Harmony OS 2 yaonesha kwamba China inajitegemea katika uvumbuzi wa sayansi na teknolojia

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111332852582.jpg
Hivi karibuni, kampuni ya Huawei ya China imetangaza rasmi mfumo wa simu ya kisasa Harmony OS 2 na vifaa kadhaa vinavyotumia mfumo huo. Hatua hii sio tu inamaanisha simu na vifaa vingine vinavyotumia mfumo wa Harmony OS 2 ni bidhaa rasmi inayoingia katika soko, bali pia ni alama kwamba Huawei imeanza kuchukua hatua kujibu ukandamizaji wa nchi za magharibi, ikiwemo Marekani.

Jina la kichina la mfumo wa Harmony OS 2 ni “Hongmeng”, ambalo maana yake ni kujenga dunia mpya. Mwonekano wa mfumo wa Harmony hauna tofauti kubwa na mfumo wa Android wa Google na mfumo wa IOS wa kampuni ya Apple, na kuna baadhi ya watu wana mashaka kwamba, mfumo wa Harmony ni mfumo wa Android ulioboreshwa. Lakini ukizingatia wazo la kubuni mfumo wa Harmony, tunaweza kugundua kuwa mfumo huu umefafanuliwa kama mfumo wa uendeshaji wa vifaa vya kielektroniki katika zama ya mtandao wa vitu na vitu IOT, ambao unaweza kutumiwa katika simu za kisasa na pia unaweza kutumiwa katika vifaa vingine vya kisasa yakiwemo magari.

Ubunifu wa Harmony haushangazi, kwa sababu kampuni ya Huawei inaongoza dunia nzima katika sekta ya ufundi wa mtandao wa 5G, pia imefanya utafiti wa muda mrefu zaidi kuhusu mtandao wa vitu na vitu (IOT) ikilinganishwa na kampuni ya Apple na kampuni ya Google. Hivyo Harmony si mfumo uliotolewa kutokana na ukandamizaji wa Marekani, ambao unatokana na wazo na teknolojia zinazoongoza. Hivyo, Harmony ina umuhimu mkubwa kwa utafiti wa teknolojia ya mtandao wa Internet na ujenzi wa mtandao wa IOT, pia ina maana ya kimkakati kwa kujitegemea kwa kampuni za teknolojia ya juu za China. Wakati Harmony ikielekea kuingia kwenye soko la kimataifa, soko kubwa la China litakuwa msingi wa ukuaji wa mfumo huo, na hatimaye mfumo wa Harmony utakuwa na uwezo wa kushindana na Android na IOS.

Kuanzia kampuni ya Huawei kutangaza kubuni mfumo wa kujitegemea hadi kutangaza rasmi “Harmony OS 2”, mfumo huo umefuatiliwa sana katika soko la China na imani za wateja wa China. Uchunguzi husika umeonesha kuwa zaidi ya robo moja ya wateja wa China wamesema kwamba watanunua bidhaa husika zinazotumia mfumo wa Harmony mara baada ya mfumo huo kutolewa.

Vyombo vya habari vya kimataifa pia vimepongeza mfumo wa Harmony. Kituo kimoja cha Televisheni nchini Ujerumani kimesema, katika soko la simu za kisasa, mfumo wa Harmony utavunja ukiritimba wa Android na IOS, huku Shirika la Hbari la CNN la Marekani likisema, mfumo wa Harmony utakuwa mshindani rasmi wa Android katika historia.

Jarida la Forbes limesema, lengo la kubuni mfumo wa Harmony sio kuchukua nafasi ya Android, bali ni kuanzisha mfumo halisi wenye uwazi kwa watumiaji wote. Tovuti ya sayansi na teknolojia Ars Technica imesema, mamilioni ya mifumo iliyojaribu kushindana na Android na IOS imeanguka, na mfumo wa Harmony unaoungwa mkono na teknolojia ya Huawei na soko kubwa la China una uwezo mkubwa zaidi kuwa mshindani rasmi wa Android na IOS, ambayo inachukua kiwango cha asilimia 95 cha soko la dunia.

Kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa na kampuni ya IDC, mwaka 2021 idadi ya mauzo ya simu za kisasa kote duniani imefikia bilioni 1.38 na thamani ya mtandao wa IOT wa dunia mwaka 2020 umefikia dola bilioi 690.47 za kimarekani, na inakadiriwa kuwa thamani hiyo itafikia trilioni 1.1 za kimarekani hadi kufikia mwaka 2025. Mtandao wa IOT una mustakabali mzuri, mfumo wa Harmony unaobuni juu ya msingi wa nadharia ya mtandao wa IOT umeweka msingi imara kwa kampuni za teknolojia kuelekea dunia.

Tunapaswa kufahamu kwamba kuvunja vizuizi vilivyowekwa na Marekani si jambo la kipekee la kampuni ya Huawei, ambayo inahusisha siku za baadaye za shughuli ya mtandao wa Internet na mtandao wa IOT.

Bila kujali taifa au kampuni, uvumbuzi wa kisayansi utakuwa kiini cha ushindani. Marekani kuiweka Huawei katika orodha ya vizuizi na kuendelea kuikandamiza katika ushirikiano wa kimataifa wa chip na mfumo wa simu kumethibitisha mara nyingi kwamba, teknolojia kuu haziwezi kupatikana kupitia kuomba na kununua. Kutoka chip, vifaa vipya hadi injini kubwa, mahitaji makubwa ya China kuelekea kuwa nchi yenye uwezo mkubwa wa utengenezaji yako katika orodha ya bidhaa zilizozuiwa na nchi za magharibi.

Rais Xi Jinping wa China amesema, hatuwezi kutegemea matunda ya kisayansi ya wengine kuinua kiwango chetu cha teknolojia, pia hatuwezi kuzifuata nchi nyingine katika sekta ya sayansi na teknolojia. Hatuna chaguo lingine, inabidi kuchukua njia ya kujitegemea na uvumbuzi. China haiwezi kutimiza utandawazi wa kisasa kupitia manunuzi, njia ya kipekee ni kushikilia sera ya kujitegemea kisayansi.
 
Hiyo ni android os iko hivyo na kwa taarifa yako hawawezi kutoboa kwa sababu dunia ya leo bila Google services ni sawa na bure Google services Kwenye hivyo vifaa haisupport anyway ngoja wajuvi wake
 
Mkuu yes china iko vizuri ila ukweli uwekwr wazi kuwa ileni fork ya android OS siyo kwamba katengeneza OS from scratch na wala siyo kweli kwamba ametengeneza kernel yake mpya.
Nimependa ecosystem ya vifaa vya huawei ila pia kitu kingine anasema hata simu na tv zinarun harmony os kitu ambacho siyo kweli. Developers waliopewa access za kufanya developing waligundua ni OS tatu tofauti yani ya simu ni nyingime, ya tv ni nyingne na ya saa ni nyingine.
Ila all in all mchina ni noma.
 
Hiyo ni android os iko hivyo na kwa taarifa yako hawawezi kutoboa kwa sababu dunia ya leo bila Google services ni sawa na bure Google services Kwenye hivyo vifaa haisupport anyway ngoja wajuvi wake
Siyo lazima mbona ios ina run bila hizo google services.
 
Unajitoa ufahamu nahisi...hiyo ios yako kama ingekuwa haikubali Google services sidhani kama leo ingekuwa kwenye soko kwa maana app kama WHATSAPP, INSTAGRAM, FACEBOOK, TWITTER, GMAIL zingekuwa hazifanyi kazi....hiyo OS ya Huawei haikubali Google services na app nilizozitaja hapo juu kwenye hiyo os ni ndoto je wewe unaweza tumia sim isiokuwa na hizo app?tuanzie hapo
 
Hivi mkuu unachozungumza unakijua au unaongea tu mkuu.
Whatsapp, instagram, twitter, facebook haziwezi kuwa affected na google services.
Labda useme kutumia gmail, youtube, playstore n.k
iOS haitumii playstore inaa Appstore, haitumii google maps, google services inazotumia na siyo lazima ni kama mtumiaji anatumia gmail, labda youtube.
Hivyo unaweza kuendelea kudownload whatsapp kwa simu za huawei kutoka kwenye stire nyingine mbali na playstore.
 
Unajitoa ufahamu nahisi...hiyo ios yako kama ingekuwa haikubali Google services sidhani kama leo ingekuwa kwenye soko kwa maana app kama WHATSAPP, INSTAGRAM, FACEBOOK, TWITTER, GMAIL zingekuwa hazifanyi kazi....hiyo OS ya Huawei haikubali Google services na app nilizozitaja hapo juu kwenye hiyo os ni ndoto je wewe unaweza tumia sim isiokuwa na hizo app?tuanzie hapo
Ndio
 
SHIDA HUNA ELIMU NA MAMBO HAYA
 
Kabisa sijui anadhani kisa hizo app anazidownload playstote basi anazimiliki google!
Kuna sehemu nimesema hiz app zinamilikiwa na Google au unatafuta basha kinguvu?
 
Anadhani kila kitu kinamilikiwa na google..hajui watu wengi tu wanatumia iphone na hawatumii kitu chochote cha google..labda kwa baadhi YouTube tu
Kuna sehemu nimesema hizo app zinamilikiwa na Google?au muwasho umekuzidi?
 
Kuna sehemu nimesema hiz app zinamilikiwa na Google au unatafuta basha kinguvu?
Sasa matusi ya nini mkuu unapata faida gani kwa matusi?
We kubali kuwa ulikuwa unachangia mambo usioyaelewa. Whatsapp, Twitter, Facebook, Instagram hazihitaji google services kufanya kazi.
And by the way kuna fork nyingi tu za android hazina google services moja wapo ni ya Amazon na wana app store yao.
iOS haitegemei google services unless kwa wale wanaotumia gmail na Youtube services and other google services.
Kuna KaiOS hii inayokuja kwenye vismart vitochi, haitaji google services kama hutumii huduma na apps za google. Bado ina whatsapp, na apps kibao zinarun mle.
Hivyo ni upotoshaji kusema eti kutumia whatsapp, twitter, facebook, instagram lazima uwe na google services, siyo kweli.
 
Mm napenda china waendelee kukwea pipa tu coz na sisi waafrica tunabebeka kweli maana tunapata vitu kwa unafuu na akitengeza ndege Kama mpango wake wa hapo mbele hakihaki walala hoi tuta onja Radha ya ndege
 
Back
Top Bottom