Harufu ya manukato porini na nywele kusisimka ina maana gani?

Harufu ya manukato porini na nywele kusisimka ina maana gani?

Habari jf.
Kwa wenye uzoefu wa hili jambo naomba mnisaidie ni ishara ya nini?
Siku tatu nyuma nilienda kijijini kwetu kusalimia,sasa kama mjuavyo ndugu kijijini huwa ni wengi na ukifika huko basi ni lazima ujitahidi uwatembelee wote kuepusha lawama.
Kilichonishangaza ni kwamba kuna siku nikawa nimeenda kumsalimia ndugu yangu flani ambae anaishi upande wa pili wa kijiji,na ili ufike huko lazima uvuke mto flani unaotenganisha.so baada ya kufika huko tukaongea mawili matatu then me nikaaga kuondoka,wakati narudi navuka ule mto nilikua mwenyewe tu na sikuona kiumbe mwingine yeyote pale,na lile eneo pale mtoni ni eneo ambalo lina miti mingi sana,ikumbukwe pia muda huo ilikua ni saa 6 mchana.kwanza ghafla nikahisi nywele zangu za kichwani zimesisimka na hapo hapo nikaanza kusikia harufu ya manukato,nimeshindwa kuelewa mpaka leo manukato yale yalitoka wapi na kwa nini nywele zangu zilisisimka ghafla?
Asante
nishawahi kumuona eneo kama hilo akichana nywele zake ndefu akiwa uchi.Kuniona akashtuka na kuzama mtoni.Nikapita zangu nywele zimenisisimka.
 
Kwa watu wapi sasa akati nimesema nilikua mwenyewe?
Wewe ni demu? Uandishi wako ni wa kike kike. ''akati'' ndiyo nini sasa? Kuna mimea huwa inatoa harufu ya pafyumu. Huko kusisimika nywele ni woga wako tu.
 
Harufu nzuri = manukato toka kwenye maua na mimea pori, hewa ya kijijini mara nyingi haipo contaminated hivyo ni rahisi kwa harufu za maua pori kuweza kuwa absorbed na hewa...

Kusisimuka nywele = ni uoga wako mwenyewe kiasi mwili ukaachilia vichocheo vya adrenaline hivyo kupelekea kitendo kiitwacho piloerection...
 
Wewe ni demu? Uandishi wako ni wa kike kike. ''akati'' ndiyo nini sasa? Kuna mimea huwa inatoa harufu ya pafyumu. Huko kusisimika nywele ni woga wako tu.
Kwa nini mnadharau wanawake,huwezi kunikosoa kistaarabu mpaka uhusishe wanawake?
 
Ilishawahi nitokea, na ilikuwa porini... Nikiwa na umri mdogo, na nina uhakika ile siku niliona kitu ila sikumbuki niliona nini
 
Kwa nini mnadharau wanawake,huwezi kunikosoa kistaarabu mpaka uhusishe wanawake?
Ungejua mimi ni mtu naheshimu wanawake mno mno usingesema hivyo. Kwani huamini kuwa kwenye maisha kuna feminine na masculine way of talking?
 
Harufu nzuri = manukato toka kwenye maua na mimea pori, hewa ya kijijini mara nyingi haipo contaminated hivyo ni rahisi kwa harufu za maua pori kuweza kuwa absorbed na hewa...

Kusisimuka nywele = ni uoga wako mwenyewe kiasi mwili ukaachilia vichocheo vya adrenaline hivyo kupelekea kitendo kiitwacho piloerection...
Haya ndio maelezo sahihi.
 
Back
Top Bottom