Harmonize atoa ngoma ya kwanza tokea ajiengue WASAFI. Ashindwa kufikisha views 100K ndani ya masaa 10

Harmonize atoa ngoma ya kwanza tokea ajiengue WASAFI. Ashindwa kufikisha views 100K ndani ya masaa 10

Natafuta utofauti wa wasafi fm/tv na clouds fm/tv siuoni kwa hili linaoendelea juu ya Harmo.
Au nawao Wcb wanataka kumpoteza harmo, Kama clouds walivyokuwa wanafanya?.
Harmo kugomea show zinazoandaliwa na wcb kunautofauti na diamond kugomea show zilizokuwa zinaandaliwa na clouds, au ndio kusema wcb nao wanawanyonya wasanii kama inavyosemekana kwa clouds?.
Marehem Ruge alikuwa akija hadharan anasema hana tatizo na msanii yeye kama yeye bali nimatatizo yakikazi kati ya msani na clouds, Je kuna utofauti nahivi anavyokuja Salam kusema wcb haina tatizo na harmo kama akifata taratibu na sheria zakujitoa wcb, huku ngoma zake zikiwa hazisikiki Tena wadafi fm/tv?.
Najaribu sasa hivi kutafuta utofauti wa clouds na wasafi Media kwenye kudili nawasanii hasa juu yahili la Harmonize siuoni.
Naamini katika ubepari kwahiyo wanachofanya clouds nikutafuta faida zaidi kama wanachofanya wasafi wala sio kosa, kibiashara ndio inavyotakiwa.
Kwa maana hiyo wote niwanyonyaji.
Nyimbo za harmonize zinapigwa sana tu uku WCB kila siku Wasafi TV lazima niitazame.
 
Msanii Harmonize aka Konde Boy ametoa ngoma mpya akiwa na Eddy Kenzo kutoka Uganda inayoitwa 'Inabana'. Ikumbukwe hii ngoma yake ya kwanza tokea akiwa msanii Solo, hivyo kionjo cha Wasafi kama ilivyozeoeleka hakipo, kinasikika kionjo cha Dully Sykes 'ooh nice, This is Serious'. Pia video amefanya kwa Hanscana.

Video mpaka sasa tokea iwekwe ina masaa 10 na imetazamwa mara 65,000 (65K)

Mimi nimependa hapa ' ....Fundi kakosea kuishona, hata kichwa hakiezi ingia ...INABANA...🎤🎼🎹🎶

Angalia kichupa hapa



Wimbo mashairi yake ni mabaya halafu melody yake siyo nzuri kama ya kwangaru; inakosa sifa zile za muhimu kama peak, kuchanganya steps, skips, na leaps; umetumia steps nyingi sana, halafu sehemu nyingi hazina cadences zinazomvuta msikilizaji.

La muhumi mimi nitakata rufaa wimbo huu upigwe marufuku kwa sababiu unasema nyuma "Kichuguu;" kutumia jina langu bila kibali ni kukiuka privacy yangu na kunivunjia heshima mbele ya my wife wangu! Itabidi a-apolojaizi
 
Back
Top Bottom