana habari wakati Harmo mbio anachanja mbuga wao wanaendelea kuchukua matukio. Lile jambo lingetokea bila kuwepo watu huvi ss tungesema mengine.Pia kuna somo katika hiyo clip. Watu wengi waliokuwepo pale hawaonekani kutishika kwa kutolewa silaha hiyo. Niliwahi kuwaambia watu kuwa, usiombe kuwaongoza watu waliojizira (waliokata tamaa) mwisho wake huwa mbaya sana.
Kama mamlaka husika hawataitafakari video hiyo na kujifunza kitu, basi tutaianza Tanzania iliyotajwa tajwa.
MUNGU HAWEZI KUTUPATIA AMANI WAKATI TUNAMUOMBA HUKU TUMESHIKA MAPANGA.