Harmorapa Fans' Special Thread...

Huyu jamaa ana akili sana!

Anajitoa Ufahamu ili aendelee kuzungumzwa!

Sidhani kama hajui Tofauti ya Man na Woman.
 
Huko kwao wasomi wa elimdunia ni Shida kidogo... Ingekua ile elim nyingine bila shaka angefanikiwa kuimudu
 
Aisee shishi baby ni Profesa wa kiingereza kama tu kimshinda nisha na Harmorapa
 
Japo wawili hao wanatokea upande wa Kusini mwa Tanzania, lakini wameonekana kutopikika katika chungu kimoja. Akiongea katika kipindi cha Joto La Asubuhi leo, Harmorapa ambaye ni hitmaker wa ngoma ya ‘Kiboka ya Mabishoo’ amesema hakuna kolabo yoyote itakuja kutokea kati yake na Harmonize.

“Swala la kufanya kazi na Harmonize hilo halipo.Kila mtu unajua anakuwa na ‘appetite’ na mtu fulani wa kufanya naye kazi,” amesema rapper huyo.

Harmorapa ameongeza kukosea kwake katika lugha ya kingereza, anachukulia kawaida tofauti na watu wanaochukulia jambo la yeye kujiita ‘Strong Woman’ kiukubwa na zaidi kwa kumkejeli.

 
Huyu nae sifa zimemlewesha,kila siku maneno tuuu kwani hawezi kufanya kazi kimya. Anatuchosha
 
Mwambieni jinsi ya kutumia lugha ya Malkia huyo "Strong Woman" sijui women atajua yeye akiona hawezi atumie kimakonde ataelewa zaidi mwishowe atatuambia huyo Harmonise hayuko delicious aisee kama hana appetite what next atasema hayuko delicious
 
Nimesikia Harmorapa nae yuko mbioni kuzindua perfume yake. Watanzania kaeni mkao wa kusubiri
 
itakuwa tulimskia vibaya alikuwa anasema "Strong Human"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…