Harufu ya manukato porini na nywele kusisimka ina maana gani?

Harufu ya manukato porini na nywele kusisimka ina maana gani?

Sasa unapita kwenye maeneo ya watu na husalimii kwann??
Usirudie tenaa
 
na hii ya kusikia harufu ya viazi vinakanagwa ukipita sehemu mana nishachoka
Viazi sio kweli ila harufu ya ubwabwa mkavu hiyo nimekutana nayo sana kijijini porini. Tena kuna eneo nilikuwa nalijua palikuwa na makuni mazuri yamekauka, ukifika unaokota tu na kurudi nyumbani.

Masharti yake nilipewaga kuwa katika hilo eneo pana nyoka na huyo nyoka inawezekana anakuona.
Unachotakiwa kufanya ni kufanya shida yako iliyokupeleka na kuondoka.
Usioneshe hofu yoyote wala hisia kwamba pale pana nyoka.
Walikuwa wanasema ukiona umeshindwa kuhimili kujiamini na kuchukulia kawaida ni bora usepe mapema.

Ile hali ya kuonesha hofu na mapigo ya moyo kwenda fasta na wakati wewe ndio umeenda hilo eneo, nyoka alikuwa ana uwezo wa kuhisi hofu uliyonayo na anakuchukulia kama hujaenda kwa mema.

Ni imani tu lakini.
 
Wewe ni demu? Uandishi wako ni wa kike kike. ''akati'' ndiyo nini sasa? Kuna mimea huwa inatoa harufu ya pafyumu. Huko kusisimika nywele ni woga wako tu.
Nimea inayotoa harufu si mpaka iguswe! Mimi naijua mimea ambayo ukiigusa tu inatoa harufu chafu mavi yakasome. Ukiikuta pahala unajipitia zako taratibu tu.
 
Habari JF,

Kwa wenye uzoefu wa hili jambo naomba mnisaidie ni ishara ya nini?

Siku tatu nyuma nilienda kijijini kwetu kusalimia,sasa kama mjuavyo ndugu kijijini huwa ni wengi na ukifika huko basi ni lazima ujitahidi uwatembelee wote kuepusha lawama.

Kilichonishangaza ni kwamba kuna siku nikawa nimeenda kumsalimia ndugu yangu flani ambae anaishi upande wa pili wa kijiji, na ili ufike huko lazima uvuke mto flani unaotenganisha.

So baada ya kufika huko tukaongea mawili matatu then me nikaaga kuondoka, wakati narudi navuka ule mto nilikuwa mwenyewe tu na sikuona kiumbe mwingine yeyote pale, na lile eneo pale mtoni ni eneo ambalo lina miti mingi sana, ikumbukwe pia muda huo ilikua ni saa 6 mchana.

Kwanza ghafla nikahisi nywele zangu za kichwani zimesisimka na hapo hapo nikaanza kusikia harufu ya manukato, nimeshindwa kuelewa mpaka leo manukato yale yalitoka wapi na kwa nini nywele zangu zilisisimka ghafla?

Asante
Ulipishana na Jini Maimuna akiwa anaenda kupiga zake misele kashaoga na kujipulizia unyunyu
 
si hivyo tu,
hata kuna baadhi viumbe porini wakipumua, mathalani kujamba au kujikoboa magamba yao hutoa harufu yenye manukato mwanana sana kwa viumbe wengine kuvutika na kusogea karibu, na huo huwa kama mtego wa kuwanasa kama chakula chao 🐒
Asee wanajamba manukato
 
na hyo harufu unadhani ni nn? na huko kusisimka nywele je, hapo kuna mwamba alimgusa tu nywele kwa mbaaal,
Harufu ni manukato yao na ni nzuri kuliko hizi tunazotengeneza sisi zenye spirit.
Mwili ukitizamwa na jini au kupita walipo na wachawi hujua na ndio maana unasisimka.
Kama huyo jamaa angekuwa kapata punda basi punda angepinda na kurudi kwa sababu yeye anawaona majini.
Ukiwa ni mtu wa kusafiri vijijini nyakati za usiku basi bora kutumia punda kuliko gari.
 
Ni uoga tu ikiwa ni pori na uko peke yako, kuhusu harufu, ni kawaida ya miti kutoa maua yenye harufu ya manukato.😀😀😀
 
si hivyo tu,
hata kuna baadhi viumbe porini wakipumua, mathalani kujamba au kujikoboa magamba yao hutoa harufu yenye manukato mwanana sana kwa viumbe wengine kuvutika na kusogea karibu, na huo huwa kama mtego wa kuwanasa kama chakula chao 🐒
Kwahiyo walitaka kumuweka mtu kati jamaa
 
Back
Top Bottom