Harufu ya manukato porini na nywele kusisimka ina maana gani?

Sasa unapita kwenye maeneo ya watu na husalimii kwann??
Usirudie tenaa
 
na hii ya kusikia harufu ya viazi vinakanagwa ukipita sehemu mana nishachoka
Viazi sio kweli ila harufu ya ubwabwa mkavu hiyo nimekutana nayo sana kijijini porini. Tena kuna eneo nilikuwa nalijua palikuwa na makuni mazuri yamekauka, ukifika unaokota tu na kurudi nyumbani.

Masharti yake nilipewaga kuwa katika hilo eneo pana nyoka na huyo nyoka inawezekana anakuona.
Unachotakiwa kufanya ni kufanya shida yako iliyokupeleka na kuondoka.
Usioneshe hofu yoyote wala hisia kwamba pale pana nyoka.
Walikuwa wanasema ukiona umeshindwa kuhimili kujiamini na kuchukulia kawaida ni bora usepe mapema.

Ile hali ya kuonesha hofu na mapigo ya moyo kwenda fasta na wakati wewe ndio umeenda hilo eneo, nyoka alikuwa ana uwezo wa kuhisi hofu uliyonayo na anakuchukulia kama hujaenda kwa mema.

Ni imani tu lakini.
 
Wewe ni demu? Uandishi wako ni wa kike kike. ''akati'' ndiyo nini sasa? Kuna mimea huwa inatoa harufu ya pafyumu. Huko kusisimika nywele ni woga wako tu.
Nimea inayotoa harufu si mpaka iguswe! Mimi naijua mimea ambayo ukiigusa tu inatoa harufu chafu mavi yakasome. Ukiikuta pahala unajipitia zako taratibu tu.
 
Ulipishana na Jini Maimuna akiwa anaenda kupiga zake misele kashaoga na kujipulizia unyunyu
 
si hivyo tu,
hata kuna baadhi viumbe porini wakipumua, mathalani kujamba au kujikoboa magamba yao hutoa harufu yenye manukato mwanana sana kwa viumbe wengine kuvutika na kusogea karibu, na huo huwa kama mtego wa kuwanasa kama chakula chao πŸ’
Asee wanajamba manukato
 
na hyo harufu unadhani ni nn? na huko kusisimka nywele je, hapo kuna mwamba alimgusa tu nywele kwa mbaaal,
Harufu ni manukato yao na ni nzuri kuliko hizi tunazotengeneza sisi zenye spirit.
Mwili ukitizamwa na jini au kupita walipo na wachawi hujua na ndio maana unasisimka.
Kama huyo jamaa angekuwa kapata punda basi punda angepinda na kurudi kwa sababu yeye anawaona majini.
Ukiwa ni mtu wa kusafiri vijijini nyakati za usiku basi bora kutumia punda kuliko gari.
 
Ni uoga tu ikiwa ni pori na uko peke yako, kuhusu harufu, ni kawaida ya miti kutoa maua yenye harufu ya manukato.πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
si hivyo tu,
hata kuna baadhi viumbe porini wakipumua, mathalani kujamba au kujikoboa magamba yao hutoa harufu yenye manukato mwanana sana kwa viumbe wengine kuvutika na kusogea karibu, na huo huwa kama mtego wa kuwanasa kama chakula chao πŸ’
Kwahiyo walitaka kumuweka mtu kati jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…