Harmonize hajakosea kuhusu Madam Ritha, tuache mitazamo hafifu katika imani

Umeandika ujinga mtupu, sijda ni kwa Mungu tu huyo harmonize ni mjinga na mpumbavu na amekosea mno kumsujudia mwanaadamu mwenzake
 
"sisi ni miungu hivyo Mungu yupo ndani ya madam Ritha". Kwa phrase hii umepotosha mkuu.

Sisi siyo miungu, sisi ni mfano wa Mungu. Ukishasema miungu with small 'm' tayari unakuwa unazungumza kitu kingine tofauti kabisa na Mungu with Capital 'M' ambaye huyu ni Mungu mkuu (mfalme wa majeshi) aliye juu Mbinguni.

Otherwise, hoja yako siyo mbaya kwasababu hata Pope John Paul II alipozuru Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 1990 alisujudu kama Harmonize mara tu alipotua airport, lakini haikumaanisha kwamba alikuwa anaisujudia nchi ya Tanzania.
 
Mbona tena huyo mdada anamshika kwa kumpapasa kidume kiunoni... binafsi mikono kama hiyo ikinishika tu lazima "Kichwa wazi" aanze vurugu hapo
 
Hao watu wanaojadiliwa kwenye hii mada,kwani ndio ni kina nani huko Daslam?
 
Kijana anapenda sana wanawake waliomzidi umri.
 
Jaman sisi wengine tupo shamban vip kwan huko mjini hao watu naona uzi wa pili huu unawazungumzia vip wanakulana au
 
Kwa tunavyomjua chinga haangalii umri,akijichekesha anae.
 
Dogo yupo sawa na atapata zaidi ndio maisha hayo sio mtu anakusaidia harafu ukitoboa unamletea madharau ya porini...
 
Sawa itoshe huo usumbufu wa maelezo naendelea kunywa ushindi wa yanga ni mkubwa mno.
Iko hivi..kuna taarifa ya awali kabla ya hii uliyotoa ambayo unaifahamu lakini hujaitoa kwa kudhani kila mtu anafahamu..kwa uandishi mzuri ili uende sambamba na wasomaji wapya wa habari yako ungetoa maelezo kidogo ya utangulizi ya kile kilichotokea ambacho kimepelekea wewe kuandika au kusema hicho unachotuambia.
Kubali kukosolewa ni njia mzuri ya kujifunza.
 
Uisilamu ni Elimu pana,kuna sijda za aina mbili,sijda ya Kumsalimu Mwenyezi Mungu peke yake,ndiyo ile waliofanya mitume wote,akiwemo Ibrahimu, Daudi,Musa na Yesu,na ndiyo wanaofanya Waisilamu kupitia Mtume Muhammad (S.A.W)

Kuna Sijda ya kawida ambayo Maraika na jina waliambiwa wamsujidie Adamu,yaani unainamisha kichwa chini.

Ambayo huamkiwa hata wafalme na Viongozi wakubwa
 
Unaweza kuthibitisha hayupo??
Nikishindwa kuthibitisha hayupo, hilo halithibitishi kwamba yupo.

Kwa sababu naweza kushindwa kuthibitisha hayupo kwa kuwa hayupo.

Kisichokuwepo kinaweza kutowezekana kuthibitishwa kwamba hakipo, kwa sababu hakipo ili kuthibitishwa kwamba hakipo.

Falsafa ya uthibitisho inahusika na vilivyopo, visivyopo havithibitishiki kwamba havipo, kwa sababu havipo ili vithibitishike kwamba havipo.

Kama yupo, unaweza kuthibitisha kuwa yupo?

Hujajibu swali, umelikwepa tu.
 
Ritha yupo too emotional kidogo tu analia...
 
Harmonize kamshukuru Mungu kwa kupitia Madam Ritha, shukrani huitikiwa na kubarikiwa nq Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…