Japo wawili hao wanatokea upande wa Kusini
mwa Tanzania, lakini wameonekana kutopikika
katika chungu kimoja. Akiongea katika kipindi
cha Joto La Asubuhi leo, Harmorapa ambaye ni
hitmaker wa ngoma ya ‘Kiboka ya Mabishoo’
amesema hakuna kolabo yoyote itakuja kutokea
kati yake na Harmonize.
“Swala la kufanya kazi na Harmonize hilo halipo.
Kila mtu unajua anakuwa na ‘appetite’ na mtu
fulani wa kufanya naye kazi,” amesema rapper
huyo.
Harmorapa ameongeza kukosea kwake katika
lugha ya kingereza, anachukulia kawaida tofauti
na watu wanaochukulia jambo la yeye kujiita
‘Strong Woman’ kiukubwa na zaidi kwa
kumkejeli.
View attachment 499125