kyagata
JF-Expert Member
- Oct 18, 2016
- 10,406
- 19,892
Habari JF,
Kwa wenye uzoefu wa hili jambo naomba mnisaidie ni ishara ya nini?
Siku tatu nyuma nilienda kijijini kwetu kusalimia,sasa kama mjuavyo ndugu kijijini huwa ni wengi na ukifika huko basi ni lazima ujitahidi uwatembelee wote kuepusha lawama.
Kilichonishangaza ni kwamba kuna siku nikawa nimeenda kumsalimia ndugu yangu flani ambae anaishi upande wa pili wa kijiji, na ili ufike huko lazima uvuke mto flani unaotenganisha.
So baada ya kufika huko tukaongea mawili matatu then me nikaaga kuondoka, wakati narudi navuka ule mto nilikuwa mwenyewe tu na sikuona kiumbe mwingine yeyote pale, na lile eneo pale mtoni ni eneo ambalo lina miti mingi sana, ikumbukwe pia muda huo ilikua ni saa 6 mchana.
Kwanza ghafla nikahisi nywele zangu za kichwani zimesisimka na hapo hapo nikaanza kusikia harufu ya manukato, nimeshindwa kuelewa mpaka leo manukato yale yalitoka wapi na kwa nini nywele zangu zilisisimka ghafla?
Asante