Harmonize akiwa na Boss wake mpya

Harmonize akiwa na Boss wake mpya

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Huku uongozi wa WCB kupitia Said Fella ukisisitiza hautabembeleza Harmonize kutumbuiza Wasafi festival na Kama Harmonize anataka kuondoka aage kwa amani.
Harmonize amekuwa akionekana na boss wake mpya Jembe Ni Jembe wakipanga mikakati mbalimbali
Screenshot_20190820-192832~2.jpeg
Screenshot_20190820-192812~2.jpeg
 
Huku uongozi wa WCB kupitia Said Fella ukisisitiza hautabembeleza Harmonize kutumbuiza Wasafi festival na Kama Harmonize anataka kuondoka aage kwa amani.
Harmonize amekuwa akionekana na boss wake mpya Jembe Ni Jembe wakipanga mikakati mbalimbaliView attachment 1186225View attachment 1186226

Bora aage kwa amani wakubaliane tu kwamba naye inabidi apae sasa kwani amelelewa vyakutosha ila kujifanya nyota wakati wasafi ndo wamemtambulisha ulimwenguni ni dharau ambayo sisi waswahili tunaufanya lakini inamadhara makubwa sana.

Inafahamika hawezi kubaki Wasafi maisha yote kwani inabidi wasanii wengine pia wapewe fursa ya kung’aa ndo tasnia iendelee na wengine nao wapate hela ila heshima ni muhimu.

Diamond alimbeba vizuri asije akaharibu
 
Sijui ni damu ya enterpreneurship au ni nn lakin sipendi mtu anaepiga chini ya mkanda...huyu jembe ni jembe anakosea sana mtu katengenezwa mpaka kawa hivyo then unaanza lobbying na hatimae atamtupa tu..mbaya sana...kwenye biashara mtu wa namna hii sipatani nae kabisa
.....jamaa ataivunja wasafi in a Half...Believe me !
 
Simshangai kwa sababu amekua kisanaa na kiakili pia siku zote mtoto akikua kiakili anahama nyumbani kwa baba yake anakwenda kutengeneza mji wake anajenga familia yake ila akidumaa atafika miaka 40 nakuolea nyumbani anabakia kusubiri baba afe arithi nyumba na mali

Binafsi nnampongeza harmonize sababu ana akili ameweza kujitambua mapema kutengeneza ngome yake ili na yeye awape vijana wengine ajira

Domo kama ni mwerevu na ana roho safi kama anavyo jionesha kwa jamii alitakiwa ampongeze tena amuongezee na mtaji kisha afanye sherehe kuthibitisha kwamba kijana wake amekua na anaweza kujitegemea nadhani hiyo ndio itakua fahari kwake zaidi
 
Back
Top Bottom