Harmonize rasmi amuimba Kabwili kipa wa Yanga

Harmonize rasmi amuimba Kabwili kipa wa Yanga

kenny mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2021
Posts
316
Reaction score
848
Hatimae msanii Harmonize rasmi ameachia wimbo alioshirikishwa na kundi la mabantu remix inaitwa Utamu, katika wimbo huo wa utamu remix Harmonize amesema kuwa ukimletea mambo ya kabwili unapunguza utamu[emoji1]

Ikumbukwe mchezaji huyo wa yanga ameandamwa na skendo ya ushoga kitu ambacho kimewafanya mashabiki wake kupata sitofahamu
 
Atimae msanii harmonize rasmi ameachia wimbo alioshirikishwa na kundi la mabantu remix inaitwa Utamu, katika wimbo huo wa utamu remix harmonize amesema kuwa ukimletea mambo ya kabwili unapunguza utamu[emoji1]
Ikumbukwe mchezaji huyo wa yanga ameandamwa na skendo ya ushoga kitu ambacho kimewafanya mashabiki wake kupata sitofahamu

Sent from my SM-J260T1 using JamiiForums mobile app
Hivi kabwili ndio yupo seriazi kabisa??
 
Yani siku hizi mambo yanashangaza huu wimbo umejaa maneno machafu. Nashangaa eti wanaouperform mbele ya watu wazima na redioni unapigwa.
Sijui kwanini nyimbo siku hizi zina maneno ya ngono tu
Sasa hivi ukiwaacha watoto kwenye tv wanajifunza ushenzi tu mm nimeweka cd na frash za masomo na nyimbo za din na katuni ila ndo uwaache waangalie tu utakuta wanakuimbia.... mpelekee moto.
 
Sasa hivi ukiwaacha watoto kwenye tv wanajifunza ushenzi tu mm nimeweka cd na frash za masomo na nyimbo za din na katuni ila ndo waachie waangalie tu utakuta wanakuumbia.... mpelekee moto
Ni ngumu sana kuwachunga watoto, mimi mwanangu ni mwendo wa channels za katuni lakini nashangaa anafahamu nyimbo nyingi sana. Nikimuuliza anasema anasikia kwenye school bus na wanafundishwa shuleni.

Potelea karibu ila home hakuna kutazama channels za miziki maana mtu huna hakika wimbo unaofuata watakuwa wanaimba nini.
90% ya nyimbo wanaimba ngono tu
 
Yani siku hizi mambo yanashangaza huu wimbo umejaa maneno machafu. Nashangaa eti wanaouperform mbele ya watu wazima na redioni unapigwa.
Sijui kwanini nyimbo siku hizi zina maneno ya ngono tu
Hii imeanza kitambo sana. Juzi Ijumaa mwanangu alikua anamaliza chekechea wakawa wanasherehekea na nyimbo zilizokua zinapigwa ni hizo za mpelekee moto, kanyaga, msambwanda kwa buku jero n.k.

Ni upuuzi mtupu, nakumbuka kipindi changu wimbo kama 'Kosa la Marehemu Hakuvaa Kondomu' huo wimbo hauwezi usikiliza mbele ya aliyekuzidi umri kwaajili ya uwepo wa neno kondomu, sawa sawa na ule 'Usione Soo' lakini kwa sasa msanii wa kiume ataimba jinsi gani ni hodari wa kumega na msanii wa kike ataimba jinsi gani ni hodari wa kumegwa mpaka na waume za watu.
 
Hii imeanza kitambo sana. Juzi Ijumaa mwanangu alikua anamaliza chekechea wakawa wanasherehekea na nyimbo zilizokua zinapigwa ni hizo za mpelekee moto, kanyaga, msambwanda kwa buku jero n.k...
Uko sawa kabisa hata mimi shuleni kwa mwanangu eti walikuwa wanapiga nyimbo hizi hizi kwenye hayo mahafari.

Nashangaa siku hizi watu wana ujasiri yani msanii mbele ya viongozi anaperform wimbo wa inapunguza utamu, sijui ipake wese.

Kweli nakumbuka kosa la marehemu ulikuwa huwezi uimba mbele ya watu waliokuzidi, hata usione soo sema nao ilifika muda ukazuiwa kupigwa wakasema unachochea ngono badala ya kupunguza.
 
Supplier anapeleka Sokoni bidhaa inayohitajika

Wakitaka Gongo peleka Gongo…ukijifanya mtu wa lishe ukawapelekea juice ya Chungwa na Mchicha wa kuchemsha utafunga duka lako kwa kukosa wateja
Yani siku hizi mambo yanashangaza huu wimbo umejaa maneno machafu. Nashangaa eti wanaouperform mbele ya watu wazima na redioni unapigwa.
Sijui kwanini nyimbo siku hizi zina maneno ya ngono tu
 
Huyo Harmonize aache kutafuta kiki kwa kijana kwa tuhuma ambazo hazina ushahidi wa moja kwa moja dogo akimfungulia kesi ya kumchafua asije baadae akaanza kuitisha press za kutia huruma
Kiukweli ni ujinga sana kwa wasanii wetu kutumia matukio machafu kwenye nyimbo zao, alianza kaka yake kwenye ishu ya amberruty naye kaiga
 
Kabwili kwani n kweli shoga?
Kajibu
Screenshot_20211214-120430_Instagram.jpg


Sent from my SM-J260T1 using JamiiForums mobile app
 
Hawa wapuuzi Basata wakiwapiga pin huwa wanapata support ya mashabiki wao ndio maana wamewaachia kipindi hiki wafanye wanavyotaka!

Imagine Nyambizi ya Dully Sykes ilifungiwa verse ya pili kama sikosei lakini hii unapunguza utamu inabondwa tu redioni na runingani!

Tukijisahau tutatumbukia shimo ambalo wa Marekani weusi wametumbukia, Bangi, madawa ya kulevya na matumizi ya ovyo ya bunduki sababu ya Hip hop

Si ajabu miaka michache ijayo mashoga, mateja na Ukimwi kushika kasi kwa sababu ya mziki wao wa kipuuzi huu.
 
Kabwili afungue mashtaka, hiyo ni kesi ya udhalilishaji

Na itakuwa fundisho kwa wasanii wengine wanaoharibu wasifu wa watu ili wa hit kwenye ngoma zao
 
Back
Top Bottom