Harmonize ni mbumbumbu wa sheria, mchanga wa mahusiano na mshamba bado wa umaarufu

Harmonize ni mbumbumbu wa sheria, mchanga wa mahusiano na mshamba bado wa umaarufu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Kitu kimoja kuhusu pesa nyingi: Hufunua undani wa mtu katika uhalisia wake....!!! Hata wewe ukizipata leo tutakujua tuu.. Waswahel wanasema pata pesa tujue tabia yako....

Shule ni muhimu sana sana kile kitendo cha kukaa darasani miaka kibao hutufunza mengi hata tusipofaulu mitihani..japo baadhi hawaelimiki hata wafike mpaka chuo kikuu.

Kuna wachache waliobahatika kuwa na akili na maarifa ya kuzaliwa nayo... Hawa ndio ambao huelimika bila hata ya kusoma sana
Ni wepesi kushika vitu vipya
Ni wepesi kuwa wabunifu
Ni wepesi kubadilika kuendana na mazingira yaliyopo nknk

Harmonize kiasili shule hamna na hii si dhambi hata kidogo bali ni mfano wa mamilioni ya watoto wetu waliokosa shule kwa sababu mbalimbali... Mazingira ya umasikini, ndugu wazazi na hata jamii vimezima ndoto za vijana wetu wengi kielimu.

Kuna wale wachache ambao automatically walijiona kabisa kuwa shule sio sehemu yao, hao walijiona kabisa vipaji na vipawa vyao viko kwenye sanaa mbalimbali, biashara nk

Harmonize ni nmojawapo aliyekosa elimu kwa sababu zozote zile na kuja kuibukia kwenye sanaa ya mziki.. Na amefanya vema kwakweli mpaka hapo alipofikia.. Kutompongeza kwa hili ni wivu.

Katika njia yake ya kutafuta mafanikio zaidi amejikuta anakabiliwa na changamoto kadhaa ... Ambapo anahitaji timu makini, somi na yenye weledi kuweza kumvusha.

Mahusiano
Kwa umri wake na pesa kiasi aliyonayo, haya anayofanya sasa wala si ajabu sana..hata wewe ungefanya na pengine zaidi... Lakini Harmonize kwenye future ya carrier yake ya mziki anahitajika kuwa na washauri weledi zaidi.

Inajulikana wazi hawa mabinti vibibi wa bongo movie walivyo makaburi ya pesa na matajiri wa skendo... Hawa wapo tangu enzi za mapapaa kina Msofe, wazee wa bandari, wauza unga, watoto wa mjini nknk.. Leo hii ndio aje kudate nao na kurusha picha za mahaba mazito mitandaoni!? Haya ni majambazi ya cash..na yakishakuchuna na kukuchoka yanakutengenezea skendo kisha yanakupiga chini.

Sheria
Kwa maisha anayoishi Harmo ya mziki, ya mitandaoni ya competition kwenye game, ya kupokonyana madanga ya mjini ya kuoneshana umwamba nk.. Kuna vitu haviepukiki hata atafanyeje navyo ni kuundiwa kashfa hata za uongo..kama naye alivyofanya kwa wengine.. Aishi kibon touni, akipatwa hapa naye anatafuta pa kumpata mtu wahuni ndivyo wanavyomalizana.

Ishu ya kutishia kuwapeleka watu aliowataja kwa majina kuwa atawapeleka mahakamani awafunge na wamlipe mabilioni ya pesa ni upuuzi mtupu na hao wanasheria wake wanamlia pesa tu
Kesi za fidia kama hizo huwa na mambo mengi mno mpaka watu hukata tamaa.

Mbaya zaidi keshaanza vibaya kwa kuwataja watuhumiwa wake kwa majina na kuwahukumu tayari huku akitambua wazi kuwa mahakama pekee ndio yenye uwezo wa kuhukumu.. Mambo ya sheria ni nyoko sana keshaitia doa kesi yake.

Kwa kinachoonekana wito ama tisho la wakili wake hakuna mahali anamtaja Harmonize kwa majina yake rasmi..hapa tayari napo kuna shida.

Natambua katishia kuwa wahusika itakuwa mwisho kuonekana kwenye page zao mitandaoni...Mmh Instagram na FB kwa mfano ina mitifuano mingapi kila siku duniani, tena mibaya kabisa mpaka ikimbilie kufunga account za wambea njuka?

Ushamba wa umaarufu
Bado Harmonize ana kitete kile cha ufukara, bado hajiamini lakini mbaya zaidi ana management ambayo haiko vizuri sana au haisilizi au haimshauri vema au haina weledi na exposure ya kutosha. Kusema kwamba jina lake kalijenga kwa mabilioni ni fix za kishamba sana.

Kuona kwamba kafanyiwa figisu na wabaya wake nalo ni ushamba pia.. Kwa hapo alipo anategemea kweli akose maadui kila kona?

Ajaribu kuwapuuza aone! Ishu za kupelekana mahakamani kudaiana fidia zitamuongezea stress za kufa mtu...kuna kesi maelfu za fidia zina umri sawa na wake.. Hazijalipwa!

Na je kesi zake hizo ni jinai au ni madai?
 
JamiiForums1302421012.jpg
 
Naona umetumwa na Diamond. Sasa Harmonize kwani yeye ni mwanasheria!?
Mtaenda kuyaeleza hayo mahakamani.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] Mshana endelea na fictional stories kuhusu uchawi na mazimwi.
Mambo ya sheria waachie wanasheria.
Kuna vingine wala havihitaji akili kubwa kujua ni utopolo na lack of knowledge
JamiiForums-74704411.jpg
 
Tuliite Tangazo, Onyo, Ilani, Wito, Barua ya madai au tuache ivyo ivyo kuwa Tangazo kwa Umma?

Ila hapa Learned Brother kachemka pakubwa. Sasa inaanza kusambaa kwenye ma group ya mawakili, utasikia 'jamani kuna kituko huko' mzigo unawekwa paap!
[emoji3][emoji3][emoji3] wakili msomi
JamiiForums1302421012.jpg
 
Naona umetumwa na Diamond. Sasa Harmonize kwani yeye ni mwanasheria!?
Mtaenda kuyaeleza hayo mahakamani.
😀 😀 😀 Mshana endelea na fictional stories kuhusu uchawi na mazimwi.
Mambo ya sheria waachie wanasheria.


Threads zinaporomoshwa kila baada ya dakika 2 halafu contentless.

Linafosi kuzungumzia vitu ambavyo hata halivijui vizuri.

Haya Harmonize hajasoma, vipi Jembe ni Jembe ??

Hayo mambo ya kesi huwa ni beat tu, ili watu waache kusambaza taarifa, hakuna mwenye akili timamu asiyejua kuwa hakuna kesi hapo. Kushtaki siyo lazima utangazie umma ndio uende mahakamani.
 
Hili ni moja ya mizee mipumbavu iliyo overated sana humu. Mr. know-it all.

Threads zinaporomoshwa kila baada ya dakika 2 halafu contentless.

Linafosi kuzungumzia vitu ambavyo hata halivijui vizuri.

Haya Harmonize hajasoma, vipi Jembe ni Jembe ??

Hayo mambo ya kesi huwa ni beat tu, ili watu waache kusambaza taarifa, hakuna mwenye akili timamu asiyejua kuwa hakuna kesi hapo. Kushtaki siyo lazima utangazie umma ndio uende mahakamani.
Mashabiki wa Mshana watakushukia kama mwewe..
 
Back
Top Bottom