Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Nimeisikiliza sana.
Naomba nikwambie kitu na ukifanyie kazi.

1. Katika maisha yako wapende sana watu wanaokunyanyasa, hao wanakupa presha ya kufanya kitu uondokane na manyanyaso...mwisho wa siku utakuwa bora sana.

2. Usipende kujihurumia huwezi kufika mbali.

Kama Daimond anawakandamiza wasanii wake naomba nimpongeza kwani mwenye akili atapigana ajitegemee.
Point
 
relaaaax mwache kijana aongee mnataka afiche maovu yenu ili muendelee kumpaka ubaya.

msipanic kubalini tu kuchutama mmeachwa uchi.
Unazungumzia uchi
Acha kua na mihemko, wapenzi wa nasibu msiwe na mihemko, Siwezi kujua ameachieve nini baada ya kutoka huko, yaweza kua mabaya au mazuri, ila ukweli unabaki pale pale kwamba nasibu sio mfano wa kuigwa, unamsaidia mtu then unaanza kua na roho mbaya akianza kukuzidi, halafu mbaya zaidi unasikiliza wapambe nuksi wenzio wanakujaza maneno, na bila kufanya uchunguzi wako unakurupuka kuanzisha chuki, ina mana kama sio simu ya JPM alikua asipewe termination contract, ni chuki za aina gani hizo..

Nasibu ana represent kati ya vijana wapumbavu ambao wanadhani unaposaidia mtu lazima akulipe fadhila, pia hutakiwi kufanikiwa zaidi yake in which hizo ni akili za kipumbavu..kumbe unaweza kua na pesa lakini ukawa na akili za kishamba na kipumbavu.
Umekula leo?

Una uhakika usiku ulipata usingizi wa kutosha
 
Jamaa maku sana,unabana hadi collaboration zisitoke za Shomadjozi na master KG zisitoke.

Nasikia hata Darrasa walibana show yake Oman,wakasema jamaa waachane nae eti ni mvuta bangi.Roho mbaya sana Domo
Kwani hao wakina shomadjozi na masterKG meneja wao ni Diamond mpk azuie collabo zisitoke

Use your brain
Akili mtu wangu
 
"Wamakonde hamtuwezi kiserikali, hamtuwezi kipesa na hamtuwezi kiuchawi vilevile"
 
Punguza kuponda mdau


Mimi naamini hata wale wanaijeria wanaimba visivyoeleweka.....

Kama unataka uendelee kubishana weka hapa nyimbo za wanaijeria ulizozielewa
Wanigeria wanaimba Nigerian Pidgin, na inatumika sana huko nje, hata BBC wanatoa taarifa kwa lugha hiyo (Domot - BBC News Pidgin).

Shida ninayoponda ni kujaribu kusound kama wanaija huku hauna maana kwenye lyrics zako zikipelekwa huko nje, na zikiletwa huku kwa waswahili tunakuwa pia hatuelewi.

Mfano huu ni wimbo wa Burna Boy Anybody, unamaana inayoeleweka na hata ukifuatilia ujumbe wake unauelewa yeye mwenyewe anauongelea hapo kwenye video.


Kucopy sound ya Nigeria au South Africa ili uusukume kazi zako kimataifa haina shida ila, lugha iwe inamaana....na sio kwa Harmonize tu kuna wasanii wengi tu siku hizi unawaoona wanahangaika kuiga sound kutoka upande fulani wakati lugha ni mzigo. Ukimsikiliza Anjella hapa hata kama amefanya cover utaona fluency ya lugha iliyopo,



Angeweza kutumia mbinu kama kuwa na mtu anayekusaidia kuweka mashairi sawa mwenye command nzuri ya english au hiyo pigdin anayotaka kuitumia, na kukaza zaidi kwenye kuongeza fluency ya matamshi kama anataka kuimba kiingereza. Penye ukweli tuseme ukweli, binafsi baada ya kuona alivyokuwa akipondwa kuhusu english yake kwenye Afro East nilitegemea ningeona mabadiliko ambayo ni positive ila ni kama ameongeza tu matatizo.
 
Katema nyongo zake
Kutema nyongo haisaidii chochote, back to Ommy dimpoz, sheta, rich maboko na wote hawa wanavipaji vya kufa mtu ila walipoanza kulalamika kwamba Diamond anawazibia riziki zao na tayari hiyo ilikuwa ni indication ya kufeli kwenye mziki

Back to Diamond during Ruge Era, he stand alone against big media tycoon and win the battle

Wamakonde Endeleeni kupambana na acheni kutia huruma mjini
 
Kutema nyongo haisaidii chochote, back to Ommy dimpoz, sheta, rich maboko na wote hawa wanavipaji vya kufa mtu ila walipoanza kulalamika kwamba Diamond anawazibia riziki zao na tayari hiyo ilikuwa ni indication ya kufeli kwenye mziki

Back to Diamond during Ruge Era, he stand alone against big media tycoon and win the battle

Wamakonde Endeleeni kupambana na acheni kutia huruma mjini
Polen sana.
Mmevuliwa nguo
 
KONDE BOY ALIONDOKA NA RAMANI YA VITA WCB.
------------------------------------------------

Wakati wasafi walipomsajili baba levo asaidiane na Juma lokole kwenye mashambulizi dhidi ya Harmonize. Niligundua, Harmonize anawaumiza vichwa WCB, huenda anaonekana tishio kwao, anawakera, kuna sehemu anawakosesha usingizi na kuwanyima amani ya moyo.

Inaoekana WCB hawakutegemea kama konde angeweza kusimama kimuziki bila uwepo wa lebo ya wasafi. Na kibaya zaidi, harmonize anatumia mbinu na formation ileile wanayotumia wasafi kushinda mechi zake.

Na wasafi hawajabadili mbinu za vita hata baada ya kuvunja ndoa na Harmonize. Hivyo inakuwa rahisi Konde boy kutunishiana nao misuli. Sababu anajua uimara na udhaifu wa mbinu zao ulipo.

Muda mwingi anaotumia baba levo Instagram kurusha vijembe, mafumbo, michambo na madongo kwa Harmonize. Inakupa picha, WCB bado hawajafanikiwa kupata mbinu sahihi za kuizika career ya Harmonize kimuziki.

Wakati ndoa ya wasafi na harmonize inalala mauti. Harmonize alitozwa faini ya milion 600 kama fidia ya kuvunja mkataba. Harmonize hakuondoka kifala (WCB) aliondoka akiwa ameiba ramani ya vita.

Ramani inayompa kiburi, na jeuri ya kuwavimbia kina Babu tale, Fela, na Nasibu mwenyewe.

Na kibaya zaidi wasafi hawajabadili mbinu za vita. Kama wangekuwa wamebadili mbinu, wasingemnunua baba levo asaidiane na Jumla lokole kumshambulia Konde boy jeshi.

Vita dhidi ya WCB sio kitu rahisi. Ni vita inayohitaji mtu uwe na timu yenye msuli wa pesa, timu inayojua fitna na hila zote za muziki wa bongo fleva. Timu yenye kukusanya watu wa kutengeneza antetion na kick kila siku.

Timu yenye uwezo wa kukesha macho ikitunisha misuli inapoibuka vita ya maneno kule Instagram.

Rich mavoko aliishindwa hii vita. Na leo macho yetu yanaona kaburi la mziki wake lilivyojaa nyasi."

Harmonize anaonekana kuicheza vema vita hii. Alipoamua kuanzisha lebo yake "KONDE GANG" alikuwa anaijuza dunia kuwa ameingia kwenye vita ya muziki na lebo yoyote ile.

Alikuwa anatuma ujumbe kwamba, "amejivisha mabomu na yupo tayari kulipuka na msanii yoyote anayetaka kuuchezea ugali wake. Harmonize amefanikiwa kwenye hii vita, hivyo kujiita JESHI anastahili.

By Green Osward
Hongera sana Mr, af nilikumic mno, [emoji7][emoji7]
 
Ila Harmonize ni mnafiki sana yule jamaa pia anapenda sana kuonewa huruma na kuonekana mwema sana wakati sio kweli, yani wanaume mnaongea then wewe unarecord ili iweje? kanishangaza sana jamaa hivi leo hii hata akiwa na ishu sensitive nani mjinga anaweza kubali kuongea nae ikiwa anajua nitarecodiwa, yeye kaona vyema but kwa watu wenye akili kaharibu vibaya mno.

Kutwa kumsema diamond yeye akirudishiwa moja anashusha magazeti na press anaita hahaha.. kamchonganisha vanny na serikali enzi za paula leo tena anachonganisha serikali na Diamond.

Tumuone sasa akifikia ukubwa na diamond si katoka wcb mbona hakui yuko pale pale anaongezeka mwili tu.
 
Heheee wacha movie iendelee. Ila harmonize sio wa kwanza kumkandia mondi kny vyombo vya habari.

Nikikumbuka ya zari siku hizi wamekua mabest nawacheck tuuuu
 
Ila Harmonize ni mnafiki sana yule jamaa pia anapenda sana kuonewa huruma na kuonekana mwema sana wakati sio kweli, yani wanaume mnaongea then wewe unarecord ili iweje? kanishangaza sana jamaa hivi leo hii hata akiwa na ishu sensitive nani mjinga anaweza kubali kuongea nae ikiwa anajua nitarecodiwa, yeye kaona vyema but kwa watu wenye akili kaharibu vibaya mno.

Kutwa kumsema diamond yeye akirudishiwa moja anashusha magazeti na press anaita hahaha.. kamchonganisha vanny na serikali enzi za paula leo tena anachonganisha serikali na Diamond.
Tumuone sasa akifikia ukubwa na diamond si katoka wcb mbona hakui yuko pale pale anaongezeka mwili tu.
Ukubwa ashafikia saiv amevimba km kapulizwa. Ila ukubwa kimuziki avute shuka aendelee kuota maana hafiki leo wala kesho. Alijaribu kiki nyingi kachemsha kaona hii ya wcb itamboost big time
 
Back
Top Bottom