Harmonize akiwa na Boss wake mpya

Harmonize akiwa na Boss wake mpya

Kati ya makosa ambayo mashabiki wanafanya ni kuabudu kuwa wasafi ndiyo kila kitu. Mwacheni naye ajaribu njia yake kama Diamond alivyotafuta njia yake, akishindwa atajua mwenyewe namna ya kuendelea. Ukiangalia Youtube, nyimbo za WCB zenye views zaid ya milioni 30 ni zile zinazohusisha wasanii wa nje tu, lakini WCB wasanii wa ndani tu hakuna aliyefikisha views milioni 30 wakati huyu dogo kaweza kufikisha milioni 50 kwa wasanii wa ndani tu.
 
Rayvan anajua kuliko harmo
[emoji23][emoji23] wewe sikutofauti na wanaosemaga mbappe ni Bora kuliko neymar kasikilize Atarudi,nevergiveup,nambie,bado,Aiyola,niteke,
alafu sikiliza na dukalavipodozi,chumaulete,wasiwasi,chombo
ndio utagundua rayvan hata kupangilia mashairi hawezi anaimba kichizi chizi
 
Kati ya makosa ambayo mashabiki wanafanya ni kuabudu kuwa wasafi ndiyo kila kitu. Mwacheni naye ajaribu njia yake kama Diamond alivyotafuta njia yake, akishindwa atajua mwenyewe namna ya kuendelea. Ukiangalia Youtube, nyimbo za WCB zenye views zaid ya milioni 30 ni zile zinazohusisha wasanii wa nje tu, lakini WCB wasanii wa ndani tu hakuna aliyefikisha views milioni 30 wakati huyu dogo kaweza kufikisha milioni 50 kwa wasanii wa ndani tu.

Wasanii wa ndani au msanii wa ndani maana ngoma zote za harmonize zenye viewers wengi zaidi Diamond yupo
 
Kitendo cha msanii mkubwa kama Harmonize kukosa visa hivi karibuni kinaonyesha huko anapotaka kwenda sipo, maana part time promoters tu wa ughaibuni ambao kazi zao maalum ni kubeba maboksi wakitaka kumpeleka ulaya msanii ata alietoka majuzi tu wangempatia visa kwa sababu wanaelewa utaratibu.

Mwanzo tu huko anapoenda inaonekana timu yake ni amateurs kwenye international arena.

Hivi karibuni nilikuwa nasikiliza sakata la Taylor Swift na ugomvi wake unaoendelea kwenye record label mchambuzi akawa anadai wasanii wakubwa awategemei tena distribution za record labels
kwa sababu ya streaming platform lakini kiuhalisia bado labels ni muhimu.

Akadai artists ambao ni brand kubwa kama Taylor Swift wanaweza jitegemea kwa sababu wana fan base inayoeleweka yeye mwenyewe ana followers zaidi 100m Instagram that enough of a marketing base.

Hila kwa wasani wakawaida wengi bado wanahitaji labels za kuwapa connections, ku promote kazi zao na kuwatangaza kimataifa mfano mkubwa lil Wayne album yake ‘Tha Carter V’ aijafika mbali kwa sababu aina back up nyuma yake haya mambo sio rahisi so they say.

Na kwa kusikiliza interview ya Sallam nimejifunza who is the real brain behind their international success na sio kila kitu rahisi unaweza kuona mbona fulani anafanya lakini shughuli ya kuweza kushawishi kitu kwa watu usiowajua inataka interpersonal skills na kuelewa mbinu za kuwapata kwa njia njia nyingi another skill which needs mastering.

Sijui lakini sioni mwisho wa Harmonize kuwa mzuri, hila wasafi nao lazima waanze kuelewa terms za mkataba za wasanii wanapokuwa wakubwa lazima zibadilike to include artistic freedom Harmonize na Rayvanny wa leo awawezi kuwa na terms za mikataba walizoanza nao na kila mtu anamujitaji mwenzake.
 
Wasanii wa ndani au msanii wa ndani maana ngoma zote za harmonize zenye viewers wengi zaidi Diamond yupo
Nilichosema ni kuwa Wasanii wanatunga nyimbo zao, halafu wanatafuta wasanii wengine nje ya nchi kuwashirikisha ili kuupa wimbo push; ndivyo ilivyo. Sasa Harmonize naye anazo nyimbo nyingi ambazo ametunga na halafu kushirikisha watu wa nje. Lakini wimbo wake aliokuwa ameplani kumshirikisha Davido,ila Diamond akaomba ndiye ashirikishwe nbadala yeke dio wimbo wenye views nyingi sana kuliko zote WCB ambazo hazikushirikisha mwimbaji wa nje. Hatujui iwapo angemshirikisha Davido kama alivyokuwa amepanga matokeo yangekuwaje.

Tumwache naye ajaribu njia yake; akishindwa basi atajua la kufanya. Ana exposure kubwa sana sasa hivi.
 
Simshangai kwa sababu amekua kisanaa na kiakili pia siku zote mtoto akikua kiakili anahama nyumbani kwa baba yake anakwenda kutengeneza mji wake anajenga familia yake ila akidumaa atafika miaka 40 nakuolea nyumbani anabakia kusubiri baba afe arithi nyumba na mali

Binafsi nnampongeza harmonize sababu ana akili ameweza kujitambua mapema kutengeneza ngome yake ili na yeye awape vijana wengine ajira

Domo kama ni mwerevu na ana roho safi kama anavyo jionesha kwa jamii alitakiwa ampongeze tena amuongezee na mtaji kisha afanye sherehe kuthibitisha kwamba kijana wake amekua na anaweza kujitegemea nadhani hiyo ndio itakua fahari kwake zaidi
Mkuu umenena. Nashangaa watu wanavyomuombea mabaya Harmo tunatakiwa tumuombee mafanikio zaidi nae huko akawasaidie wengine kama nae alivyosaidiwa .
 
Hakina connection ni pure businessna hapo specialist wa.mambo hayo ya contacts and networking ni hiyo dada mkenya.

Ukitaka collabo na Temi Nigeria unamcheki tuu mnafika Bei na vigezo particular fanbase manlipana mnatoa track hakina connection ingine zaidi ya hiyo.

Wasiwasi wangu ni experience ya huyo Jembe ni Jembe, sidhani kama anaconnection kubwa kwenye industry hasa kimataifa kumzidi Sallam SK, huyu jamaa anafanyia majaribio kupitia Harmonize, kama matokea hayatakua sawa na expections zake basi huo ndo utakua mwisho wa Harmonize. Kwa sasa tuuachie muda utatupa majibu.
 
Na hapa Kuna mkono wa Raisi wa dsm lakini technically ni kumuinua harmo na business investment period
 
Hakina connection ni pure businessna hapo specialist wa.mambo hayo ya contacts and networking ni hiyo dada mkenya.

Ukitaka collabo na Temi Nigeria unamcheki tuu mnafika Bei na vigezo particular fanbase manlipana mnatoa track hakina connection ingine zaidi ya hiyo.
Haha haha haha haha hah unaongea kama umekatika kichwa, unadhani ni rahisi kama kwenda chooni? Tafuta wewe hizo contact zake mtumie email, akikujibu share humu tafadhali..
 
Akitaka apotee kwenye ramani aondoke WCB
Acheni ujinga nyie watumwa,akili fupi ndio huwaza hayo utafia kwenye ualimu wa shule ya msingi usio na maslahi zaidi kula na madeni kwa mangi
 
Rayvan anajua kuliko harmo
Rayvanny hamna kitu, huyo dogo boya Sana, mwaka Jana na mwaka huu ametoa wimbo mmoja tu mzuri ule wa reggae, zingine zote ni nguvu ya Mond kushirikishwa, nyimbo kama natafuta Kiki na mbeleko zilimleta close Sana kutembea sambamba na konde boy, mara ghafula dogo kaanza kuchanja mbuga kusikojulikana, mara pochi Nene, Mara Timua vumbi, mara Nyegezi, mara paranawe nyimbo za kifala kabisa, mwenzake huku anapiga nambie, happy birthday na goma la Karne Kwangwaruu .....

Rayvanny arud kwenye mziki uliomtoa sababu saut yake ni nzur Kwa kuimba hata live anaweza kuimba kuwazidi hata konde boy na Mond, Mond anatumia nguvu nyingi Sana kumpush dogo, Ila dogo nyimbo zake za karbuni nyingi miyeyusho...
 
Ajabu ya Wabongo; ngoja msanii mpya atangazwe WCB halafu aanze kufanyiwa promo! Hawa hawa wanaosema bora aondoke tu, ndio hao hao watakaokuja tena hapa na kusema WCB wanamfanyia promo msanii wao ili kummaliza Harmonize huku wakisahau kwamba hata huyo Harmonize kafika hapo kwa promo!!

Wanaoleta hizo story za kikuda ni Team Kiba.
 
Back
Top Bottom