Harmonize: Nimewalipa Wasafi Tshs milioni 500 kuvunja mkataba

Harmonize: Nimewalipa Wasafi Tshs milioni 500 kuvunja mkataba

Asihofu acha awalipe maana domo ana wivu sana, anataka awe mfalme peke yake, kwanza mwakani anakuwa mbunge atapata na uwaziri wa michezo, akichanganya na kipaji chake atapata hizo nyumba mapema tu.
Aaah wapi,bila Mond,Konde boy angetoka wapi!?
Ametusua kupitia mgongo wa Mond
 
Nimefatilia instagram yake naona wafuasi wameongezeka. Hata views za promo ya huu wimbo una views zaidi ya 200K.

Kiufupi Harmo kawa mjanja kuliko Mavoko. Kule kuna unyonyaji ila sasa utatokaje kama huna hela?
Ashukuru Mungu hizo nyumba zimemuokoa
Mkuu wapi ambako hakuna unyonyaji?
 
Aaah wapi,bila Mond,Konde boy angetoka wapi!?
Ametusua kupitia mgongo wa Mond
Jidanganye tu, maana mondi ndio kampa kipaji cha kuimba? Konde wakati anakashifiwa pale bongo star search alikuwa amepeleka kipaji cha upishi? Konde ni kama Mesi anasajiliwa na timu kubwa kwa kuwa ana kipaji. Mtasubiri sana aanguke lakini hamtashuhudia hilo kabisa.
 
acha umama wewe,usifananishe mmakonde wa chitoholi na mmakonde wa Mtwara mjini shubamiti
nawewe ni sawa na huyo hao wote ni wamakonde usianze ubaguzi wa wapi katoka wewe tetea kabila lako usiangalie alikotoka usubwada sana
 
Jana Nimemwona QBoy Amebaki Kuwa Kinyozi Tu, Kariakoo !

Domo Ukimchekea Utabaki Kupata Tu Sifa Mitandaoni, Mademu, Na Show Offs.

Ukichokwa Unapigwa Chini, Unapotea.

Harmonize Kashtuka Mapema. Anaweza Kuinuka
Kabisa yan yy anafanya vitu kwa faida yake
 
Akihojiwa na Clouds FM kwenye XXL amesema imemlazimu kulipa million 500 ili kuvunja mkaba na Kampuni ya Wasafi.

Amesema kampuni ya Wasafi walimzuia kutumia chochote kilichotokana na Wasafi ikiwemo nyimbo zake ,akaunt za mitandao ya kijamii na mengineyo.

Ili kuendelea kutumia nyimbo hizo imemlazima kulipa milion 500, amesema kuwa ameuza nyumba zake tatu na baadhi ya aseti na yupo kwenye hatua za kumalizia deni lake ili aweze kupiga nyimbo zake popote pale.

Kuhusu kugombea ubunge amesema kauli ya Rais ni kama sheria hivyo yupo tayari kutekeleza agizo la mheshimiwa.

2020 Harmonize mjengoni.!

Ameongeza kuwa ugomvi wa Vyombo vya habari unarudisha mziki nyuma.

Amewekea mfano Whozu na Marioo kuwa ni wasanii ambao wanashindwa wasimame na media ipi.

Hapa inaonesha kuna wasanii wengi wanapenda kushirikiana Wasafi fm ila wanaogopa kutengwa na Clouds.

Aachane na siasa!! Keshakuwa mwanamziki mkubwa....

Yaani kwa wimbo mmoja tu wa kumsifu na kumuabudu jiwe anaonekana anaweza ubunge!? Mbona tunakuwa wajinga hivi!!!
 
Ukimsikiliza vizuri dogo Harmonize tayari asha haribika kisaikolojia ( Kachanganyikiwa).
Eti kauli ya Raisi ni sheria, yaani Mie umenipa sifa nimefanya vizuri.. Kwanini na mie nisikupe Sifa hata Kinafiki.

Clouds wanazidi kumpoteza Huyu kijana, Hicho chakula ndio Kabisa.. Wanakula wanapotea.

Uzuri Korosho itasimamiwa vizuri.. Atajipatia Kipato huko
Yaani wewe chokoraa wa Jamii Forum unamuona harmo kachanganyikiwa !!!


Umute unaishi kwa dada yako unakula matunda ya jitihada za dada yako chumbani.
 
dogo una ki wivu flani katika maandishi yako una hakika gani sifa za raisi kwa konde ni za kinafiki

mwakani konde boy mjengoni ikuume vzr
Labda kama mgeni mualikwa, Mbona hata pierre ( Chiii) Kaingia mjengoni hakuna cha ajabu hapo
 
Back
Top Bottom