Harmonize atoa ngoma ya kwanza tokea ajiengue WASAFI. Ashindwa kufikisha views 100K ndani ya masaa 10

Harmonize atoa ngoma ya kwanza tokea ajiengue WASAFI. Ashindwa kufikisha views 100K ndani ya masaa 10

Sisi watu wa mtwara tunampenda sana harmonize na atafikisha views hata milion 10
watu wa mtwara na nani? jisemee mwenyewe,binafsi nasema hivi kijana huyu nje ya wcb kumantain hii status yake ni ngumu,wcb inambeba sana kwa kila.kitu....kwa sisi tunaofahamu ukweli hatuna maneno mengi sana,tunaangalia mchezo tu unavyoenda..🙏
 
Msanii Harmonize aka Konde Boy ametoa ngoma mpya akiwa na Eddy Kenzo kutoka Uganda inayoitwa 'Inabana'. Ikumbukwe hii ngoma yake ya kwanza tokea akiwa msanii Solo, hivyo kionjo cha Wasafi kama ilivyozeoeleka hakipo, kinasikika kionjo cha Dully Sykes 'ooh nice, This is Serious'. Pia video amefanya kwa Hanscana.

Video mpaka sasa tokea iwekwe ina masaa 10 na imetazamwa mara 65,000 (65K)

Mimi nimependa hapa ' ....Fundi kakosea kuishona, hata kichwa hakiezi ingia ...INABANA...🎤🎼🎹🎶

Angalia kichupa hapa


Wewe utakua mchawi au unaroho ya kichawi sana.
 
Anafikishaje wakati wale mnaowalipis bundle wapo upande ule .... Yaani hi inadhihirisha kama kweli ni michezo yao wcb ....
Mbna mnaanza kusingizia mapema, unafkr nan hapend kufanya hvo ili apae, kama kuna kununua view bas anunue na yy,
 
Kuna mtu yoyote anaweza kunielezea ile Inabana ft Chamillion iliishia wapi?
 
Nyimbo ya eddy kenzo msichoelewa ni nini hapo
 
Nyimbo ya eddy kenzo msichoelewa ni nini hapo
Ukiona wameandika FEATURING eg Eddy Kenzo featuring Harmonize (Nyimbo ya Eddy amemshirikisha Harmonize),ila hii ni Eddy Kenzo X Harmonize (Nyimbo ni ya wote Harmonize na Eddy Kenzo).

Hii nyimbo ni ya Harmonize na Eddy Kenzo.
 
Natafuta utofauti wa wasafi fm/tv na clouds fm/tv siuoni kwa hili linaoendelea juu ya Harmo.

Au nawao Wcb wanataka kumpoteza harmo, Kama clouds walivyokuwa wanafanya?.

Harmo kugomea show zinazoandaliwa na wcb kunautofauti na diamond kugomea show zilizokuwa zinaandaliwa na clouds, au ndio kusema wcb nao wanawanyonya wasanii kama inavyosemekana kwa clouds?.

Marehem Ruge alikuwa akija hadharan anasema hana tatizo na msanii yeye kama yeye bali nimatatizo yakikazi kati ya msani na clouds, Je kuna utofauti nahivi anavyokuja Salam kusema wcb haina tatizo na harmo kama akifata taratibu na sheria zakujitoa wcb, huku ngoma zake zikiwa hazisikiki Tena wadafi fm/tv?.

Najaribu sasa hivi kutafuta utofauti wa clouds na wasafi Media kwenye kudili nawasanii hasa juu yahili la Harmonize siuoni.

Naamini katika ubepari kwahiyo wanachofanya clouds nikutafuta faida zaidi kama wanachofanya wasafi wala sio kosa, kibiashara ndio inavyotakiwa.

Kwa maana hiyo wote niwanyonyaji.
 
Jamani tafadhalini! Ndege irudi shime!
 
Back
Top Bottom